Kama ungepewa urais ungeanza wapi kunyanyua hali za wananchi?

Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
888
Nimekuwa nikisoma hoja mbalimbali za wanaJF na ningependekeza hoja zijengwe kuhusu suala hili.
Baadhi ya wanaJF wamesema urais si lelemama ni kitu complicated etc. Sasa mimi natoa challenge, je kama wewe ungekuwa rais ungeanza wapi?
Naomba nianze kwa kusema tatizo letu kubwa ni utendaji:
- Ningeanza kwa kuteua mawaziri 15 tu! Ningeunganisha wizara na kufanya idara. Mawaziri hawa 15 wangepewa mwongozo (hamna haja ya semina, wapewe mwongozo kimaandishi na mkutano moja wa orientation) wa kazi na kukumbushwa miiko na maadili
- Ningetangaza mali zangu hadharani na kuwabana mawaziri nao wafanye hivyo
- Ningeomba ushauri wa wakuu wa idara na watendaji katika mawizara. Nimegundua kwamba administrators wengi serikalini wako very frustrated na wanaelewa matatizo ni nini na hata suluhisho wanayo lakini wizara zinaendeshwa kisiasa
- Ningetoa maagizo ya kupitia upya auditing za wizara yote, where there is a problem watendaji na viongozi wawajibishwe.
- TAMISEMI ingefanyiwa pia auditing at all level. Kuwapa nguvu zaidi local governemnet is not a free hand kuchota.
- Kuipa nguvu zaidi PCCB tuprosecute without interference
- Baada ya kuweka adminsitration in place, that is when money and spending etc can be looked at with priority to Education, Infrastructure and Health. Others will improve accodingly.

Tusikae kulalamika nchi inaenda wapi, tujenge hoja hapa na tutoe suluhisho. Maybe one of us here is president-in-waiting! :)
 
tatizo ni mfumo wa nchi yetu,Siasia ya makundi ndio inatawala,na ni vigumu sana kutekelza hayo kwa serikali ya sisiemu,Kiwkete alichangiwa na watu wengi sana na utegemee atawalipa vipi?
mie cha msingi kwanza ni kuanza kuwang'oa hawa mafisadi kwa kutumia sanduku la kura then mambo mengine yatafuata.
 
Nakubaliana na wewe MkomboziUfisadi, mimi sisemi ungekuwa in the place of Kikwete. He has to do what he has to do (or not do), but ninachosema ni kwamba ungepewa fursa?
I think that we can expect changes in Tanzania, I am optimistic, wananchi wamechoka sana! Yaani mitaani ukisikia mazungumzo ya vijiweni utajua. Juzi nilisikia vijiweni, wachuuzi wakielezana jinsi Mauritius ilivyoendelea, watoto wanasoma shule, wana umeme na hawana madini wala mbuga za wanyama. Wana bahari tu! Hawa kaka zetu 'wenye elimu duni' walisema wazi tatizo ni kuwa umaskini wetu unasbabishwa na viongozi wenye uchu wa madaraka na mafisadi!
Watu wamefunguka macho. Sijui kama CCM watawadanganya nini tena 2010?!
 
Mimi nadhani tatizo kubwa ni mfumo wetu wa utawala ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na katiba yetu isiyojali maslahi ya mwananchi wa kawaida. Kwa hiyo suala hapa si kama ukipewa nchi bali ni namna gani uchukue nchi ili uwe na uwezo wa kubadili mfumo mzima wa utawala. Kwa upande wangu nadhani inabidi iendeshwe kampeni moja ya kufa mtu itakayoing'oa CCM madarakani kwanza kisha baada ya kuchukua nchi ni kubadili mfumo wa utawala kwa kuanza na suala la katiba mpya baadaye ni masuala ya kiuchumi ambayo kimsingi yatafanyiwa kazi vizuri tu ikiwa mfumo wa utawala utakuwa ni mzuri.
 
Na anza Na Elimu...Nina endeleza walio ya shindwa..kama Chakula kwa watoto wa shule..
Nita unganisha wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari kwenye Mfumo wao wa komputa...secondari vyuo na taasisi zote za elimu..

Mikopo kwa wananchi...Mshahara inayo endana na wakati kwa wafanya kazi wa serikali...
Nita punguza Ukubwa wa Jeshi ..na kuunda jeshi La hifadhi ya chakula..Kila Mkoa au eneo Lita jitegemea kwa chakula...( maghala ya mkoa)

Nipe Kula yako Naona uanachelewa..
 
