Kama wewe ni "mvivu wa akili" usisome andiko hili (Fanya mambo mengine)

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaandika Malisa Godlisten
Kama wewe ni "mvivu wa akili" usisome andiko hili (Fanya mambo mengine).!
____________
Tangu juzi nimekuwa nikiandika na kufuta. Nimejizuia sana kusema lakini nimeona niseme japo kwa "kifupi" kwa sababu kukaa kimya katikati ya uovu ni kuunga mkono uovu huo. Polisi wameua tena. This time wamemuua binti mdogo asiye na hatia, Aquilina B. Aqueline mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kozi ya ugavi (Bachelor degree in Procurement) chuo cha NIT. Huko nyuma Polisi wamewahi kuua tena watu kadhaa wasio na hatia.

Mwaka 2011, Polisi waliwaua bila hatia vijana watatu ambao ni Denis Shirima, Omary Ismail na raia wa Kenya, Paul Njuguna kwenye maandamano ya Chadema yaliyofanyika Janary 05, mwaka 2011 jijini Arusha. Vijana hao hawakuwa kwenye maandamano, walikuwa kwenye shughuli zao za kuwapatia kipato, kwa mfano Shirima yeye alikua gereji lakini risasi ikamfuata hukohuko na kumuua. Sikumbuki kama kuna polisi waliowajibishwa kwa mauaji hayo.

Mwaka 2012, Polisi walimuua bila hatia kijana Ally Zona mfanyabiashara ndogondogo pale Msamvu Morogoro. As usual Zona naye hakuwa kwenye maandamano. Alikua kwenye shughuli zake za kujitafutia riziki, risasi ikamfuata hukohuko, ikampiga kichwani akafa. Sikumbuki kama kuna askari aliyechukuliwa hatua kwa mauaji hayo.

Mwaka 2012, Polisi walimuua bila hatia mwandishi Daudi Mwangosi pale Nyololo akiwa ktk shughuli zake za kikazi. Akiwa na camera na kalamu tu mkononi, Mwangosi alipigwa bomu na kugeuka mapande ya nyama ndani ya sekunde chache.

Askari polisi, Bw.Picifius Simo aliyefyatua bomu hilo alihukumiwa miaka 15 gerezani, lakini aliyempa order ya kufyatua hakuwajibishwa. Ikumbukwe polisi hawafanyi kazi bila order, lakini ajabu ni kuwa mkuu wa kikosi hakuguswa, OCD wa Mufindi hakuguswa wala RPC Iringa Kamuhanda ambaye alikua eneo la tukio hakuchukuliwa hatua yoyote. Badala yake Kamuhanda alipandishwa cheo kutoka SACP kuwa DCP miezi michache baada ya polisi wake kumuua Mwangosi.

Mwaka 2006, Polisi waliwaua wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge Morogoro, na kudai kuwa walikua majambazi. Lakini Tume ya Jaji Kipenka ilipochunguza ilibaini kuwa watu hao hawakuwa majambazi. Walikua ni wafanyabiashara wa madini na polisi waliwaua ili kuwapora fedha na madini waliyokua nayo. Jaji Kipenka alieleza kuwa Polisi waliwafunga mikono na miguu na kuwafunika vitambaa vyeusi usoni kisha kuwapiga risasi wote watatu pamoja na dereva wao.

Baada ya hapo Polisi wakapora madini waliyokua nayo, pamoja na kiasi cha pesa kinachokadiriwa kuwa milioni 200. Just imagine ukatili huu unafanywa na polisi. Badala ya kulinda raia na mali zao, waliua raia na kupora mali zao.

Ripoti ya Jaji Kipenka iliifanya taifa kuzizima kwa uchungu kwani hakuna mtu ambaye alitegemea Polisi kufanya unyama wa aina hiyo. Bahati mbaya kamanda Zombe aliyetoa amri ya kuuawa wafanya biashara hao aliachiwa huru na mahakama baada ya Jamhuri kukosea charge sheet na kumshtaki kwa kosa la kuua (murder) badala ya kosa la kusaidia kuua.

