Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,709
Tuchukulie kuwa wewe ni daktari mkuu wa eneo fulani na upo kwenye ndoa
Siku moja ukiwa kazini unasikia habari za kigaidi eneo husika kuwa kutokana na habari za kiintelijensia kuna mahali limetegewa bomu na inasemekena ni eneo na mkutanyiko wa watu wengi ila hawajui ni wapi,lakini baada ya muda mfupi unapokea simu kutoka kwa kiongozi mkuu wa eneo husika kuwa wanausalama wamefanikiwa kumkamata mtu mmoja ambae anahusika na njama hizo za kigaidi na katika harakati za wanausalama kumkamata walimjeruhi sehemu za kifuani na amevuja damu sana na alikuwa amekubali kuwatajia eneo bomu lilipotegwa na alikuwa amesema kuwa ni shule moja ya chekechea
Lakini kabla ya kuitamka ni shule gani akawa amepoteza fahamu na alisema kuwa bomu hilo litalipuka baada ya dakika 45 hivyo wanakimbizana na muda na yupo njiani na mkuu alitaka wewe uendeshe zoezi la kumtibu na kumrudishia fahamu ili aitaje shule husika lilipotegwa bomu ili likateguliwe na kusalimisha maisha ya watoto hao
Lakini wakati unakata simu unapokea simu nyingine ikikujulisha kuwa mwenzi wako wa ndoa [mke/mume] amepata ajali mbaya sana na yupo njiani kuletwa hapo kazini kwako [hospital] kwaajili ya matibabu na unajulishwa kuwa hali yake sio nzuri kabisa
Kwa bahati sijui mbaya au nzuri wagonjwa wote hawa wawili wanafika hospital kwa pamoja na kwa kuwatazama unaona wote wako mahututi na kwa namna ambayo wameumia ni lazima wapelekwe "thieta" kwa upasuaji na kibaya zaidi daktari bingwa wakufanya hiyo kazi uko peke yako hakuna mwingine
Lakini kikubwa zaidi huwezi kuwafanyia wote kwa pamoja,yaani ni lazima uanze na mmoja na maamuzi yoyote yale utakayofanya utakuwa unahatarisha maisha au uhai wa mmoja kwa namna wote walivyojeruhiwa na matukio yao
Sasa hebu niambie,kama wewe ndio daktari huyu utachagua kumhudumia mgonjwa gani hapa?
Nijibu halafu nitakuja kuwapa sababu ya kuleta hiki kisa hapa ..........
Mtambuzi nakusalimu popote ulipo ......!!