Ndio kazi ya serikali kuelimisha jamii,hebu tumia akili kwa hiyo daktari mwenye ukimwi asiwaambie watu ukimwi unaua kwa kuwa tu anao ukimwi,Sasa kama waziri kaajiriwa akae kimya kisa yeye anaajira,Nini maana ya serikali sasaTatizo la ajira ni kubwa sana katika nchi yetu na dunia kwa ujumla. Lakini kuna kauli ambazo mimi binafsi huwa zinanikera sana kuzisikia kutoka kwa viongozi wetu na watu walioajiriwa. Utasikia mathalani mtu aliyeajiriwa au kiongozi wakisema mathalani: Ni aibu kwa msomi wa chuo kikuu kulalamika kuwa hana ajira, vijana wajiajiri, nk nk. Sasa swali la kujiuliza hapa ni hili. Huyu mtu kasomea kwa mfano ualimu. Sasa anajiajiri ki vipi? Anaanzisha shule? Mwingine kasomea udaktari. Je huyu anaanzisha dispensary?
Kinachokera ni kuwa utakuta anayesema wenzake wajiajiri yeye mwenyewe kaajiriwa au ni kiongozi kama mbunge, waziri au rais aliyeajiriwa na umma. Maana yake ni kuwa yeye mwenyewe ameshindwa kujiajiri ikabidi aajiriwe au aombe uongozi kama sehemu ya ajira yake. Watu kama akina Mengi au Bahresa wakisema hivi wanaeleweka kwakuwa wao wenyewe ni mifano hai na wana udhu wa kuwaelimisha wasio na ajira kujiajiri lakini wengine wanaposema hivyo inakuwa kama kejeli tu kwa watu wasio na ajira.
Ninyi mlioajiriwa kwenye taasisi mbali mbli na mashirika ikiwa ni pamoja na viongozi wa kisiasa acheni kujiona ninyi ndio mnajua zaidi kuwaambia wenzenu wasiokuwa na ajira eti ni aibu kulalamika hawana ajira badala ya kujiajiri. Kama ni rahisi kiasi hicho hebu achieni hizo nafasi ili wasio na ajira wazishike na nanyi mkajiajiri muone kama ni rahisi kama manavyosema. Na mlivyokuwa wabinafsi utakuta wengine mnastaafu badala yakujiajiri bado mnazengea ajira za mikataba na wengine mnazengea nafasi ya kuteuliwa kama uDC, RC, uenyekiti wa bodi nk hivyo kuendelea kuziba nafasi za wasiokuwa na ajira. Na kwakuwa system imeshikwa na ninyi wenyewe hata mteauji anaacha wasio na ajira anateua walio staafu. Ndio utasikia Kanali, Meja, Kepteni mstaafu Mkuu wa Mkoa au Wilaya fulani. Acheni kejeli na nyamazeni kimya kwasababu ninyi wenyewe mmeshindwa kujiajiri ndio maana mnategemea mishahara na posho!
Nimejaribu,kuonyesha mantiki ya kujiajiri au kuajiriwa sio hoja ya kutaka kila mtu ajiajiri maana sahizi umekuwa kama wimbo kila MTU anakwambia bora kujiajiri kiukweli hatuwezi kuajiriwa wote na atuwezi kujiajiri wote,wapo waliojiajiri awajatoka kimaisha na wapo walioajiriwa wametoka kimaisha pia kinyume chake.so ni ya Mungu anayepanga maisha,kauli za wanasiasa kwamba watu wajiajiri ni kutokana nchi kutokua na ajira kwahiyo ili kukunyamazisha usidai ajira ndipo wanaporeta Sera ya kujiajiri,na kauli kma hizi zinapatikana kwa hata kwa wazazi walioshindwa kuandaa maisha ya watoto,utakuta wanawaambia wajitaidi kutafuta kwani hata wao baba zao awakuwaachia kitu,lakini aliyenacho atamwambia mwanaye ajitaidi kuendeleza,kauli ya jiajiri ni ya MTU aliyeshindwa kukusaidia sasa anataka ujisaidie mwenyewe huku akijitaidi asionekane awezi kukusaidia.sijatoka kwenye somo.mkuu, kichwa cha somo kinahusika!
