Kama Wabunge hawafanyi mikutano majimboni mwao, wanavyovizungumza Bungeni wanavitoa wapi?

Wabunge ni wajumbe kwenye vikao vya madiwani na wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika vikao hivyo. so wanayoyazungumza huwa wanayatoa kwenye hivyo vikao
Pamoja na jibu lako zuri mwongezee na ujumbe huu kwamba akamuulize huyo aliyekataza hiyo mikutano
 
Katika hali ya kukosekana kwa mikutano ya Wabunge katika majimbo yao, Wabunge wanayapata wapi mambo wanayoyaongea na kuyajengea hoja Bungeni?
Wengi wamehama majimbo yao eti kukwepa kuombwa misaada na waliowatuma bungeni (iwe ya kifedha ama hali)! Mifano ipo.
 
Nadhani kuna umuhimu wa kuwatengenezea wabunge scorecard ambayo itaonesha mbunge amefanya vikao vingapi na wananchi wake na ushahidi wa maoni ya wananchi wake kuhusiana na hoja mbalimbali zinazowasilishwa bungeni.

Wengi wa wabunge wanawakilisha maslahi yao,vyama vyao na marafiki zao tu .
Umenena mkuu maana Hawa wengine wakisha chaguliwa wanapotea, kuna mbuge anaitwa MBONI MHITA huyu tangu achaguliwe amerudi jimboni Mara moja nahuko bungeni hata humsikii yani Taifa hili hasara tupu mtu akisha chaguliwa hakumbuki nyuma inasikitisha Sana hawa wawakilishi wetu, baadhi Wana wajibika ila wachache niuozo mtupu
 
Ndugai juzi kasema Ubunge hauitaji uzoefu wala utaalamu wowote...ndio maana na wao hawajihangaishi kufanya mikutano kwenye majimbo yao.
 
Nadhani kuna umuhimu wa kuwatengenezea wabunge scorecard ambayo itaonesha mbunge amefanya vikao vingapi na wananchi wake na ushahidi wa maoni ya wananchi wake kuhusiana na hoja mbalimbali zinazowasilishwa bungeni.

Wengi wa wabunge wanawakilisha maslahi yao,vyama vyao na marafiki zao tu .
nadhani tungetengeneza score cards za ahadi za uchaguzi kwanza . tuanze na ile ya ml 50 kwa kila kijiji hadi mikopo kwa wanafunzi na tanzania ya viwanda vya maji ya kunywa!
 
Kwani mbunge hana simu?
Kwani mbunge hana katibu wake na madiwani?

Madiwani wanaweza mfikishia kero za wananchi.
 
Kuna matatizo yanajulikana hapa Tanzania sekta ya kilimo,afya,uchukuzi,Elimu n.k haitaji muujiza kubaini, mbuge kama mjumbe wa council wajumbe wenzake wanampa tips ata kwa SMS au email.
 
Whatsupp groups............
Kila Kijiji...........
Kila Kata.........
Kila wilaya......
 
Back
Top Bottom