Kuwa na uchaguzi ambapo wabunge wanawaogopa wapiga Kura ni balaa

Oneya

JF-Expert Member
Mar 5, 2022
209
201
Ninafuatilia majimbo mbalimbali za uchaguzi kwa mienendo ya wabunge wa maeneo hayo. Vitendo vifuatavyo vimebainika.

1. Hawaitishi mikutano ya hadhara kuwaeleza wananchi mipango ya serikali inayohitaji utekelezaji. Wananchi hawahusishwi kwenye MAAMUZI yoyote ya kimaendeleo. Wenye viti wengi wa vijiji na mitaa hutumia matukio ya misiba na sherehe kufikisha ujumbe kwa wananchi. Kama hakuna mikutano, je, wananchi watashirikishwaje kwenye maendeleo.

2. Viongozi wengi wakiwemo wabunge hutumia ziara za wakuu wa nchi, mfano ; rais, waziri mkuu, mawaziri na wenyeviti wa vyama vyao kuhudhuria mikutano inayofanyika majimboni mwao. Hapa hawapati nafasi ya kufikisha ujumbe wao Bali huishia kutoa salaamu na kumsifia rais tu. Yeye Kama kiongozi Ni kutafuta tu namna ya kuhonga watu ili waujaze uwanja.

3. Viongozi wengi Ni waoga wanaogopa kujibu maswali ya wananchi juu ya Hali mbaya ya uchumi, mifumuko wa Bei, kadhia za serikali kujiingiza katika khashifa mbalimbali mfano DPW na umeme kukatikatika.

4. Viongozi wengi hawakutokana na chaguo la wananchi hivyo wanaogopa kuzomewa.
Kuwa na mwarubaini wa kadhia hii Ni kuwepo na tume huru. Kiongozi atokane na watu na siyo Dola.

IMG-20230929-WA0049.jpg
 
Back
Top Bottom