Kama unataka mali utaipata shambani

Kama unataka mali utaipata shambani

Acha uongo. 2003 LA saba then 2010 umemaliza chuo na serving ya bum 130000. Mnapeana moyo na ambayo hayapo.
Mbona nimeisha sahihisha hapo chini? Alafu sijakulazimisha uniamini ni wewe na maisha yako ila fahamu kuwa nilisoma kwa kulipwa boom la 150,000 kila mwezi mkopo asilimia 90 iliyobaki nilikuwa najilipia sikuwai kukaa hostel nilipanga mtaani nilifungua kijiwe kidogo cha chips japo biashara ilikuwa sio nziri ila faida ya buku tano ilikuwa haikosi. Mwisho nililudi nyumbani na 1,300,000/= kwahyo uniamini usiniamini ni wewe tu.
 
Bado nasema na nitazidi kusema kuwa vijana tuamke narudia tena tuamke maana tunasafari ndefu sana, tatizo letu kuwekeza kwenye miradi ya mda mrefu tunaogopa kuwa hatufaidi maana tutakufa, nani ajuaye kuishi kwake? Utaishi miaka zaidi ya 70 ukijitunza na hata zaidi sasa jifikirie utaishije miaka hiyo kama hujawekeza?

Ardhi ndo suruhisho. KAMA UNATAKA MALI UTAIPATA SHAMBANI
 
Tanzania kwnye kilimo hatuna tatizo changamoto kubwa ni masoko mfano tuna mazao mengi ambayo yanapatikana tanzania kwa wingi lakini waziri husika anashindwa kujenga mahusiano na nchi zinazohitaji hayo mazao tungekuwa tunafanya export zaidi ata haya mazao yanayouzwa hapa nchini thamani ingeongezeka sasa ndo hivyo tumebaki kuumia kila siku kila mkulima anatoka na fuso lake la nyanya mkoani wote wanakutana dar
 
Mbona nimeisha sahihisha hapo chini? Alafu sijakulazimisha uniamini ni wewe na maisha yako ila fahamu kuwa nilisoma kwa kulipwa boom la 150,000 kila mwezi mkopo asilimia 90 iliyobaki nilikuwa najilipia sikuwai kukaa hostel nilipanga mtaani nilifungua kijiwe kidogo cha chips japo biashara ilikuwa sio nziri ila faida ya buku tano ilikuwa haikosi. Mwisho nililudi nyumbani na 1,300,000/= kwahyo uniamini usiniamini ni wewe tu.
Wabongo hata ukimpa somo kupitia mifano hai bado wataona uongo, cha msingi umeeleweka mkuu, katika maisha bisha kwa vitendo ndipo ubishe. Endelea kupiga kazi mdau maisha mazuri ya baadaye ni maamzi yako mwenyewe.
 
Tanzania kwnye kilimo hatuna tatizo changamoto kubwa ni masoko mfano tuna mazao mengi ambayo yanapatikana tanzania kwa wingi lakini waziri husika anashindwa kujenga mahusiano na nchi zinazohitaji hayo mazao tungekuwa tunafanya export zaidi ata haya mazao yanayouzwa hapa nchini thamani ingeongezeka sasa ndo hivyo tumebaki kuumia kila siku kila mkulima anatoka na fuso lake la nyanya mkoani wote wanakutana dar
Nadhani ufumbuzi upo ndio maana humsikii mtu wa Ilula pale Kilolo Iringa analalamika humu ndani.
Usisahau tayari Ilula wana kiwanda cha kuchakata zao la nyanya "Dabaga tomato"
Jambo la msingi ni kuanza. Mengine utayakuta mbele ya safari.
 
Mkuu wewe umemsikiliza tu bila kumuuliza maswali na yeye kuwa amefikaje hapo?
Serikali zao zimeamua kumuinua mkulima kwa hali na mali
Hata kama mazao yataharibika wanalipwa fidia na serikali
Mashine kubwa kubwa wanakopeshwa kwa riba ndogo
Mazao yao soko ni guarantee
Kuanzia wakulima na wafugaji wote wanainuliwa na Serikali sana.

Kuna wakati mifugo ilichomwa moto sana kwa sababu ya ugonjwa wa Foot and mouth na wafugaji walilipwa fidia zote
Swali je sisi ni kama wao?

Lingine kuna wanyama wanaitwa badger anaambukiza TB sana mifugo na waliuwawa sana mifugo lakini bunge likasema maadamu Serikali haijadhibiti hao wanyama lazima watu walipwe na wakalipwa

Sisi bado sana ingawa utajiri tunao lakini je Serikali inawasaidiaje wakulima na wafugaji kwa kupanga bei ziambatane na bidhaa za sokoni kwa mahitaji ya kila siku?
Bashe anasema bati zimepanda x2 wakati gunia la mahindi limeporomoka pamoja na mbolea kupanda

Nilitaka kucomment..lakini ww umenisaidia nisicomment..!
 
Tanzania kwnye kilimo hatuna tatizo changamoto kubwa ni masoko mfano tuna mazao mengi ambayo yanapatikana tanzania kwa wingi lakini waziri husika anashindwa kujenga mahusiano na nchi zinazohitaji hayo mazao tungekuwa tunafanya export zaidi ata haya mazao yanayouzwa hapa nchini thamani ingeongezeka sasa ndo hivyo tumebaki kuumia kila siku kila mkulima anatoka na fuso lake la nyanya mkoani wote wanakutana dar
So tuache kulima? Au tuendelee kulima ili taratibu za kutafuta masoko ziendane na uzalishaji?
 
Nadhani ufumbuzi upo ndio maana humsikii mtu wa Ilula pale Kilolo Iringa analalamika humu ndani.
Usisahau tayari Ilula wana kiwanda cha kuchakata zao la nyanya "Dabaga tomato"
Jambo la msingi ni kuanza. Mengine utayakuta mbele ya safari.
Nimeupenda ujumbe wako
 
Hebu jifunze kwa Emmanuel Mgaya. a.k.a Masanja mkandamizaji. Je ni mkulima wa Ulaya? Je, analalamikia soko? Je ana kelele za serikali? Mtu mvivu husema simba yuko njiani..
Tofauti yetu na wao ni kuwa hawa tumbo jembe la mkono,
Wana machine na kuvunia
Wana soko la kuaminika la mazao yao.
 
Nilitaka kucomment..lakini ww umenisaidia nisicomment..!
Basi sio lazima ukachukua wazo langu ila niliweka kama kujifunza. Kwa mwelewe hata hao waliofanikiwa masoko yalikuja baada ya uzalishaji kuwa juu na sio kwamba masoko yalianza hapana.
 
Nadhani ufumbuzi upo ndio maana humsikii mtu wa Ilula pale Kilolo Iringa analalamika humu ndani.
Usisahau tayari Ilula wana kiwanda cha kuchakata zao la nyanya "Dabaga tomato"
Jambo la msingi ni kuanza. Mengine utayakuta mbele ya safari.

Hahhaa kwa hapa una lack of information mkuu...nahakika huelewi sana kuhusu kilimo...!hyo dabaga ipo toka mie nakua...najionea uvv kucomment kwa kirefu...!limeni sie tutanunua mazao fullstop
 
Tulisoma uchumi hata kidogo huwa tunaamini kwa 100% kuwa unapozalisha sana ndipo na soko litafuatwa ila haliwezi kuanza soko kabla ya kuzalisha.

Mfano iringa miaka ya nyuma miti ilibakia kama mapambo ila masoko ya mbao yalipofunguliwa baada ya kuona uzalizaji upo juu wazee wetu na sio vijana walianza kula maisha na walijenga na usafiri wakapata na walisomesha.

UZALISHAJI KWANZA SOKO LITAFUATA
 
Nadhani ufumbuzi upo ndio maana humsikii mtu wa Ilula pale Kilolo Iringa analalamika humu ndani.
Usisahau tayari Ilula wana kiwanda cha kuchakata zao la nyanya "Dabaga tomato"
Jambo la msingi ni kuanza. Mengine utayakuta mbele ya safari.
Ndo mana nasema kama tungekuwa tunaexport zaidi mazao hasa ya biashara thamani ya mazao inge ongezeka
kuletwa kwa kiwanda ni kama kumetatua Changamoto kidogo na sio kumsaidia mkulima kuwa tajiri nimejibu kulingana na mtoa mada anavyosema mali ipo shambani akati watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi
 
Pole, endelea kuwekeza pesa tutakutana sokoni, kifupi wanunuzi pia wanahitajika ili mzunguko wa pesa uwepo hivyo kama umeamua kukaa upande huo ni jambo jema.
Kuhusu Dabaga. Ni kweli kipo lakini mimi nakizungumzia kile kilichojengwa hivi karibuni mara tu baada ya kumaliza mlima kitonga. Kama kungekuwa hakuna uhitaji huo sidhani kama kingejengwa.

Halafu tambua kusafirisha nyanya kuja Kariakoo au Buguruni ni hiyari ya mkulima anaweza akauza pale au akasafirisha kutegemea na bei anayo ona inamlipa.
Hahhaa kwa hapa una lack of information mkuu...nahakika huelewi sana kuhusu kilimo...!hyo dabaga ipo toka mie nakua...najionea uvv kucomment kwa kirefu...!limeni sie tutanunua mazao fullstop
 
Umeeleweka mkuu.
Lakini Export si inakuja baada ya production? Pale ambapo soko la ndani limezidiwa bila shaka njia ya nje itajitokeza tu, je unajua Mchele kutoka Kyela unauzwa Kenya? Unajua kuwa mahindi ya Mbeya yanauzwa Zambia na Kongo?
Ndo mana nasema kama tungekuwa tunaexport zaidi mazao hasa ya biashara thamani ya mazao inge ongezeka
kuletwa kwa kiwanda ni kama kumetatua Changamoto kidogo na sio kumsaidia mkulima kuwa tajiri nimejibu kulingana na mtoa mada anavyosema mali ipo shambani akati watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi
 
Wakati nipo kidato cha nne miaka kadhaa iliyopita nilimwambia mamangu nataka kwenda iringa kwa babu nikamwone ila naomba hela nimchukulie zawadi. Mamangu alisema nitakupa hela ukampe baba inatosha nikamwambia nataka nikampe zawadi mimi kama mimi. Nakumbuka mamangu kwa kuwa familia yetu ilikuwa ahueni alinipa hela nikamnunulia babu viwalo vya maana sana na nilifanya hivyo lengo kuu ni kuomba anipe shamba.

Nilipofika kwa babu nilitoa zawadi zangu na dagaa kama kilo 2 hivi na babu alinogewa sana na mjukuu wake wa kwanza kumuonyesha upendo ule. Babu aliniambia mjukuu wangu naona umekua naomba tuzunguke kwenye miliki zangu za ardhi nikuonyeshe mipaka nikasema haina shida babu, tulizunguka sana karibia masaa 4 maana alikuwa anamiliki mashamba/ mapori zaidi ya eka 500. Mwishoni mwa mizunguko nikaomba shamba akasema unataka kiasi gani nikasema hata eka 25 au 50 zinatosha babu.

Baada ya kuomba alisema nakupa kadri ulivyoomba na ntawambia wajomba zako na mama zako ili baadae wasikusumbue kama ntakufa karibuni. Akanionyesha mwisho wa shamba langu na kuanzia hapo kila likizo nilirudi iringa kuchimba mashimo ya miti na kupanda miti ya mbao na ikumbukwe sikuwashirikisha wazazi hivyo nilitumia mikono yangu na niliombea niwe na afya njema na hakika Mungu akabariki mwili, roho na nafsi vikawa katika usalama.

Hadi sasa namiliki shamba la miti zaidi ya eka 20 na nilianza kupanda mwaka 2009 na sijawahi kutumia kibarua yoyote labda kwa sasa kwa vile nafanya kazi serikalini.

Vijana tuna mda mwingi sana na nyumbani ardhi zipo ila hatujashituka na mda unaenda. TURUDI NYUMBANI YAJAYO YATAFURAHISHA
Ngoja turudi tukawape wazee wetu zawadi walai mi ntawapelekea hata tecno smart nione
 
Back
Top Bottom