Kama unataka mali utaipata shambani

Kama unataka mali utaipata shambani

Mkuu una dhahabu halafu unaona uvivu kwenda sokoni kuiuza ilhali wanao wakufa kwa njaa na ufukara.

Waza kuhusu ufugaji wa Nguruwe je inakuchukua muda gani kuanza kuuza nguruwe wako ? Je kwa miaka mitano utakuwa na nguruwe wangapi?

Soko la nyama ya nguruwe a.k.a Kitimoto kuna wakati wowote limewahi kupungua mijini?

Umaskini kwetu ni wa kujitakia

"KAMA MNATAKA MALI MTAIPATA SHAMBANI."!
Labda wanipe kidonge nami nimeze niwe mkulima naipenda sana kulima na kufuga ila kunatime moto unakuja alafu unakata navisahau kabisaa na nimeaomea mifugo ila sijawahi juhusisha
 
Nashukuru mleta Uzi wenye fursa kubwa kwangu Mimi na kwa mwingine ,Mwenye uelewa chanya katika jamii yetu inayotuzunguka nadhani yote haya ni kwajili yetu sisi vijana wengi wetu wapenda ajira za kuajiriwa .Kumbe fursa ni nyingi kupitia kilimo zipo nyingi kupita kiasi,cha msingi ni muda mwafaka wakusema "KAMA UNATAKA AJIRA UTAIPA SHAMBANI"
 
Kaka Nchi hii tuna baadhi watu walio lelewa kiajabu sana wanao amini katika ajira kwa sabbu ajira za wazazi wao serikalini pamoja na deal za hapa na pale ndio zilizo walea na kuwakuza, Baba au mama alikuwa mwanasiasa ama mtumishi
Wa mshahara mkubwa na nafasi fulani

Hawa ukiwaambia kuna maisha nje ya Ajira ambayo ni huru zaidi kwao katu hawawezi kukuelewa, Kamwe kwani wanaamini wamenyang'anywa nafasi waliyo stahili kuwepo.
Ukizunguka Tanzania ukaangalia ukubwa wa Ardhi iliyopo na nguvu kazi inayopotea mtaani na kwenye mitandao ya kijamii inauma sana.
kweli chief
 
Kuongeza msisitizo "KAMA MNATAKA MALI MTAIPATA SHAMBANI".
Screenshot_2019-06-02-08-01-47.jpeg
 
Nakumbuka Rais wa awamu ya 4 alisema kizuri kula na wenzio. Wengi walielewa upande mmoja tu wa shilingi ila hata kwenye mafanikio unapofanikiwa kwa kitu fulani jaribu kuwashirikisha wenzio maana kwenye mafanikio usiwe mchoyo kuwambia wenzio.

KIZURI KULA NA WENZIO
 
Matrekta yamekaa tu pale suma jkt badala ya kupelekwa shamba..... unategemea kilimo kitaleta utajiri
Kama walio stahili kulima wanakesha kwenye mitandao ya kijamii kufanya siasa unategemea yataenda wapi? Tunasuburi waje wageni waaanze kuyatumia kulima ndo tupige kelele.
Hata pale Doma nimeona kuna zana za kilimo pia.
 
Waliopo shamban mbona hawapelekewi hayo matrekta
Kama walio stahili kulima wanakesha kwenye mitandao ya kijamii kufanya siasa unategemea yataenda wapi? Tunasuburi waje wageni waaanze kuyatumia kulima ndo tupige kelele.
Hata pale Doma nimeona kuna zana za kilimo pia.
 
Binafsi sidhani kama kuna mtu yupo serious ameenda kuhitaji trekta wakamkatalia, trekta ziko kila mahali, ukienda tamko kibaha zipo, Ukienda Suma Jkt zipo, na kuna kampuni binafsi nyingi tu wana trekta za kuuza. Na zipo show room
Huenda unaziona sabbu kuna uhitaji uhitaji usingekuwepo bila shaka usingeziona.

Kwa maelezo zaidi unaweza wafuata wahusika, natumai hawatasita kukupa ufafanuzi unao uhitaji.
Basi tuendelee na vigezo yakae showroom yalime lami
 
Umeeleweka mkuu.
Lakini Export si inakuja baada ya production? Pale ambapo soko la ndani limezidiwa bila shaka njia ya nje itajitokeza tu, je unajua Mchele kutoka Kyela unauzwa Kenya? Unajua kuwa mahindi ya Mbeya yanauzwa Zambia na Kongo?
Tatizo ni kama serikali hasa awamu hii wanakosa mbinu za kufanya biashara na mataifa mengine nchi kama china wana export zao la nyanya zenye thamani ya zaidi mill 300 za kimarekani lakini wanakiwa wameshajenga mahusiano na nchi husika kwamba sisi tunawauzia nyanya na sisi tunaimport bidhaa zenu
kama serikali wangeisaidia private sector kwa mfumo wanaoenda nao china naamini kabisa mkulima nae angenufaika pia lakini hali ililiyopo sasa mnunuz anapanga bei anayoitaka yeye sababu anauza soko la ndani tu
Juzi hapa rais kapata tenda yakupeleka hayo mahindi tani laki saba huko Zimbabwe lakini sisi hatuhitaji chochote kutoka huko je Zimbabwe wataendelea kununua hayo mahindi wakati hawaoni manufaa kutoka kwetu
 
Tukiachana na ugonjwa wa kuilamu na kuituhumu serikali kwa kila jambo tutayaona mafanikio.
 
Back
Top Bottom