Kwa kifupi orodha ya matukio ya polisi kuua raia wasio na hatia ni ndefu sana. Bahati mbaya juzi wameendeleza orodha hiyo, kwa kumuua Aquilina, binti mdogo ambaye wala hakuwa kwenye maandamano ya Chadema.

Kama kawaida hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa hadi sasa. Askari aliyemfyatulia risasi Aquilina bado yupo kazini, OCD bado yupo kazini, RPC bado yupo kazini, na Kamanda kanda maalumu bado yupo kazi. Ajabu ni kwamba hata waziri wa mambo ya ndani ambaye alipaswa kuwa wa kwanza kuwajibika kisiasa bado yupo ofisini. Ni kama vile hakuna jambo lolote lililotokea. Maisha yanaendelea. Who cares??

Kamanda Mambosasa amefanya press jana. Nilitegemea baada ya Press angetangaza kuwajibika kwa kuwa Askari wake wamefanya makosa yaliyogharimu uhai wa watu, kwa sababu HAPAKUWA NA SABABU YOYOTE kwa Polisi kutumia silaha za moto kuzima maandamando hayo. Busara ya kiongozi unakiri sabordinates wako wamekosea kisha unawajibika, kama Mwinyi alivyofanya mwaka 1994.

Lakini Mambosasa akaishia kuelezea tukio hilo lilivyotokea. Akasema polisi hawakulenga kumpiga mtu risasi badala yake walikua wakirusha juu ili kuwatawanya waandamanaji.

Lakini ukimtizama Aquilina amepigwa risasi ya kichwa juu kidogo ya sikio. Nashindwa kuelewa risasi iliyorushwa juu inawezaje kushuka hadi usawa wa gari ikakata kona na kuingia kwenye kioo kisha ikampata Aquilina. The Law of Gravitational Force inanizuia kuamini majibu haya ya Mambosasa.

Hata hivyo ukimuacha Aquilina kuna vijana wengine watatu nao walipigwa risasi. Wawili risasi za paja, na mmoja risasi ya mguu. Hapa napo nashindwa kuelewa risasi zilizopigwa juu ziliwezaje kurudi chini na kumvunja mtu mguu au kumjetuhi paja?

Nadhani Mambosasa aache kufocha ukweli. Jambo hili linahusu uhai wa watu, let him be serious. Akiri kwamba Polisi wake walifanya makosa kwa kufyatua risasi kiholela zikaua na kujeruhi watu wasio na hatia. Kutoa "story" mara risasi zilipigwa juu zikashuka chini ni kujaribu kuhalalisha mauaji haya ya kikatili. Lakini ukweli ni kwamba hakuna sababu yoyote inayoweza kujiustify mauaji haya wala kujustify polisi kutumia risasi kutawanya watu ambao hawakua hata na wembe mkononi.

Nimeona watu wengi wakilaumu mauaji yaliyotokea, lakini wanasahau kwamba mauaji ni matokeo tu. Kinachopaswa kulaumiwa ni matumizi mabaya ya silaha whether imeua au haikuua. Polisi wamefyatua risasi nyingi sana zikawapata watu wanne. Mmoja akafa, watatu wakajeruhiwa. Hao waliojeruhiwa wangeweza kufa pia kama alivyokufa Aquilina. So tunachopaswa kulaumu hapa ni ujinga wa Polisi kufyatua risasi hovyo hata kama hazijaua. Tusisubiri ziue ndipo tulaani.

Polisi hana mamlaka yoyote kisheria kuua watu wanaoandamana kwa amani bila kufanya fujo. Haijalishi hayo maandamano yana kibali au hayana kibali si ruhusa polisi kuua. Hawana hiyo mamlaka. Polisi kujitetea kwamba walipiga risasi kwa sababu watu waliandamani bila kibali ni utetezi dhaifu sana na usiokubalika popote duniani.

