Kama wewe umeajiriwa au kiongozi huna haki kuwaambia wasio na ajira wajiajiri

ni kweli unavyosema, na huo mtazamo nimeangalia wastani
mf. katika watu 500 wenye kazi binafsi, wangapi wana hadhi sawa na mfanyakazi wa serikali hata wa kada ya chini?
Hadhi gan unazungumzia kupata shikamooo mtaan au tunaangalia pesa mfukoni kwa mfano kada za chini kama ualimu private wanapata pesa ndefu zingine chini ya serikali ni uwajibikaji wako tuu
 
Hadhi gan unazungumzia kupata shikamooo mtaan au tunaangalia pesa mfukoni kwa mfano kada za chini kama ualimu private wanapata pesa ndefu zingine chini ya serikali ni uwajibikaji wako tuu
hivi unajua kama kuna vitu hela haiwezi?
 
Kwahiyo kwa mawazo yako wewe kuajiriwa ni bora kuliko kujiajiri?

Hivi labda nikuulize. Unafanya kazi kwenye kampuni ya fulani. Unakula mshahara kila siku, bima juu na mafao vilevile.

Yeye huyo aliyekuajiri anakuwa anapata nn kiasi cha kukufanya wewe uvimbe tumbo na kusumbua watu mtaani? Fikiri.

Unadhan kila mtu angekuwa na mawazo yako hayo wangapi mngekuwa mmeajiriwa? Mngeajiriwa na serikali wote? Fikiri.

"Employees seek for security while entrepreneurs seek for freedom."

Utumwa mwema.
unapojadili usiwaze kwamba, mtu anapoweka hoja anaweka hoja inayomhusu, kuwaza hivo ni uwezo mdogo wa mijadala, na kwa mantiki hiyo hoja yako na swali lako hazijibiki.

halafu mantiki ya hoja siyo kuajiliwa wala kujiajiri kasome upya kichwa cha habari ili uelewe, kama una uzito kuelewa soma hata mara kumi kwa kutafakari, mwisho utaelewa tu!
 
Kujiajiri ni mawazo binafsi yanayokuja ndani ya Mtu Mwenye macho ya kuziona fulsa zilizopo,hii kauli ya kujiajiri inarudisha maendeleo ya wengi nyuma,coz hawana ubunifu hata wakielekezwa vipi fulsa awazioni,wanabaki kushika na kuacha kisha kile mwisho kuwa na wingu kubwa la mikopo kwenye sakosi na mabenki,HANGALIA FOMULA INAYOKUFAA TUMIA KATIKA MAISHA,Acha na kauli za kisiasa.
mkuu, kichwa cha somo kinahusika!
 
mkuu, kichwa cha somo kinahusika!
MADA:
Neno "kujiajiri" ni neno la kisiasa.

MCHANGO:
Kujiajiri ni mawazo binafsi yanayokuja ndani ya Mtu Mwenye macho ya kuziona fulsa zilizopo,hii kauli ya kujiajiri inarudisha maendeleo ya wengi nyuma,coz hawana ubunifu hata wakielekezwa vipi fulsa awazioni,wanabaki kushika na kuacha kisha kile mwisho kuwa na wingu kubwa la mikopo kwenye sakosi na mabenki,HANGALIA FOMULA INAYOKUFAA TUMIA KATIKA MAISHA,Acha na kauli za kisiasa.
 
Wana Jamii Forums,
watanzania wenzangu, na wengine wanaoishi katika Sheria zinazofanana na za Tanzania.

Ajira siyo kazi, ajira ni mkataba.

wapo wengine wanaofanya kazi sawa na hao walioajiliwa, halafu wanaitwa vibarua,

Na mara nyingi (siyo mara zote) watu huitwa vibarua kabla ya ajira, hii inamaanisha kwamba kuitwa kibarua unaikaribia ajira

Mtu anaefanya kazi binafsi hajafikia hata levo ya kibarua.

Neno "KUJIAJIRI"
ni msemo wa kisiasa tu! na ulianzishwa na wana siasa kutupofusha macho tusipambanue!

kuna "kazi binafsi" "kibarua" na "ajira"
hakuna "ajira binafsi"

kazi binafsi asilimia kubwa ni ndogondogo ambazo ni za kukufanya ule walau ugari na maharage, kukuacha hai usife, ili uendelee kulipa vati kwa ajiri ya mishahara yao hao walioajiliwa

nasema hivi kwa sababu, mtu anaefanya kazi binafsi anakabiliwa na matatizo mengi kuliko aliyeajiriwa.
kwa mfano:
(a) inapotokea akaugua siliasi, hana mdhamini wa kumsafirisha kwenda hospitali za mbali.

(b) heshima katika jamii, kwa walio na kazi binafsi ni ndogo ukilinganisha na waajiriwa, (isipokuwa kwa wachache wenye mafanikio makubwa)

(c) hawana malipo ya mapumziko ya kazi, baada ya kuzeeka, wala hawalipwi overtime

(d)walioajiriwa wanaitwa viongozi, huku wenye kazi binafsi wakiitwa wananchi nk.

hiyo ni baadhi ya mifano niliyoitoa ambayo naona inaweka utofauti baina ya kada hizo mbili, yaani wenye mkataba wa kazi na wasio na mkataba.

karibu kwa hoja
Halafu mwanasiasa huyo huyo anaekuambia ujiajiri, yeye kakimbilia kwenye siasa akijua ndipo mteremko ulipo, yupo radhi akalale kwenye makaburi, au kwenda kwa waganga ili abaki kwenye nafasi hiyo hiyo Maisha yake yote, na sio "kujiajiri"
Mifano mizuri na Mungu anavyowahumbua, tumeanza kuwaona baadhi ya wabunge, yupo radhi hata arudi Chama tawala, au kukabana na kesi ya uchaguzi, iliapate kula yake.,na sio kujiajiri wanakokesha wakihubiri kwenye majukwaa kila baada ya miaka 5.
 
nasema hivi kwa sababu, mtu anaefanya kazi binafsi anakabiliwa na matatizo mengi kuliko aliyeajiriwa.
kwa mfano:
(a) inapotokea akaugua siliasi, hana mdhamini wa kumsafirisha kwenda hospitali za mbali.