Ningelipata fursa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania ningelibalisha mfumo wa siasa yetu na utendaji kazi wetu.
1. Wizara za serikali zingelikuwa ni 11 tu.
a. Wizara ya Fedha
b. Wizara ya Kilimo na Maji
c. Wizara ya Elimu Primary na Secondary
d. Wizara ya Elimu ya Juu, Sience na Techologia
e. Wizara ya Afya.
f. Wizara ya Ardhi.
g. Wizara ya Umeme na Madini
h. Wizara ya Industries(Viwanda) , Usafiri na Tele Communication
i. Wizara ya Kazi,Vijana na Michezo
j. Wizara ya Maendeleo ya Jamii na utawala wa majimbo.
k. Wizara ya Sheria.

2. Mawaziri wote wa wizara hizi wangelikuwa ni wapya kabisa na ni wasomi.
3. Makatibu wote wa wizara hizo wangelikuwa ni wapya na wenye ujuizi wa adrministartion.
4. Kila wizara ingelikuwa na Accountant mpya na wenye shahada nzuri wa kuweza kufanya kazi hiyo.

5. Kila mtanzania angelipata “personal number”(identity number) toka azaliwapo.Nambari hii itamfuata katika maisha yake yote, katika vyeti vyake vyote.

6. Kila mtoto atapewa fedha za kutiunzwa kila mwezi mpaka akitimia umri wa miaka 10. Fedha hizi zitapewa wazaki kina mama kwenye account zao benki.

7. Wanafunzi wa Secondary na High School watapatiwa fedha za matumizi wao wenyewe kila mwezi.

8. Elimu yote ya primary,secondary na high School ingelilipwa na serikali kutokana na kodi za wafanyakazi.

9. Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wote wangelipewa mikopo ya kusomea mafunzo yao.

10. Mlo mmoja wa bure kwa kila mwanafunzi wa primary,secondary na high School.

11. Hatua hizi ni za kuwapunguzia mzigo wazazi wote na kupambana na umasikini.

12. Ningelifanya juhudi za kuchimba madini tuliyonayo kwa manufaa ya Tanzania. Tungechimba chuma, makaa ya mawe(ili kutengeneza umeme).

13. Tungelijaribu kutengeneza umeme kutokana ma nguvu za upepo(WindMills),nguvu za mawimbi ya bahari na nguvu za miayanzi ya Jua(Solar Energy).

14. Tungeliimarisha ukulima wa kisasa na uvunaji wa kisasa kwa mazao yetu yote.

15. Tungelijenga barabara mpya na kuziboresha reli zetu na bandari zetu zote ili usafiri uwe ni rahisi kwa wote.

16. RUSHWA NI MWIKO.KILA ANAYEPATIKANA NA RUSHWA AWE KIONGOZI AU SI KIONGOZI SHERIA ATACHUKUWA MKONO WAKE MADHUBUTI. ATAWAJIBIKA.
 
 • Kwanza...
 • Miundombinu-Umeme,barabara,madaraja, na njia nyingine za mwasiliano.
 • Rejesho la Mapato kwa kuboresha njia za upatikanaji wa kodi
  Halafu...
 • Kubainisha njia za kutoa ajira na kuendeleza marekebisho ya mishahara kwenye sekta binafsi
 • Kuhakikisha pensheni zinapatikana kwa wastaafu kutoka sekta zote hususan zisizokiserikali au binafsi kwa kuweka na kuboresha sheria zinazoendana na wakati na zenye mfumo mwelekeo kwenye vitega uchumi kwa ajili ya maisha ya wastaafu
 • Kuweka mkarakati wa kuwezesha watoto wote waendao shule yaani darasa la kwanza mpaka la saba wanapata matibabu ya bure kuondoa mzigo kwa mzazi na vile vile kuhakikisha vijana hawa wa kesho wanasoma na kukuwa wakiwa na afya njema pamoja na kuhamasisha elimu kwa watu wazima
 • Kuendeleza cooperative kwa ajili ya wakulima wadogo ili waweze kujiinua kikulima na kimapato
 • Kutafuta na kuboresha mbinu zitakazotoa ukiritimba serikalini kwa njia ya decentralization na utumiaji wa teknolojia- asilimia kubwa ya watanzania 90% wako vijijini badala ya kuja mijini na kupoteza maelfu barabarani na hata kwa wala ruswha haya maelfu yatabaki mikononi