Kwenye social ethics kuna kitu kinaitwa "lesser evil" yani kama una mambo mawili ambayo yote ni makosa na ni lazima ufanye moja, basi chagua kosa lenye madhara madogo zaidi. Kwa mfano Chadema kuandamana bila kibali ni kosa, na kuwafyatulia risasi ili kuwatawanya ni kosa. Kama kiongozi una busara unafanya "impact assesment" kati ya makosa haya mawili ni lipi lenye madhara makubwa.

Kuwaacha Chadema waandamane (bila kibali) madhara yake ni kwamba daladala zitachelewa kufika vituoni maana barabara itakuwa "busy" kwa muda. Lakini kuwafyatulia risasi ili kuwatawanya madhara yake ni kwamba watu watakufa na wengine kujeruhiwa na kupata ulemavu wa kudumu. So kama kiongozi wa Polisi ana akili, atapima kati ya daladala kuchelewa, na watu kufa/kujeruhiwa/kupata ulemavu which is the lesser evil, then anachagua kufanya the lesser evil. Bahati mbaya baadhi ya polisi shule hamna, busara hamna, hekima hamna. So kujua mambo kama haya ni msamiati mgumu kwao.

Vyovyote iwavyo haki ya mtu ya kuishi inapaswa kulindwa kwa namna yoyote ile. Japokuwa kisheria haki zote ni sawa lakini haki ya kuishi ni haki mama kwa sababu haki nyingine zote zinabebwa na haki hii. Ukinyimwa haki ya kuishi obviously unapoteza na haki nyingine zote. Bahati mbaya vyombo vilivyopewa dhamana ya kulinda haki ya raia kuishi ndivyo vinavyoua raia. Paradox.!!

Kwa hili tukio la kuuawa kwa Aquilina na kujeruhiwa kwa wengine watatu Jeshi la Polisi linabeba sehemu kubwa ya lawama, na viongozi wa jeshi hilo poja na askari aliyefyatua risasi wote wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria na za kinidhamu.

Lakini lawama nyingine zinakwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aaron Karugumujuli (kada wa CCM) aliyeamua kuweka mbele maslahi ya chama chake kuliko maisha ya watanzania. Huyu angetoa viapo mapema Aquilina asingeuawa wala wanachama wa Chadema wasingejeruhiwa kwa risasi na kuachwa na vilema vya kudumu. Huyu ndiye chanzo cha matatizo yote.

Ikumbukwe Chadema wamefuatilia viapo ofisini kwake zaidi ya wiki moja akiwazungusha tu. Hadi siki ya ijumaa jioni mawakala hawana viapo na kesho yake asubuhi kura zinapigwa. Huyu Aaron amebeba sehemu kubwa ya damu ya Aquilina pamoja na watanzania waliojeruhiwa kwa risasi na kupewa vilemavya kudumu.

Lawama zingine zinakwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambayo ilipewa malalamiko juu ya Aaron lakini haikuchukua hatua zozote.

Pia Chama cha mapinduzi hakiwezi kuepuka lawama kwa sababu Aaron ni kada wake na alikua anahujumu uchaguzi kwa faida ya CCM.

[HASHTAG]#NiniKifanyike[/HASHTAG];

1. Rais JPM atoe kauli ya kuonesha kusikitishwa na ukatili huu wa polisi. Yeye ndiye baba yetu na mfariji mkuu wa taifa letu (Comforter In-Chief). Tunamtaka aseme neno litakalogusa mioyo iliyopondeka ya wanafamilia wa Aquilina, na majeruhi waliopigwa risasi kwa uzembe wa Polisi, ikiwezekana awatembelee hospitalini. Kama alitoa pole kwa familia ya Tsvangirai na kuonesha kuumizwa na kifo hicho, naamini atakuwa ameumizwa zaidi na kifo cha kikatili cha Aquilina.

2. Serikali iubebe msiba wa Aquilina na kufanya azimio la pamoja la kitaifa kwamba mauaji ya aina hii hayatatokea tena nchini.

