Kama unaubavu tumbua jipu kiwanda cha sukari

Kahtan Ahmed

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
765
489
Yaa kama kweli ww muheshimiwa umeamua kutumbua majipu bila kumuogopa yoyote na kwa maslahi ya taifa tumbua kiwanda cha mtibwa maana tumeshachoka na maigizo yako ya sanaa za zamani mana kama ingelikua movie wala isingenivutia
 
Mkuu hebu ongezea nyama mada yako huko mtibwa kuna jipu gani?, maana wengine hatuna taarifa ya mtibwa kuwa na jipu
 
mkapa ndio mwenye kiwanda atueleze kwanini gharama za sukari kutoka nje mpaka hapa ni rahisi mara 2 ya sukari kutoka mtibwa yani mfuko wa sukari ya kilo 50 kutoka vietnam au thailand pamoja na usafiri mpaka hapa tsh 40000 wakati kiwandani hapa kutoka mtibwa ni tsh 75000 na tumezuiwa kuleta sukari kutoka nje ili kulinda kiwanda cha mtibwa hali ya kua kinawanyonya wanachi?
 
jipu liko kwapani mwake mwenyewe,yule bwana alitengeneza kinga kubwa sana kuwaita watu mabwege,Sijui mandezi, Sijui malofa...aargh sikumbuki vzr barna
 
mkapa ndio mwenye kiwanda atueleze kwanini gharama za sukari kutoka nje mpaka hapa ni rahisi mara 2 ya sukari kutoka mtibwa yani mfuko wa sukari ya kilo 50 kutoka vietnam au thailand pamoja na usafiri mpaka hapa tsh 40000 wakati kiwandani hapa kutoka mtibwa ni tsh 75000 na tumezuiwa kuleta sukari kutoka nje ili kulinda kiwanda cha mtibwa hali ya kua kinawanyonya wanachi?[/QUO
mkapa ndio mwenye kiwanda atueleze kwanini gharama za sukari kutoka nje mpaka hapa ni rahisi mara 2 ya sukari kutoka mtibwa yani mfuko wa sukari ya kilo 50 kutoka vietnam au thailand pamoja na usafiri mpaka hapa tsh 40000 wakati kiwandani hapa kutoka mtibwa ni tsh 75000 na tumezuiwa kuleta sukari kutoka nje ili kulinda kiwanda cha mtibwa hali ya kua kinawanyonya wanachi?

Mwenye kiwanda cha sukari cha Kagera ndiye anamiliki kiwanda cha Mtibwa, sasa hapa Mzee Mkapa anaingiaje hapo - sio vizuri kuwazulia watu, ungesema Mh.Mkapa ni outgrower wa miwa hapo ningekuelewa lakini ili la kusema anamiliki kiwanda hiyo si kweli.

Kitu kingine, sukari kutoka Thailand na Vietnam serikali zao zinawapa ruzuku wenye viwanda vya sukari ndio maana bei zao ziko chini sana, wanafanya hivyo maksudi ili waweze kuuza sukari nje kwa wingi.
 
Mliona wapi mtu anasukuma gari akiwa ndani? Wabongo komaeni mpate lishe bora mkuze IQ zenu maana CCM inawateka kwa ufinyu wa akili zenu.
 
Weka uthibitisho wa Mkapa kumiliki hicho kiwanda cha mtibwa. Tumechoka na Story za kutungwa.

Rais Jpm kuzuia uingizwaji wa sukari toka nje ya nchi hauhusiani na kumlinda Mkapa. Jpm analinda wawekezaji kwenye viwanda vilivyopo nchini kwetu pamoja na ajira za watanzania . Ni sera za uwekezaji ambazo zipo dunia nzima.

Huwezi kuvutia uwekezaji wakati umeruhusu bidhaa inayofanana na hiyo toka nje ya nchi. Ni hasara kwa muwekezaji, wafanyakazi wa kampuni, pamoja na wakulima wa muwa.
 
Huwezi kuvutia uwekezaji wakati umeruhusu bidhaa inayofanana na hiyo toka nje ya nchi. Ni hasara kwa muwekezaji, wafanyakazi wa kampuni, pamoja na wakulima wa muwa.
Hasara ya mwekezaji inatuhusu nini wananchi katika enzi hizi za soko huria? Kwani serikali inapaswa kuangalia lipi; faida ya mwekezaji au unafuu wa bei kwa mwananchi wake?
 
Mwenye kiwanda cha sukari cha Kagera ndiye anamiliki kiwanda cha Mtibwa, sasa hapa Mzee Mkapa anaingiaje hapo - sio vizuri kuwazulia watu, ungesema Mh.Mkapa ni outgrower wa miwa hapo ningekuelewa lakini ili la kusema anamiliki kiwanda hiyo si kweli.

Kitu kingine, sukari kutoka Thailand na Vietnam serikali zao zinawapa ruzuku wenye viwanda vya sukari ndio maana bei zao ziko chini sana, wanafanya hivyo maksudi ili waweze kuuza sukari nje kwa wingi.
Tatizo la Watanzia weng wenu ni vilaza na ccm wanawapenda sana watu kama nyie kwan ndo mtaji wao, Ina mana mpaka leo ivo viwanda ni vya mh rais Mstaafu? Acha kutetea ujinga ww, Jifunze kufatilia mali za nch yako kwa kina
 
Serikali iruhusu sukari kutoka nje sukari ilikuwa inauzwa 2000 baada ya kupiga marufuku sukari ya nje leo inauzwa 2200 mpaka 2500.

Hii bei inaumiza wananchi.,tunalinda ajira za watanzania wachache huku kundi kubwa la Watanzania wanatumia sh.200-500 fedha ya ziada kununua sukari.
 
Kiwanda cha mtibwa ni mali ya CCM haiwezekani kwa madhila yote wayapatayo wana mtibwa bado serikali imekaa kimya huku ikimkumbatia muwekezaji.
Wafanyakazi hawalipwi mishahara kwa wakati yaani sometimes hadi miezi mitatu no mshahara.
Outgrowers karibu 90% wameachana na kilimo cha miwa kutokana udharimu uliopindukia hasa kutolipwa kwa wakati, makato yasoeleweka na miwa kupunguzwa kiwango cha sukari kwa maksudi.
Kuna malalamiko mengi kuhusu kutolipwa kwa wastaafu stahili zao na manyanyaso kwa wafanyakazi.
Kiujumla maendeleo ya Turiani yamefifishwa na kusuasua kwa kiwanda cha mtibwa wakati wananchi wana ardhi nzuri tu ya kulima zao hili.

Magufuli kama unaona haiwezekani kusitisha mkataba na huyu muwekezaji basi wafungulie kiwanda kingine wananchi kwani ardhi ipo ya kutosha na watu wana nia ya kulima zao hili kwa wingi.
 
Back
Top Bottom