  Kuhamasisha na Kuhakikisha utamaduni wetu wakiTanzania hauingiliwi kwa kuweka ukiritimba unaoendana sambambamba na wakati na utamaduni na mila zetu ili kuepusha mila na desturi zingine zinazoonekana kuleta maafa kwenye nyanja nyingi za utamaduni ambao ndio chanzo cha kuharibika vijana wengi kimaisha na kuboresha elimu na huduma ya jamii
  Ni mengi tu ambayo yanawezekana kuboreshwa au kunyanyua hali ya Mtanzania! Njiwa wengi hapa! :)
 
Atanae unaweza kuni PM longolongo too much muyomba!!! Wapi susuvir the starter of this thred? you would assume him to be moderating!!!
 
Nitafikiria labda!! utakua mashauri wangu
SAWA?.Punguza maneno kwanza Nimalizie...Nisikilize ....au endele a Kufafanua..Una haraka haraka...Tulia...
 
Jamani samahani! :( Nilianza thread alafu nilifuatila kwa muda nikaona watu wanaisoma tu... nikajua labda hakuna wakereketwa! Nimefurahi kuona maoni mbalimbali naomba nijajibu hapo chini!
 
Mimi nadhani tatizo kubwa ni mfumo wetu wa utawala ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na katiba yetu isiyojali maslahi ya mwananchi wa kawaida. Kwa hiyo suala hapa si kama ukipewa nchi bali ni namna gani uchukue nchi ili uwe na uwezo wa kubadili mfumo mzima wa utawala. Kwa upande wangu nadhani inabidi iendeshwe kampeni moja ya kufa mtu itakayoing'oa CCM madarakani kwanza kisha baada ya kuchukua nchi ni kubadili mfumo wa utawala kwa kuanza na suala la katiba mpya baadaye ni masuala ya kiuchumi ambayo kimsingi yatafanyiwa kazi vizuri tu ikiwa mfumo wa utawala utakuwa ni mzuri.

Kama wewe ukiukwaa urais it means chama chako kimeshinda, kwa hiyo kuing'oa chama tawala kama upinzani utakuwa umefanikiwa.
Kuandika upya katiba pia inawezekana kama una majority bungeni, lakini inawezekana ukawa rais na chama chako kisishike viti vingi bungeni kwa sababu ni kura tofauti. Hata hivyo kwa sababu tunazungumzia katiba ya nchi, mi nadhani kuna haja ya kuwa na consensus.
Mi napenda sana kuangalia katiba ya Marekani na kusoma katika historia ni jinsi gani walibishana na kuja kuandika katiba akina Jefferson. Pia ni katiba nzuri kwa sababu iko simple alafu ina amendments inayoruhusu katiba iwe inakwenda na wakati (kwa mfano kufuta utumwa after 200 years - historian correct me if I am wrong!)
So mi nadhani Tanzania tungeweza kuangalia mifano ya nchi zingine. Siyo lazima tutunge katiba mpya kabisa bali tunaweza kufanya amendments. Kama kuna kipengele chenye utata sana tunaweza kubadili au kukifuta.
 
Na anza Na Elimu...Nina endeleza walio ya shindwa..kama Chakula kwa watoto wa shule..
Nita unganisha wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari kwenye Mfumo wao wa komputa...secondari vyuo na taasisi zote za elimu..

Mikopo kwa wananchi...Mshahara inayo endana na wakati kwa wafanya kazi wa serikali...
Nita punguza Ukubwa wa Jeshi ..na kuunda jeshi La hifadhi ya chakula..Kila Mkoa au eneo Lita jitegemea kwa chakula...( maghala ya mkoa)

Nipe Kula yako Naona uanachelewa..

Mikopo kwa wananchi inafanywa na serikali ya sasa na kwa mtazamo wangu ni kugawa tu pesa na zinakuja kutumika vibaya. Utahakikisha vipi wananchi wanarudisha mikopo? Utatumia utaratibu gani kugawa mikopo?
Kuhusu ukubwa wa jeshi, kuna hatari hapo kwani kumbuka jeshio hilo kubwa limepewa mafunzo ya kupigana, wakiingia mtaani wanaweza kuendeleza attitude hiyo hiyo ya kupigana. Nadhani umesoma ktk habari jinsi vijana wa JKT wanavyofanya vurugu uraiani! Mi nadhani hao wanajeshi wanaweza kufanya kazi nyingi muhimu kama vile kujenga mabarabara n.k. na kuwa kama Peace Corps au ndiyo hiyo jeshi la kuhifadhi chakula unayozungumzia?