3. Serikali igharamie matibabu ya watu watatu waliojeruhiwa kwa risasi na kusababishiwa ulemavu wa kudumu.

4. Waziri wa mambo ya Ndani ajiuzulu kuonesha uwajibikaji. Asipofanya hivyo Rais amuwajibishe kwa kumfita kazi. Matukio mengi ya kuogofya yametokea kipindi Mwigulu akiwa Waziri wa mambo ya ndani na hakuna hatua za maana alizochukua. Baadhi ya matukio hayo ni kama kupotea kwa Ben Saanane, kutekwa na kuuawa kinyama kwa Katibu wa Chadema kata ya Hanabasif na maiti yake kutupwa ufukwe wa Coco, kupotea kwa Mwandishi Azory etc.

5. Askari Polisi wote waliofyatua risasi (whether ziliua, kujeruhi, au hata kama hazikumpata mtu) wafukuzwe kazi na kufikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya silaha. Pia aliyetoa order ya risasi kufyatuliwa nae aunganishwe kwenye kesi.

6. Safu ya uongozi wa polisi kanda maalumu ya Dar na mikoa yake ya kipolisi ifumuliwe. Miezi michache ya Mambosasa ameprove failure kubwa hasa jinsi ya kudeal na wanasiasa. Polisi wameonesha double standatd za waziwazi ktk baadhi ya maamuzi. Atafutiwe nafasi nyingine.

7. Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni afukuzwe kazi au apangiwe kazi nyingine ambayo haitamuweka kwenye "conflict of intetest" pale atakapohitajika kufanya maamuzi.

8. Mtulia aombe radhi taifa kwa sababu "ujinga" wake wa kuhama chama ili kuunga mkono juhudi, umeliingiza taifa kwenye hasara kubwa ya kupoteza mabilioni ya shilingi, na kupoteza rasilimali watu (Binti Aquilina aliyeuawa na watu watatu waliosababishiwa vilema kwa majeraha ya risasi).

9. Mkurugenzi wa NEC Ramadhani Kailima afukuzwe kazi kwa kushindwa kumchukulia hatua mkurugenzi wa Kinondoni licha ya kupelekewa malalamiko mara kadhaa kuhusu mwenendo wa uchaguzi huo. Kama Kailima alipopewa malalamiko, angemuagiza Aaron atoe viapo kwa mawakala wa Chadema, maandamano yasingekuwepo, na Aquilina asingeuawa.

10. Mabadiliko ya Katiba yafanyike ili kuondoa vipengele vyote vinavyo-surbotage taifa na haki za raia. Mojawapo ya vipengele hivyo ni kile kinachomruhusu Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye ni kada wa chama cha siasa, awe msimamizi wa uchaguzi. Kipengele hili kinamuweka Mkurugenzi kwenye "conflict of interest" pale anapotakiwa kuwa refarii kati ya mgombea wa chama chake na wagombea wa vyama vingine. Ni wazi hawezi kutenda haki.!

[HASHTAG]#Justice4Aquilina[/HASHTAG]
 
Well said.Huwezi kupata vijana wenye uwezo wa kujenga hoja kwa ka mr slowly kaliko silimiwa udevil
 
Nini kifanyike hasira zimeenza kutuingia ngoja zikolee Majibu yatapatikana
 
.kaandika ukweli mtupu. Ila Ktk nini kifanyike. Hayo maoni/mapendekezo yote hayatafanyiwa kazi. Labda yafanyiwe kazi na katibu mkuu wa umoja wa mataifa. Ila kwa hapa hapa bongo, tuendelee kusubiri.
 
-Waziri wa mambo ya Ndani ajiuzulu kuonesha uwajibikaji. Asipofanya hivyo Rais amuwajibishe kwa kumfuta kazi. Matukio mengi ya kuogofya yametokea kipindi Mwigulu akiwa Waziri wa mambo ya ndani na hakuna hatua za maana alizochukua.
 
Mwandishi hakika unafaa kuwa jamii forum.

Umeandika kisiasa na wala si kiuanachama, heko kwako.
 
Kilio, kilio, kilio mpaka watanzania tuamke kudai katiba mpya. Vinginevyo kila chaguzi ni kilio.
 
Back
Top Bottom