(b) heshima katika jamii, kwa walio na kazi binafsi ni ndogo ukilinganisha na waajiriwa, (isipokuwa kwa wachache wenye mafanikio makubwa)

(c) hawana malipo ya mapumziko ya kazi, baada ya kuzeeka, wala hawalipwi overtime

(d)walioajiriwa wanaitwa viongozi, huku wenye kazi binafsi wakiitwa wananchi nk.

hiyo ni baadhi ya mifano niliyoitoa ambayo naona inaweka utofauti baina ya kada hizo mbili, yaani wenye mkataba wa kazi na wasio na mkataba.

karibu kwa hoja
a) health insurance haizuii mtu anaefanya kazi binafsi kujiwekea bima
b)labda jamii yenye upeo mdogo
c)lapf/nssf etc wote wanakaribisha wenye ajira binafsi kujiwekea akiba. Mapumziko ya kazi anaefanya kazi binafsi anajipangia ila alieajiriwa anapangiwa. Yupi ana afadhali hapo?
d)walioajiriwa wanaitwa viongozi? kumbe huko maofisini kuanzia mamesenja hadi meneja wote ni viongozi?

Usisahau unaweza ukawa UMEAJIRIWA na anaefanya kazi binafsi.
 
A)watu walio na kazi binafsi, wasio na mkataba wa kazi kama 80% au zaidi wapo vijijini ambako hata matangazo hayo wakiyasikia ofisi hazipo, labda wasafiri kwanza.

b)kama hujawahi kuishi kijijini inawezekana hilo hulijui, mahala ambapo mtu mmoja tu, anaweza kukupandikizia fitina kwamba wewe ni mchawi hadi ukaogopwa na watu.

c) niambie, ni kata gani Tanzania, ukiondoa kata zilizopo mikoani katikati ya miji ambazo zina ofisi hizo, ukizingatia watu wengi wako mbali na miji (hii kwa mujibu wa utafiti uliotokana na sensa ya mwaka 2012)
 
vipo vitu vingi sana, zikiwemo shughuli za kijamii, hizi hufanyika kwa heshima ya mtu na siyo kwa pesa zake.
mmmh uko mkoa gani mzee?maana Mimi niko iringa na huku tunawadharau sana waliosoma na wana maisha ya kulalamika pia wenye heshima kwa Jamii ni wenye pesa
 
mmmh uko mkoa gani mzee?maana Mimi niko iringa na huku tunawadharau sana waliosoma na wana maisha ya kulalamika pia wenye heshima kwa Jamii ni wenye pesa
uko sahihi, ila msiwadharau, maana "cheo ni dhamana"
lakini zaidi ya yote, haya ninayoyasema hayatokani na mahala fulani tu, na kama unadhani ni hivyo, niambie, hata kata unayoishi wewe je unajua kama wenye pesa ni wachache kuliko waganga njaa?
 
ni kweli unavyosema, na huo mtazamo nimeangalia wastani
mf. katika watu 500 wenye kazi binafsi, wangapi wana hadhi sawa na mfanyakazi wa serikali hata wa kada ya chini?
bas utafiti wako umefanyia vijijini tu na si mjini maan ukianza na wamiliki wengi wa majumba mengi mjini ni hao waliojiajiri,ukija upande wa wamiliki wa biashara asilimia 90 ni hao waliojiajiri hata wamiliki wengi wa magari either ya biashara au kutembelea wengi ni waliojiajiri ...wafanyakazi wengi wamekuja kujenga na kununua japo usafiri baada ya mikopo kufumuka enzi za utawala wa awamu ya nne
 
niliendelea kukujibu ila hata hivyo
hukuelewa mada kasome kichwa cha habari tu, halafu utafakari
 
niliendelea kukujibu ila hata hivyo
hukuelewa mada kasome kichwa cha habari tu, halafu utafakari
nadhani sijaelewa sababu Mimi ni kati ya waliojiajiri n am living ma life ...hata kutafakari nadhani hakuna maana hapa mtaani ninapoishi hakuna wafanyakazi mkuu sina sehem ya kuoanisha hii mada na uhalisia niunao hapa nlipo
 
Neno "kujiajiri" ni neno la kisiasa,
badala ya neno hilo ni "kazi binafsi"
kwa sababu ajira ni mkataba kati ya anaefanya kazi na anaefanyiwa kazi.(mimi pia nina kazi binafsi)

hicho tu ndicho nilichosema, hayo mengine, ya uwiano na maisha ya wahusika niliendekea kujibu kwa kua kujadili kunategemea kuelewa na kueleweka.
 
hapo nmekupata vyema kiongozi
 
Jipe moyo tu mama yangu,na siku hizi mabenki yanataka kusitisha mikopo tutaheshimiana tu.

Mdau kama ulikua uheshimiw hutaheshimiwa tu,kauli ya 'TUTAHESHIMIANA' ni ya watu waliokata tamaa wanaotaman wenzao waanguke ili wawe wote kwenye hali mbaya ya kiuchumi japo hawanufaiki au kuathiriwa na yule aloanguka.
Ni neno linalotamkwa au kuandikwa kwa MTAZAMO WA HINDA
 
Back
Top Bottom