You have some very good points! Just elaborate a bit
 
Ningelipata fursa ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania ningelibalisha mfumo wa siasa yetu na utendaji kazi wetu.
1. Wizara za serikali zingelikuwa ni 11 tu.
a. Wizara ya Fedha
b. Wizara ya Kilimo na Maji
c. Wizara ya Elimu Primary na Secondary
d. Wizara ya Elimu ya Juu, Sience na Techologia
e. Wizara ya Afya.
f. Wizara ya Ardhi.
g. Wizara ya Umeme na Madini
h. Wizara ya Industries(Viwanda) , Usafiri na Tele Communication
i. Wizara ya Kazi,Vijana na Michezo
j. Wizara ya Maendeleo ya Jamii na utawala wa majimbo.
k. Wizara ya Sheria.

2. Mawaziri wote wa wizara hizi wangelikuwa ni wapya kabisa na ni wasomi.
3. Makatibu wote wa wizara hizo wangelikuwa ni wapya na wenye ujuizi wa adrministartion.
4. Kila wizara ingelikuwa na Accountant mpya na wenye shahada nzuri wa kuweza kufanya kazi hiyo.

5. Kila mtanzania angelipata “personal number”(identity number) toka azaliwapo.Nambari hii itamfuata katika maisha yake yote, katika vyeti vyake vyote.
6. Kila mtoto atapewa fedha za kutiunzwa kila mwezi mpaka akitimia umri wa miaka 10. Fedha hizi zitapewa wazaki kina mama kwenye account zao benki.

7. Wanafunzi wa Secondary na High School watapatiwa fedha za matumizi wao wenyewe kila mwezi.

8. Elimu yote ya primary,secondary na high School ingelilipwa na serikali kutokana na kodi za wafanyakazi.

9. Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wote wangelipewa mikopo ya kusomea mafunzo yao.

10. Mlo mmoja wa bure kwa kila mwanafunzi wa primary,secondary na high School.

11. Hatua hizi ni za kuwapunguzia mzigo wazazi wote na kupambana na umasikini.

12. Ningelifanya juhudi za kuchimba madini tuliyonayo kwa manufaa ya Tanzania. Tungechimba chuma, makaa ya mawe(ili kutengeneza umeme).
13. Tungelijaribu kutengeneza umeme kutokana ma nguvu za upepo(WindMills),nguvu za mawimbi ya bahari na nguvu za miayanzi ya Jua(Solar Energy).

14. Tungeliimarisha ukulima wa kisasa na uvunaji wa kisasa kwa mazao yetu yote.

15. Tungelijenga barabara mpya na kuziboresha reli zetu na bandari zetu zote ili usafiri uwe ni rahisi kwa wote.

16. RUSHWA NI MWIKO.KILA ANAYEPATIKANA NA RUSHWA AWE KIONGOZI AU SI KIONGOZI SHERIA ATACHUKUWA MKONO WAKE MADHUBUTI. ATAWAJIBIKA.

Uliyoyaandika ni mazuri sana! Lakini mimi naona kuna matatizo katika utekelezaji.
Hapo mwanzo ni nzuri sana ulivyowalenga watendaji wakuu kuwapunguza na also kupandisha standard! Hilo halina mjadala!
Lakini kwenye personal ID number ninasita kidogo! Umesikia jinsi data za wananchi milioni 25 wa Uingereza ilivyo'potea'au kuibiwa hivi majuzi? Kwa hapa nchini utunzaji wa data ni mbovu na hatuna utaratibu mzuri wa utunzaji especially IT. Mi naona tutawaexpose sana wananchi!
Kuna points zingine za elimu bure na pesa kwa wananchi alafu ile ya migodi. Masuala yote yanahitaji pesa, mi nadhani kwa nchi maskini kama Tanzania kuna haja ya kubalance. Kuchimbua yale madini kunahitaji mtaji mkubwa sana ambao nchi haina! Mi nadhani ubia ni kitu kizuri zaidi kuliko umiliki wa 100% wa serikali, je hilo unafikiriaje?
 
