Kama wewe umeajiriwa au kiongozi huna haki kuwaambia wasio na ajira wajiajiri

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,303
12,962
Tatizo la ajira ni kubwa sana katika nchi yetu na dunia kwa ujumla. Lakini kuna kauli ambazo mimi binafsi huwa zinanikera sana kuzisikia kutoka kwa viongozi wetu na watu walioajiriwa. Utasikia mathalani mtu aliyeajiriwa au kiongozi wakisema mathalani: Ni aibu kwa msomi wa chuo kikuu kulalamika kuwa hana ajira, vijana wajiajiri, nk nk. Sasa swali la kujiuliza hapa ni hili. Huyu mtu kasomea kwa mfano ualimu. Sasa anajiajiri ki vipi? Anaanzisha shule? Mwingine kasomea udaktari. Je huyu anaanzisha dispensary?

Kinachokera ni kuwa utakuta anayesema wenzake wajiajiri yeye mwenyewe kaajiriwa au ni kiongozi kama mbunge, waziri au rais aliyeajiriwa na umma. Maana yake ni kuwa yeye mwenyewe ameshindwa kujiajiri ikabidi aajiriwe au aombe uongozi kama sehemu ya ajira yake. Watu kama akina Mengi au Bahresa wakisema hivi wanaeleweka kwakuwa wao wenyewe ni mifano hai na wana udhu wa kuwaelimisha wasio na ajira kujiajiri lakini wengine wanaposema hivyo inakuwa kama kejeli tu kwa watu wasio na ajira.

Ninyi mlioajiriwa kwenye taasisi mbali mbli na mashirika ikiwa ni pamoja na viongozi wa kisiasa acheni kujiona ninyi ndio mnajua zaidi kuwaambia wenzenu wasiokuwa na ajira eti ni aibu kulalamika hawana ajira badala ya kujiajiri. Kama ni rahisi kiasi hicho hebu achieni hizo nafasi ili wasio na ajira wazishike na nanyi mkajiajiri muone kama ni rahisi kama manavyosema. Na mlivyokuwa wabinafsi utakuta wengine mnastaafu badala yakujiajiri bado mnazengea ajira za mikataba na wengine mnazengea nafasi ya kuteuliwa kama uDC, RC, uenyekiti wa bodi nk hivyo kuendelea kuziba nafasi za wasiokuwa na ajira. Na kwakuwa system imeshikwa na ninyi wenyewe hata mteauji anaacha wasio na ajira anateua walio staafu. Ndio utasikia Kanali, Meja, Kepteni mstaafu Mkuu wa Mkoa au Wilaya fulani. Acheni kejeli na nyamazeni kimya kwasababu ninyi wenyewe mmeshindwa kujiajiri ndio maana mnategemea mishahara na posho!
 
Binafsi huwa ninawadhalau sana hao watu maana wanazungumzia mambo ambayo wao hawawezi kuyafanya, mathalani watazame wengi wakistaafu hushindwa hata kudumu wakipambana na magumu tu ya kitaani hujifia zao.

Kweli alieshiba hamjui mwenyewe njaa.HII NDIO TANZANIA
 
Tatizo la ajira ni kubwa sana katika nchi yetu na dunia kwa ujumla. Lakini kuna kauli ambazo mimi binafsi huwa zinanikera sana kuzisikia kutoka kwa viongozi wetu na watu walioajiriwa. Utasikia mathalani mtu aliyeajiriwa au kiongozi wakisema mathalani: Ni aibu kwa msomi wa chuo kikuu kulalamika kuwa hana ajira, vijana wajiajiri, nk nk. Sasa swali la kujiuliza hapa ni hili. Huyu mtu kasomea kwa mfano ualimu. Sasa anajiajiri ki vipi? Anaanzisha shule? Mwingine kasomea udaktari. Je huyu anaanzisha dispensary?

