SoC02 Kama unahitaji kufanikiwa kwenye jambo lolote, unapaswa kuwa na kasi(speed)

Stories of Change - 2022 Competition

plan z

JF-Expert Member
Jun 10, 2019
1,381
1,414
Katika dunia ya sasa yenye ushindani mkubwa katika nyanja mbalimbali hasa za kiuchumi, kama unahitaji ufanikiwe haraka katika biashara yako au kampuni yako, kasi ni ya muhimu sana. Kama nilivyotangulia kusema dunia ya sasa ni ya ushindani hivyo unapaswa kuwa na kasi katika mambo yako, nitakuambia ni kwanini.

Tuanze na mfano mgumu kisha twende mfano mrahisi, kwa mfano unataka kuandika kitabu ili ukiuze na kitabu hicho kiweze kuisaidia jamii huku na wewe ukinufaika kwa mauzo hayo na upige pesa, kasi yako utakayoitumia kumaliza kitabu hicho ndivyo utakavyoanza kupata pesa haraka kutokana na mauzo.

Mfano pia wewe ni mtaalamu wa kuunda website na unaamua kutengeneza website labda kwa wiki mbili, kwa hiyo kwa mwezi unaunda website mbili tu au moja kabisa kwa mwezi, kwa kufanya hivyo utapata kiwango kidogo kwa uchache huo, lakini kama ukiamua utaunda website kwa siku tatu na ikafanya kazi, ndivyo utakavyojiharakishia kupata pesa mapema kutokana na kasi yako. Kwa wiki mbili mtu ambaye hajui kabisa kuunda website anaweza akajifunza online na akaweza akiwa na bidii.

Una blog yako au "facebook page" na unachapisha andiko moja tu kwa mwezi au unajisahau muda mrefu kisha ndiyo unachapisha andiko lingine, kwanza unafanya wafuatiliaji wako wakusahau na utapata mapato machache kutokana na andiko lako kutokupata wasomaji wengi, tofauti na ukichapisha angalau andiko moja kila siku ili wafuatiliaji wako waweze kurudi kila siku kuchungulia kuna nini kipya umewaletea, kwa kufanya hivyo utawafanya wakukumbuke na wataambiana na utapata wafuasi wengine zaidi.

Kama unatengeneza matangazo ili kuyarusha kwenye radio au televisheni, fanya makubaliano mengi kwa kadri inavyowezekana na kwa muda mfupi, kwa mfano umepanga kuhojiana na upande wa pili na wamekuambia watakuja labda jumamosi na leo ni jumatano, waambie tunawafuata huko kesho na ukishamalizana nao unaangalia kwa wengine, muhimu hapa ni kuwa na kasi na kumaliza mambo kwa haraka.

Kumbuka kasi isikufanye upunguze ubora wa bidhaa au huduma yako, kama ni bidhaa itengeneze kwa ubora na kwa haraka, itangaze kwa haraka ili uiuze kwa haraka, na huduma pia vilevile iwe bora na itolewe kwa haraka, mfano kama unamiliki hospital binafsi, endelea kuhudumia watu kwa haraka na kwa ubora, sio hospital tu, shughuli yeyote ile. Kasi kasi kasi kasi.

Wakati mwingine ndo unaanza biashara na haujaanza kutengeneza faida, labda ni fundi seremala, unaweza ukapata mteja wa kwanza akakupa kianzio ukapata wa pili naye akakupa kianzio, kile kianzio cha wa pili ukakitumia kumtoa yule wa kwanza kwa haraka ukatafuta mwingine watatu ili umtoe wa pili haraka, unaweza ukaona hakuna faida ila kwa kuwa shughuli zinasonga, baada ya muda utashangaa kumbe tayari biashara inakua, hapa kinachotakiwa ni kasi ya wewe kujitangaza ili utambulike na upate wateja watakao kupa hicho kianzio kitakacho mtoa aliyetangulia kwa haraka.

Kama una wazo la biashara yeyote usisubiri wiki nzima bila kuchukua hatua yeyote, anza kutangaza hiyo bidhaa au huduma hata kama huna mtaji, ukipata mteja wa kwanza unaenda unamnunulia na kisha faida unayopata unabaki nayo, kikubwa hapa ni usipoteze wiki, mwezi, miezi, mwaka hata miaka na wazo lako kabla ya kulifanyia kazi, ni bora ukajaribu kulifanyia kazi kisha ukashindwa kuliko kutokujaribu.

HITIMISHO.
Kasi yako katika jambo lolote ndiyo itakufanya ulikamilishe kwa upese na kupata faida yake kwa haraka. Usilipue, fanya kitu kwa ubora ila kwa haraka, ukiwa na wazo usibaki nalo muda mrefu bila kulifanyia kazi, kwa kufanya hivyo utanufaika mapema.

Kama umebarikiwa na andiko hili nijulishe kwenye maoni hapo chini, pia kura yako ni muhimu.
 
Back
Top Bottom