 • Kwanza...
 • Miundombinu-Umeme,barabara,madaraja, na njia nyingine za mwasiliano.
 • Rejesho la Mapato kwa kuboresha njia za upatikanaji wa kodi
  Halafu...
 • Kubainisha njia za kutoa ajira na kuendeleza marekebisho ya mishahara kwenye sekta binafsi
 • Kuhakikisha pensheni zinapatikana kwa wastaafu kutoka sekta zote hususan zisizokiserikali au binafsi kwa kuweka na kuboresha sheria zinazoendana na wakati na zenye mfumo mwelekeo kwenye vitega uchumi kwa ajili ya maisha ya wastaafu
 • Kuweka mkarakati wa kuwezesha watoto wote waendao shule yaani darasa la kwanza mpaka la saba wanapata matibabu ya bure kuondoa mzigo kwa mzazi na vile vile kuhakikisha vijana hawa wa kesho wanasoma na kukuwa wakiwa na afya njema pamoja na kuhamasisha elimu kwa watu wazima
 • Kuendeleza cooperative kwa ajili ya wakulima wadogo ili waweze kujiinua kikulima na kimapato
 • Kutafuta na kuboresha mbinu zitakazotoa ukiritimba serikalini kwa njia ya decentralization na utumiaji wa teknolojia- asilimia kubwa ya watanzania 90% wako vijijini badala ya kuja mijini na kupoteza maelfu barabarani na hata kwa wala ruswha haya maelfu yatabaki mikononi

  Kuhamasisha na Kuhakikisha utamaduni wetu wakiTanzania hauingiliwi kwa kuweka ukiritimba unaoendana sambambamba na wakati na utamaduni na mila zetu ili kuepusha mila na desturi zingine zinazoonekana kuleta maafa kwenye nyanja nyingi za utamaduni ambao ndio chanzo cha kuharibika vijana wengi kimaisha na kuboresha elimu na huduma ya jamii
  Ni mengi tu ambayo yanawezekana kuboreshwa au kunyanyua hali ya Mtanzania! Njiwa wengi hapa! :)

Asante kwa mchango mzuri ingawa naona iko vague kidogo. Mi naamini hata Mwungwana alikuwa na malengo kama haya ukisikiliza hotuba yake ya kwanza, tatizo inakuwa utekelezaji.
Labda niulize ili kufikia malengo haya utawezaje kuongeza mapato? Kusema kwamba utaongeza kodi utaua wananchi! We are already paying too much taxes? Je Reagonomics ni suluhisho? Rais Reagan wa US wakati huo alipunguza kodi binfasi na ya makampuni ili kuhamasisha ujasiriamali na matokeo yake yalikuwa mazuri ingawa wapo wachumi wanaosema kubwa mafanikio yake yalikuwa ni short term!
 
Akhsante na we pia SUSUVIRI! Kwa kuleta hii! Nitaendela kibluu-bluu hapa!
"Asante kwa mchango mzuri ingawa naona iko vague kidogo. Mi naamini hata Mwungwana alikuwa na malengo kama haya ukisikiliza hotuba yake ya kwanza, tatizo inakuwa utekelezaji."
 • Kwa kweli Sijasoma hotuba hiyo. Naamini kuwa na Vision! Na huyo Muungwana anayo!!
 • Na naomba nikusahihishe! Not Vague but broad in perspective! or Perspicuous!!
Labda niulize ili kufikia malengo haya utawezaje kuongeza
mapato?

 • Nchi karibu nyingi za Afrika zina miundombinu zilizopwaya-Hii imetokana na mengi tu, hapa- ongezeko la watu ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo na ufinyu katika sekta hii na tunajua kuwepo ongezeko hilo barabara,mahospitali, au niseme tu Huduma za jamii zinakuwa hazitoshelezi matakwa- na ni lazima kuwe na miundombinu ambayo ita accomodate wingi huo-remember this is dynamic-na ndio pale watu wakiwa na afya nzuri na wanaweza kwenda popote kufanya biashara, uchumi utakuwa, na ndio hapo utaweza kuona ni sehemu gani yenye kuleta mafanikio na maslahi kwa taifa na jamii na ndio sehemu hiyo hiyo unaweza kubainisha au kuboresha upatikanaji wa kodi!
 • Kukujibu swali lako...Miundombinu, Miundombinu,Miundombinu!!
Kusema kwamba utaongeza kodi utaua wananchi! We are already paying too much taxes?

