Habari wanajamvi.
Ni hivi majuzi mke wangu mama Baraka nimemkuta anaongea kwenye simu na mzazi mwenzake baba Baraka, kinachonipa mashaka ni namna alivyokuwa anajibu kwa unyenyekevu wakati mwingine akijitetea kuwa hakumkatia simu bali lilikuwa ni tatizo la mtandao.
Hofu yangu ya kwamba huenda ninachapiwa ilikuja baada ya kumwuliza Ulikuwa unaongea na nani? hakutoa majibu ya kuridhisha, psychologically alichanganyikiwa.
Ukweli sina imani nae kabisa na wazo nililonalo nikumwacha, na iwapo nitamwacha atakuwa ni wa nne.
Nipeni ushauri.