Nimejaribu,kuonyesha mantiki ya kujiajiri au kuajiriwa sio hoja ya kutaka kila ajiajiri maana sahizi umekuwa kama wimbo kila MTU anakwambia bora kujiajiri kiukweli hatuwezi kuajiriwa wote na atuwezi kujiajiri wote,wapo waliojiajiri awajatoka kimaisha na wapo walioajiriwa wametoka kimaisha pia kinyume chake.so ni ya Mungu anayepanga maisha,kauli za wanasiasa kwamba watu wajiajiri ni kutokana nchi kutokua na ajira kwahiyo uli kukunyamazisha usidai ajira ndipo wanaporeta Sera ya kujiajiri,na kauli kma. His zinapatikana kwamkuu, kichwa cha somo kinahusika!
si ndo hapo mkuu af utakuta nae alikua anatupigia kelele tujiajiriHata yule mkubwa wa Mkoa wa Moro angeweza Kujiajiri asingelialia
Wassira kila siku kiguu na njia mahakamani.hao wanaoshauri watu waji ajiri waki staf wanarudi mtaani na kiinua mgongo milioni zaidi ya 70 mwaka hauishi hana hata buku anapata bp anakufa.
Hiyo ni kweli tupu.Tatizo la ajira ni kubwa sana katika nchi yetu na dunia kwa ujumla. Lakini kuna kauli ambazo mimi binafsi huwa zinanikera sana kuzisikia kutoka kwa viongozi wetu na watu walioajiriwa. Utasikia mathalani mtu aliyeajiriwa au kiongozi wakisema mathalani: Ni aibu kwa msomi wa chuo kikuu kulalamika kuwa hana ajira, vijana wajiajiri, nk nk. Sasa swali la kujiuliza hapa ni hili. Huyu mtu kasomea kwa mfano ualimu. Sasa anajiajiri ki vipi? Anaanzisha shule? Mwingine kasomea udaktari. Je huyu anaanzisha dispensary?
Kinachokera ni kuwa utakuta anayesema wenzake wajiajiri yeye mwenyewe kaajiriwa au ni kiongozi kama mbunge, waziri au rais aliyeajiriwa na umma. Maana yake ni kuwa yeye mwenyewe ameshindwa kujiajiri ikabidi aajiriwe au aombe uongozi kama sehemu ya ajira yake. Watu kama akina Mengi au Bahresa wakisema hivi wanaeleweka kwakuwa wao wenyewe ni mifano hai na wana udhu wa kuwaelimisha wasio na ajira kujiajiri lakini wengine wanaposema hivyo inakuwa kama kejeli tu kwa watu wasio na ajira.
Ninyi mlioajiriwa kwenye taasisi mbali mbli na mashirika ikiwa ni pamoja na viongozi wa kisiasa acheni kujiona ninyi ndio mnajua zaidi kuwaambia wenzenu wasiokuwa na ajira eti ni aibu kulalamika hawana ajira badala ya kujiajiri. Kama ni rahisi kiasi hicho hebu achieni hizo nafasi ili wasio na ajira wazishike na nanyi mkajiajiri muone kama ni rahisi kama manavyosema. Na mlivyokuwa wabinafsi utakuta wengine mnastaafu badala yakujiajiri bado mnazengea ajira za mikataba na wengine mnazengea nafasi ya kuteuliwa kama uDC, RC, uenyekiti wa bodi nk hivyo kuendelea kuziba nafasi za wasiokuwa na ajira. Na kwakuwa system imeshikwa na ninyi wenyewe hata mteauji anaacha wasio na ajira anateua walio staafu. Ndio utasikia Kanali, Meja, Kepteni mstaafu Mkuu wa Mkoa au Wilaya fulani. Acheni kejeli na nyamazeni kimya kwasababu ninyi wenyewe mmeshindwa kujiajiri ndio maana mnategemea mishahara na posho!
True, wale watoto wa vigogo waliojazana kule BOT walishindwa nini kujiajiri?Wanawatafutia watoto wao kazi,ila watoto wa masikini wanawaambia wajiajiri