Kinachokera ni kuwa utakuta anayesema wenzake wajiajiri yeye mwenyewe kaajiriwa au ni kiongozi kama mbunge, waziri au rais aliyeajiriwa na umma. Maana yake ni kuwa yeye mwenyewe ameshindwa kujiajiri ikabidi aajiriwe au aombe uongozi kama sehemu ya ajira yake. Watu kama akina Mengi au Bahresa wakisema hivi wanaeleweka kwakuwa wao wenyewe ni mifano hai na wana udhu wa kuwaelimisha wasio na ajira kujiajiri lakini wengine wanaposema hivyo inakuwa kama kejeli tu kwa watu wasio na ajira.

Ninyi mlioajiriwa kwenye taasisi mbali mbli na mashirika ikiwa ni pamoja na viongozi wa kisiasa acheni kujiona ninyi ndio mnajua zaidi kuwaambia wenzenu wasiokuwa na ajira eti ni aibu kulalamika hawana ajira badala ya kujiajiri. Kama ni rahisi kiasi hicho hebu achieni hizo nafasi ili wasio na ajira wazishike na nanyi mkajiajiri muone kama ni rahisi kama manavyosema. Na mlivyokuwa wabinafsi utakuta wengine mnastaafu badala yakujiajiri bado mnazengea ajira za mikataba na wengine mnazengea nafasi ya kuteuliwa kama uDC, RC, uenyekiti wa bodi nk hivyo kuendelea kuziba nafasi za wasiokuwa na ajira. Na kwakuwa system imeshikwa na ninyi wenyewe hata mteauji anaacha wasio na ajira anateua walio staafu. Ndio utasikia Kanali, Meja, Kepteni mstaafu Mkuu wa Mkoa au Wilaya fulani. Acheni kejeli na nyamazeni kimya kwasababu ninyi wenyewe mmeshindwa kujiajiri ndio maana mnategemea mishahara na posho!

Ni kweli kabisa mkuu nakubaliana nausemi usemao "aliye Shiba hamjui mwenye njaa
 
hao wanaoshauri watu waji ajiri waki staf wanarudi mtaani na kiinua mgongo milioni zaidi ya 70 mwaka hauishi hana hata buku anapata bp anakufa.
 
Wana Jamii Forums,
Watanzania wenzangu, na wengine wanaoishi katika Sheria zinazofanana na za Tanzania.

Ajira siyo kazi, ajira ni mkataba.

Wapo wengine wanaofanya kazi sawa na hao walioajiriwa, halafu wanaitwa vibarua,

Na mara nyingi (siyo mara zote) watu huitwa vibarua kabla ya ajira, hii inamaanisha kwamba kuitwa kibarua unaikaribia ajira

Mtu anaefanya kazi binafsi hajafikia hata levo ya kibarua.

Neno "KUJIAJIRI"
Ni msemo wa kisiasa tu! na ulianzishwa na wanasiasa kutupofusha macho tusipambanue!

Kuna "kazi binafsi" "kibarua" na "ajira"
hakuna "ajira binafsi"

Kazi binafsi asilimia kubwa ni ndogondogo ambazo ni za kukufanya ule walau ugali na maharage, kukuacha hai usife, ili uendelee kulipa VAT kwa ajili ya mishahara yao hao walioajiriwa

Nasema hivi kwa sababu, mtu anayefanya kazi binafsi anakabiliwa na matatizo mengi kuliko aliyeajiriwa.
kwa mfano:

(a) Inapotokea akaugua sirias, hana mdhamini wa kumsafirisha kwenda hospitali za mbali.

(b) Heshima katika jamii, kwa walio na kazi binafsi ni ndogo ukilinganisha na waajiriwa, (isipokuwa kwa wachache wenye mafanikio makubwa)

(c) Hawana malipo ya mapumziko ya kazi, baada ya kuzeeka, wala hawalipwi overtime

(d)Walioajiriwa wanaitwa viongozi, huku wenye kazi binafsi wakiitwa wananchi nk.

Hiyo ni baadhi ya mifano niliyoitoa ambayo naona inaweka utofauti baina ya kada hizo mbili, yaani wenye mkataba wa kazi na wasio na mkataba.

Karibu kwa hoja
 
binafsi naona hoja zako zimejikita kulinganisha small scale ajira binafsi na watumishi wa serikali ungeangalia kwa upana wake na ngazi zote za ajira binafsi then upangilie hoja zako
Wana Jamii Forums,
watanzania wenzangu, na wengine wanaoishi katika Sheria zinazofanana na za Tanzania.

