Kama Una Akaunti ya Mitandao ya Kijamii Uliyoisahau au Hutumii Tena, Nenda Ukaihakiki Mara Moja

Kama Una Akaunti ya Mitandao ya Kijamii Uliyoisahau au Hutumii Tena, Nenda Ukaihakiki Mara Moja

Naipenda nchi yetu

New Member
Joined
Sep 18, 2025
Posts
3
Reaction score
4
Ndugu wanajukwaa, Naomba jamii iwe makini na kuchukua tahadhari inapostahili, hasa katika kipindi hiki ambacho mijadala kuhusu matukio ya mauwaji ya Oktoba 29 hadi Novemba 4 pamoja na maandalizi ya maandamano ya Desemba 9 yamezidi kushika kasi.

Leo nimejulishwa na rafiki yangu kuhusu matumizi yasiyoeleweka ya akaunti yangu ya zamani ya Facebook. Akaunti hiyo niliiacha kutumia takribani miaka kumi iliyopita, lakini ghafla imeonekana ikitoa kauli za vitisho dhidi ya wananchi wanaozungumzia mabadiliko ya nchi. Kauli hizo ambazo si zangu, sina uhusiano na vyombo vya ulinzi na usalama na sijawahi kushiriki katika vitendo vinavyohusisha vitisho kwa raia. Mimi binafsi natamani kuona mabadiliko yenye maslahi kwa taifa letu.

Kutokana na tukio hilo tulilazimika kufuatilia kwa kina ili kufahamu kinachoendelea. Katika ufuatiliaji huo tumegundua kuwa hata ukurasa wa rafiki yetu aliyefariki dunia takribani miaka mitano iliyopita umeonekana ukiweka machapisho mapya yasiyoendana na historia ya marehemu ilihali rafiki yetu alikwishafariki. Matukio kama haya yameanza kuripotiwa na watu mbalimbali wanaodai kuwa kurasa zao za zamani, hususan za Facebook, zimeonekana zikidukuliwa na TCRA, na kutumiwa bila idhini yao.

Natoa taarifa hii kwa sababu naamini ni muhimu kwa jamii kuwa na tahadhari. Nawasihi wenzangu mkague akaunti zenu za zamani, muimarishe usalama wa taarifa zenu (Updates) mtandaoni na mtoe taarifa kwa mamlaka husika (hapa namaanisha META wenyewe) endapo mtagundua matumizi yasiyo ya kawaida katika majina yenu.

Lengo langu si kuleta taharuki, bali kuhimiza umakini na ulinzi wa taarifa binafsi, kwa sababu usalama wa utambulisho wetu wa kidijitali ni sehemu muhimu ya usalama wetu kama raia.

Naipenda nchi yetu.
 
Back
Top Bottom