Wahitimu wa kada za Afya walia na Gharama za usajili na kuhuisha leseni kila mwaka. Waomba zifutwe kwa watu wasio na Ajira

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Wadau mbalimbali wa Kada za Afya wametoa malalamiko yao wakiomba Mabaraza ya taaluma ya kada hizo kurejea upya miongozo mbalimbali ya utozaji wa pesa hasa kwa vijana wa kada hizo wasio na ajira.

Mdau mmoja ambaye ni Afisa Tabibu (Clinical Officer) ameeleza kuwa wao hutozwa Tsh. 300,000/= kila mwaka pasipo kujali una ajira au la kwa utaratibu ufuatao-
  1. Enrollment registration Tsh 75,000/=
  2. Renewal practicing license Tsh 75,000/=
  3. Pending debt Tsh 150,000/= ambayo amesema hawaelewi humaanisha nini.
Amebainisha kuwa Kila mwaka huwa ni lazima walipe TSH 75000/= kuhuisha (renew) leseni.

Pia, mdau mwingine wa Kada ya Famasi ngazi ya shahada (Pharmacist) ameeleza kuwa Baraza lao hutoza Tsh. 320,000/= kwa kila mwanafunzi aliyefaulu ili aweze kupata usajili wa kudumu. Aidha, Tsh. 150,000/= hulipwa kila mwisho wa mwaka kama ada ya kuhuisha leseni ili waendelea kubaki kwenye rejesta ya msajili.

Uchunguzi ambao JamiiForums imeufanya umebaini kuwa kada nyingi za Afya zimeyapa mabaraza ya kitaaluma nguvu ya kusajili, kufuta na kufuatilia mienendo ya wanataaluma wake, ambapo hata michango hii inayotajwa hulipwa huko.

Wadau waeleza kuwa kwenye kada za afya, kigezo cha kwanza kupata ajira inabidi uwe na leseni hai (Active licence to practice). Je, kwa ambao hawajapata ajira watawezaje kuajiriwa pamoja na kumudu gharama za kulipia huduma hizi kila mwaka ili waendelee kutambuliwa na mabaraza yao kama wanachama hai?

Wanaomba utaratibu huu ufanyiwe marekebisho, waanze kulipia leseni na kuzihuisha baada ya kupata ajira ili waweze kujimudu kiuchumi.

Wamesema kumtoza mtu gharama kwa huduma ambayo hajatumia ni unyonyaji, pia ni kikwazo kikubwa kwa vijana wasio na ajira kwa kuwa kila nafasi inayotangazwa huwadai wawe wanachama hai kabla hata hawajaanza kutumikia taaluma hiyo.
 
Nilijua ni walim peke yao ndio wanalia na CWT, kumbe hadi watu wa afya?
CWT ni chama Cha wafanyakazi (Walimu).

Hata Afya Kuna vyama vya wafanyakazi n vinakata pesa kila mwezi, kwa wafanyakazi.

LESENI hizo za kila mwaka ni kitu kingine.

Ummy Mwalimu alikuwa anabweka bweka hivi karibuni kuhusu pesa ya Kumuona Daktari mara LESENI, Sasa hivi kapotea haijulikani Yuko busy na Nini Tena.
 
kuna hawa MAT wanakula pesa za madaktari balaa kila mwaka kurenew lisence ni pesa na lazma uwe na CPD point kuanzia 20 na ili upate hizo uhudhurie mafunzo ambayo yanalipiwa si chini ya laki 2
kikubwa serikali itambue kazi ya utabibu sio biashara ni huduma kwanin watu wake wanalipia leseni kama biashara alafu haki ya mtumishi kupata mafunzo kulingana na mabadiriko ya tecnologia ni haki ya msingi aitakiwi kulipiwa
WABUNGE WAKATIE LESENI, MAASKARI NA WANAJESHI WAKATIWE LESENI KAMA MADAKTARI HUU NI UNYANYASAJI,
DAKTARI ANA HAKI ZA MSINGI KAMA AFISA WA SERIKALI WA NGAZI ZA JUU
 
Na bodi yetu ya maabara pia inatusulubu sana asee..., Hapa leseni yangu ime expire tangu mwez wa kwanza.., sasa hiv nawatafutia kibunda cha kurenew....
 
La msingi uwe na ajira au ofis ya kukupatia kipato.., ikiwa hauna mchongo na leseni huna au ime expire inakuwa hatari zaid
 
kuna hawa MAT wanakula pesa za madaktari balaa kila mwaka kurenew lisence ni pesa na lazma uwe na CPD point kuanzia 20 na ili upate hizo uhudhurie mafunzo ambayo yanalipiwa si chini ya laki 2
kikubwa serikali itambue kazi ya utabibu sio biashara ni huduma kwanin watu wake wanalipia leseni kama biashara alafu haki ya mtumishi kupata mafunzo kulingana na mabadiriko ya tecnologia ni haki ya msingi aitakiwi kulipiwa
WABUNGE WAKATIE LESENI, MAASKARI NA WANAJESHI WAKATIWE LESENI KAMA MADAKTARI HUU NI UNYANYASAJI,
DAKTARI ANA HAKI ZA MSINGI KAMA AFISA WA SERIKALI WA NGAZI ZA JUU
Hatar sana mkuu,
 
Back
Top Bottom