Ajira siyo kazi, ajira ni mkataba.

wapo wengine wanaofanya kazi sawa na hao walioajiliwa, halafu wanaitwa vibarua,

Na mara nyingi (siyo mara zote) watu huitwa vibarua kabla ya ajira, hii inamaanisha kwamba kuitwa kibarua unaikaribia ajira

Mtu anaefanya kazi binafsi hajafikia hata levo ya kibarua.

Neno "KUJIAJIRI"
ni msemo wa kisiasa tu! na ulianzishwa na wana siasa kutupofusha macho tusipambanue!

kuna "kazi binafsi" "kibarua" na "ajira"
hakuna "ajira binafsi"

kazi binafsi asilimia kubwa ni ndogondogo ambazo ni za kukufanya ule walau ugari na maharage, kukuacha hai usife, ili uendelee kulipa vati kwa ajiri ya mishahara yao hao walioajiliwa

nasema hivi kwa sababu, mtu anaefanya kazi binafsi anakabiliwa na matatizo mengi kuliko aliyeajiriwa.
kwa mfano:
(a) inapotokea akaugua siliasi, hana mdhamini wa kumsafirisha kwenda hospitali za mbali.

(b) heshima katika jamii, kwa walio na kazi binafsi ni ndogo ukilinganisha na waajiriwa, (isipokuwa kwa wachache wenye mafanikio makubwa)

(c) hawana malipo ya mapumziko ya kazi, baada ya kuzeeka, wala hawalipwi overtime

(d)walioajiriwa wanaitwa viongozi, huku wenye kazi binafsi wakiitwa wananchi nk.

hiyo ni baadhi ya mifano niliyoitoa ambayo naona inaweka utofauti baina ya kada hizo mbili, yaani wenye mkataba wa kazi na wasio na mkataba.

karibu kwa hoja
 
binafsi naona hoja zako zimejikita kulinganisha small scale ajira binafsi na watumishi wa serikali ungeangalia kwa upana wake na ngazi zote za ajira binafsi then upangilie hoja zako
hilo la ajira binafsi silitambui na nimelipinga, lakini pia mlinganyo uliopo siyo wa viwago vya kazi, ni wa viwango vya kipato na heshima ya kazi husika.
 
ok nmekupata mkuu ila umeliangalia kwa level ya chini sana hili suala la kazi binafsi kama unavolitambua wewe
ni kweli unavyosema, na huo mtazamo nimeangalia wastani
mf. katika watu 500 wenye kazi binafsi, wangapi wana hadhi sawa na mfanyakazi wa serikali hata wa kada ya chini?
 
Kwahiyo kwa mawazo yako wewe kuajiriwa ni bora kuliko kujiajiri?

Hivi labda nikuulize. Unafanya kazi kwenye kampuni ya fulani. Unakula mshahara kila siku, bima juu na mafao vilevile.

Yeye huyo aliyekuajiri anakuwa anapata nn kiasi cha kukufanya wewe uvimbe tumbo na kusumbua watu mtaani? Fikiri.

Unadhan kila mtu angekuwa na mawazo yako hayo wangapi mngekuwa mmeajiriwa? Mngeajiriwa na serikali wote? Fikiri.

"Employees seek for security while entrepreneurs seek for freedom."

Utumwa mwema.
 
% % kabisaa yaani ni sawa na mzazi aliyeshindwa kuandaa maisha kwajiri ya mtoto wake alafu anamwambia komaa hata Mimi babu yako hakuniachia kitu ujinga .mtupu
 
Kujiajiri ni mawazo binafsi yanayokuja ndani ya Mtu Mwenye macho ya kuziona fulsa zilizopo,hii kauli ya kujiajiri inarudisha maendeleo ya wengi nyuma,coz hawana ubunifu hata wakielekezwa vipi fulsa awazioni,wanabaki kushika na kuacha kisha kile mwisho kuwa na wingu kubwa la mikopo kwenye sakosi na mabenki,HANGALIA FOMULA INAYOKUFAA TUMIA KATIKA MAISHA,Acha na kauli za kisiasa.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom