Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,077
Kama Watanzania hawaijui katiba, basi hakuna haja ya kuwa na Serikali, hakuna haja ya kuwa na Bunge wala hakuna haja ya kuwa na Mahakama. Turudi kwenye utawala wa jadi ambao haukuwa na katiba.
Kama wananchi hawajui katiba, Serikali, Bunge na mahakama vinapatikana kwa njia gani? Au ndiyo maana wanajipa Urais, wanajipa ubunge na udiwani bila ya kuchaguliwa na wananchi?
Serikali na Rais, Bunge na wabunge, mahakama na majaji, wote upatikanaji wake umeelekezwa na katiba. Kama wananchi hawajui katiba, hakuna haja ya kuwa na uchaguzi, wala hakuna haja kuwa na Rais, Serikali, Bunge, Mahakama, Polisi wala wala mahakama. Wale machifu wa kale, warudishwe kuongoza makabila yao. Wazee wenye hekima, warudishwe kuwahukumu wanaokosea.
Haiwezekani useme wananchi hawaielewi katiba, halafu wewe Urais wako uwe halali. Kama wananchi hawaelewi katiba, na wewe uliyetakiwa kupatikana kwa maelekezo ya katiba, huwi halali, unatakiwa kuondoka au kuondolewa. Ina maana umetumia ujinga wa wasioelewa katiba, kujipa madaraka na mamlaka.