 • Sikusema hivyo! nimesema kuboresha njia za upatikanaji wa kodi!
 • kwa mfano: mimi na wewe tuwe na magari aina moja kilakitu kinafanana isipokuwa mimi matairi ni 15" na wewe 20" nitakuchaji wewe visenti zaidi kwa sababu tu umeongeza thamani kwenye hilo gari!(NI mfano) Mimi sio mchumi lakini I beleive we can find an equilibrium somewhere!...nisaidie equilibrium kwa kiswahili hapa!!;)
Je Reagonomics ni suluhisho? Rais Reagan wa US wakati huo alipunguza kodi binfasi na ya makampuni ili kuhamasisha ujasiriamali na matokeo yake yalikuwa mazuri ingawa wapo wachumi wanaosema kubwa mafanikio yake yalikuwa ni short term!
 • Kama sitaweza kupita kasulu and beyond(kwasababu ya Miundombinu) siwezi kusamehe au kushusha kodi kwa mwananchi! Lakini nikipata watu beyond kasulu wenye kujichanganya kiuchumi basi nitapunguza kwasababu tu nimepata watu wengine wawili au watatu ambao watachangia!
 • Na kuhusu makampuni nitafanya vinginevyo kwani sasa ndio waliosamehewa makodi haya na hakuna ajira kwa mtanzania!
Hivyo basi bila watanzania angalau 100 kuwepo na ajira katika kampuni hiyo...kodi utalipa!
zoezi hili la kusamehe makampuni lipo...
Hii inaendelea nchini na ndio sababu ya matatizo yote ya kuibiwa mfuko wa mapato wa kodi za wananchi! kwa hivyo basi hii Reagonomics...na nafikiri ulikuwa na jibu... "mafanikio yalikuwa short term! Mimi nitasema ATANAYE-GOES-ECONOMICS!

Na Kuongeza tu...Vague is to be uncertain-naamini haya yanatekelezeka na ni wakati muafaka kwa Mtanzania kuwa mzalendo haswa na kuona hii juhudi inafanywa pamoja na wote!

A quote from Thomas Edison "If we all did things we are capable of doing, we would literally astound ourselves?:eek:
 
Msosi kwanza!

Nchi ni lazima iwe na msosi wa kutosha na aina ile ipendwayo.
Kilimo cha mpunga na ufugaji wa kuku ng'ombe na mbuzi bila kusahau maharage na mbogamboga.

Kuna mashangingi mengi kuliko matrekta.
Nitahakikisha kuna matrekta mengi kuliko mashangingi.

Nitakufa na wattendaji juu ya suala la umeme na maji mpaka kieleweke.
Umeme na maji ni kama mishipa ya fahamu na damu mwilini.

Nitaangalia viwango vya kodi na kuviwianisha ku discourage Rushwa Kisha Nitasimamia makusanyo ya kodi na matumizi yake kwa ukali wa mbwa mwenye meno.

Nitapiga marufuku kuingiza bidha tunazoweza kuzarisha wenyewe.Sukari, Chumvi, Juice, Nyanya, Nyama aina zote, Viberiti,Cement, mbao nk. Nitahimiza waagizaji wawekeze viwanda vya kusindika mazao hayo.

Nitaanzisha mpango kabambe wa makusudi wa kusomesha vipanga maelfu wa Kitanzania nje ya nchi katika fani za Science na Technolojia,utawala na sheria, Biashara na uchumi.
 
MADELA WA MADILU,
Kwa nini uwapeleke vijana nje ya nchi- kwa nini usiimarishe vyuo vilivyopo na kuanzisha vingine? Kisha ajiri Waaalimu wazuri toka nje- ili kujenga uwezo wa ndani?
 
Taabu kama nchi tumeweka vipaumbele vingi mno wakati mmoja! Tunashika kila kitu at the end we achieve so little! Hayo wawazo kuwaondoa mawaziri wote na Makatibu wakuu wote na kuweka wapya ni hadithi za Alinacha- as a country you need stability and peace na siyo kulipiza kisasi au kukomoana!
This is how I would prioritize:

A: Priorities 1st 10 Years
1. Chakula cha kutosha (Green/Food Revolution)
2. Massive Investment in Education haswa ufundi vijijini
3. Investment in health
4. Ujenzi wa barabara
5. Massive Investment in reliable energy
6. Kuhakikisha nakusanya kodi toka 40% or less kwa vyanzo vya sasa to 80% or more in 10 years

B: Priorities 2nd 10 years
1: Promote industrialization
2. Promotion of tourism
3. Cut off of external AID (to support budget) unless for humanitarian reasons
4. E.t.c

Muhimu baada ya miaka 10 ya mwanzo ni kukataa misaada- je humjatambua kuwa Misaada ndo inatudumaza? When 40% of budget ni AID- you can not prioritise independently, wakati serikali inakusanya only 40% ya vyanzo vya mapato kwa sasa!
 
In fact, katika majadiliano haya nimekumbuka kuna suala moja muhimu ambayo hatujazungumzia na inawagusa wengi hapa JF:
Return of Tanzanians living abroad.
Mi nadhani suala la uraia wa nchi mbili ni muhimu sana! Lakini kutokana na unyeti wa suala hili, ningekuwa rais ningeanzisha utaratibu kama uliopo Ethiopia.
Ningetoa pasi maalum kwa watanzania wanaoishi nje au wenye uasili wa Kitanzania (Tanzanian ancestry hata kama ni babu yako au bibi yako alikuwa mtanzania)
Pasi hizi zinamwezesha mhusika kuingia nchini bila visa, anaweza kumiliki ardhi, ana haki zote sawa na watanzania ila katika siasa hataruhusiwa kugombania na MAYBE hata kupiga kura hataruhusiwa (haishi hapa)
Nadhani hii ni njia moja nzuri ya kuwavutia watanzania wanaoishi nje kurudi kuwekeza nchini.
Sijui kuhusu suala la remittance lakini nadhani kama Philippines unakuta asilimia kubwa ya pato la taifa linatokana na wafilipino wanaoishi nje na wanaorudisha pesa nyumbani. Hii inamaana hata masharti ya kuhamisha pesa yangelegezwa.
We should be more inclusive. Kwani kwa njia hii hatuhitaji wataalam kutoka nje. Also lecturers waliolowea nje wa kibongo na ambao wangependa kurudi hata for a few years wanaweza kuja and test the waters witha special contract.
 
Taabu kama nchi tumeweka vipaumbele vingi mno wakati mmoja! Tunashika kila kitu at the end we achieve so little! Hayo wawazo kuwaondoa mawaziri wote na Makatibu wakuu wote na kuweka wapya ni hadithi za Alinacha- as a country you need stability and peace na siyo kulipiza kisasi au kukomoana!
This is how I would prioritize:

A: Priorities 1st 10 Years
1. Chakula cha kutosha (Green/Food Revolution)
2. Massive Investment in Education haswa ufundi vijijini
3. Investment in health
4. Ujenzi wa barabara
5. Massive Investment in reliable energy
6. Kuhakikisha nakusanya kodi toka 40% or less kwa vyanzo vya sasa to 80% or more in 10 years

B: Priorities 2nd 10 years
1: Promote industrialization
2. Promotion of tourism
3. Cut off of external AID (to support budget) unless for humanitarian reasons
4. E.t.c

Muhimu baada ya miaka 10 ya mwanzo ni kukataa misaada- je humjatambua kuwa Misaada ndo inatudumaza? When 40% of budget ni AID- you can not prioritise independently, wakati serikali inakusanya only 40% ya vyanzo vya mapato kwa sasa!

Mzalendohalisi, nimecheka sana! Kwa kuandika hivyo una maana kwamba umepanga kuwa rais kwa miaka 20? Umekuwa Musharaff? ;)
Kwa bahati mbaya if all goes well, una miaka 10 tu kuwa rais. Je utaweza kuyatimiza haya yote ndani ya miaka 5 - 5?
On a more serious note:
Nakubaliana na wewe ya kuwa misaada ndiyo chanzo kikubwa cha Tanzania kutopata maendeleo na ndiyo maana baadhi ya nchi zilizopata misukosuko kama vita n.k. wakijakutulia wanapata maendeleo sana look at Vietnam, Angola (fastest growing economy in Africa! 20 something percent per year!) Tatizo ni kwamba we are very dependent so we have to be weaned off. Ule msamaha aliou-achieve Mkapa was a good step lakini tumerudi nyuma tena, we have to maintain fiscal discipline!
 
Back
Top Bottom