Kama umeguswa saidia watoto hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama umeguswa saidia watoto hawa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by TIQO, Jan 11, 2012.

 1. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Na Mwandishi wetu
  KATIKA gazeti la Uwazi, toleo la wiki iliyopita tulitoa habari za mtoto Mustafa Ally, 12, (pichani), mkazi wa Mtoni Mtongani, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam anayewauguza wadogo zake mapacha wenye umri wa miezi nane.
  Mtoto Mustafa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Twiga, Temeke amelazimika kuwauguza wadogo zake hao, Swaumu na Ramadhani kwa kuwa baba yao alishafariki na mama yao yupo mahututi.
  Watoto hao mapacha wanaumwa na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu. Mama yao aliyekuwa akiwauguza aliugua ghafla na kupewa matibabu na kwa sasa yupo hoi nyumbani kwake, hivyo Mustafa kuchukua mzigo huo wa kuwauguza.
  Matatizo yanayoikabili familia hiyo ni pamoja na ukosefu wa chakula, nguo za kawaida na za shule, fedha za matumizi, maziwa ya unga ya watoto na kodi ya nyumba.
  Gazeti hili kwa niaba ya familia hiyo linatoa shukrani kwa watu mbalimbali waliompatia msaada wa maziwa, sabuni, sukari, nguo na fedha, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 300,000.
  Bado msaada unakaribishwa kwa watoto hawa. Aliyeguswa na kilio cha mtoto Mustafa afanye mawasiliano na Afisa Ustawi wa Jamii Muhimbili, Erika Ishengoma kwa simu 0714 220 038 au mwandishi wetu kwa namba 0713 454 656 au afike Muhimbili wodi ya watoto, Makuti B atakutana nao ana kwa ana.

  [​IMG]

  Mtoto Mustafa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Twiga, Temeke amelazimika kuwauguza wadogo zake hao, Swaumu na Ramadhani kwa kuwa baba yao alishafariki na mama yao yupo mahututi.

  Source: Global Publishers
   

  Attached Files:

 2. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Jamani akina baba, mama, dada, kaka tuwekeni kando lawama na sihasa tuwasaidie hawa watoto ili waokoe maisha yao na wao waishi kama sisi wengine tunavyo ishi.
   
 3. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  dunia mapito wapendwa!! kutoa ni moyo na si utajiri
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,142
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  very sory, i hop MUNGU atawalinda watoto hao. AMINA
   
 5. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mungu atawasaida, mimi niko mbali tu lakini ningepita kuwasaidia.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Too bad!
  Really paining!
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Duh, inasikitisha sana.
   
 8. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mkuu fanya kama yule member aliye fiwa na mkewe. Kutoa ni moyo chochote ulicho nacho
  Fikiria dogo huyo wa darasa la sita ndo anauguza hao watoto mapacha mama ake yupo mahututi nae.
   
 9. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tujitoleeni jamani, leo kwao kesho kwetu!!
   
 10. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Kuna namba za simu umepewa, watumie hata kwa tigo rusha, au tigo pesa, sawa baba yangu?
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Unakanyagwa
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Muhimbili na watumishi wao siwaamini bora tutume kwa huyo mwandishi wa habari
   
 13. Kitope

  Kitope JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Penye nia, Njia haikosekani mkuu!! Hata mimi niko mbali tena sana tu kutoka kwetu!! Lakini No doubt wengi wetu tunaoishi mbali na nyumbani huwa tunafanya mengi tu bila sisi wenyewe kuwepo. kwani kuna watu huwa wantuwakilisha. Piga moyo konde kakaa!
   
 14. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Wafanyakazi wa Muhimbili watageuza mtaji hawa bora kwa mwandishi
   
Loading...