c&p
*BAADA YA MIAKA 20 MTAKUJA TANZANIA KUOMBA KAZI*
Nilipokuwa mwanafunzi nchini Poland miaka ya 90, tulikuwa na tabia ya kwenda Sweden wakati wa likizo na kufanya vibarua mbalimbali hasa kwenye mashamba ya wakulima. Watanzania kutoka nchi mbalimbali za Ulaya Mashariki tulikuwa na sehemu zetu tulikokuwa tunakutana na kufanya vibarua hivyo kwa malipo ambayo kwa mwenyeji yalikuwa madogo sana lakini kwa sisi toka Ulaya ya Mashariki ya wakati huo yalikuwa makubwa sana. Tukirudi Poland na hizo nchi zingine na dola zetu, basi tunaanza kuishi kama watoto wa mfalme wa Nsesi. Pombe kwa wingi, watoto wa kizungu, na sherehe kila weekend.
Hao wakulima wa Sweden walikuwa watu wa kawaida wenye elimu za chini lakini wakiwa matajiri wenye mashamba makubwa makubwa na machine kubwa kubwa. Sisi vibarua wao tulikuwa na elimu kubwa kubwa, wanafunzi wa Ph.D, Masters, Degrees. Tulikuwa engineers, madaktari, wanasheria, wachumi nk.
Siku mmoja boss wetu huyo mkulima akawa anapiga story na sisi na kuanza kumwuliza kila mmoja anasomea nini. Tukamwambia maelimu yetu makubwa makubwa. Tulipomaliza akasema yeye elimu yake ni ya msingi ambayo ilikuwa kama form four ya Tanzania lakini ana mashamba na anaweza kutuajiri sisi Wasomi. Akaendelea kusema amefika Tanzania mara nyingi na ni nchi nzuri sana na hali ya hewa nzuri kwa kilimo na uwekezaji mwingine. Anashangaa kwanini ni maskini hivyo mpaka wasomi wake tunakuja kufanya vibarua mashambani ili kujiongezea kipato? Akasema Sweden peke yake imeisaidia mno Tanzania lakini haoni tukisogea mbele.
Alichomalizia ndio kimenifanya niandike leo. Akasema tukibadilishana watu leo. Waswedish wote wakaenda Tanzania na mikono yao mitupu na Watanzania wote wakaja Sweden na mikono yao mitupu. Baada ya miaka 20 Tanzania itakuwa nchi tajiri na Sweden itafilisika na kuwa nchi maskini na mtaanza kurudi Tanzania kuomba vibarua.
Ukweli mwingine unauma lakini hubaki kuwa ukweli. Ni miaka karibu 25 toka tuambiwe hayo na bado Sweden ni nchi tajiri na Tanzania ni nchi maskini. Zile elimu zetu kubwa kubwa hazijatusaidia kitu. Naendelea kutafakari. Yule Mzungu ni kama alikuwa sahihi.
Tunakosea wapi watanzania na nani atakuja kutwambia kuwa sio kila kitu uwe na mtaji bali kama ardhi ipo basi fulsa ya kwako wewe ni kuwa na afya njema. Jifunze kuumia ili baadae uje uwaajili wasomi na wakuite bosi.
Bado nawakumbusha vijana rudini vijijini mkatumie ardhi ya familia ipasavyo na ukipata nafasi nunua pia ardhi itakusaidia. Limeni kila aina ya mazao yaani mazao ya mda mrefu miti nk na mazao ya mda mfupi mbogamboga na matunda.
KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI