Kama Uliacha Kufanya Haya Kwa Mke wako. Jua umeoa Uliyoyataka mwenyewe

Ndugu Waafrika. Tumeacha Mema kwa Mambo mafupi yanayopita na Kudandia Tamaduni za Hovyo

Wazee wetu waliangalia haya Kabla Hawajamruhusu Mtoto wao kuoa /kuolewa
Walichunguza Familia ya Binti
Walichunguza Jina la Binti
Walichunguza ukoo
Walichunguza magonjwa

Walichunguza Familia Ya Binti
Familia ya Binti huchunguzwa kwa sababu binti ndio anaenda Kuolewa. Familia zilizojaa Ushirikina, wambea watu wasiofaa katika jamii. Hawa Mabinti zao ilikuwa ni ngumu sana kupata wanaume wa Kuwaoa. Ni familia zilizokuwa zinaepukwa Sana. Na Kumbuka Wazee Walikuwa wanazungumza na Familia husika na Kuwa karibu nazo Kabla Watoto wao hawajaoana

Walichunguza Jina la Binti
Jina ni kitu kikubwa kuliko watu wanavyodhani. Unapompatia Mwanao jina Hakikisha Jina Hilo lina maana na Linaendana na Wakati na Epuka kabisa kumpatia mtoto wako jina la Ndugu wako au Babu zako au wajomba zako wa Nyuma. Wazee wetu Walichunguza majina maana Kuna Watu wamepewa majina Kumbe hayo majina Yalikuwa mabaya huko nyuma. Unampatia Jina Mtoto wako kutoka kwa Mjomba sijui Bibi. Kumbe huyo Bibi alishawahi kuwa mchawi.. Mshirikina.. Mwizi wa wanaume za watu. Mwizi wa mali. Malaya.. N. K n. K

Kwahiyo majina Hayo yalichunguzwa na Kama yalitakiwa kurekebishwa Basi Yalirekebishwa ili hizo tabia zisimpate Mtoto.

Hayo yaliyobaki Kwa akili timamu unajua kabisa Walichunguza mengi.

Sasa Wakati huu
Mwanaume anakutana na binti club, Sherehe za Harusi, Ukumbini, kwenye semina,barabarani n.k Tamaa zinamjaa anaona Huyu anafaa kuwa mke (nani kakuambia)

Mabinti wengi Mnaowaona Kama hamjawachunguza Jueni wametoka na Mambo yao huko kwao na kwenye Ukoo wao ambayo ww huyaelewi na Yatakutesa na Ndicho ulichokioa hicho ndugu yangu. Unamuoa Binti kumbe Wazazi wake au ndugu au Babu zake na Bibi zake walishamlaani huko na Kumtamkia maneno kama Vile (popote utakapoenda Hutofanikiwa, utakapoenda Na ukiolewa hutopata mtoto, utakapoenda Mwanaume utakayekuwa naye hatofanikiwa, Utakapoenda Hutoweza tulia na Mwanaume mmoja )

Baada ya Hayo unakuja Kulalamika ooh Ss hivi mke wangu ndio unaonyesha Makucha. Hapana ndugu ulioa Matatizo hayo kabla hujayarekebisha. Ulioa mchoyo.. Ulioa mmbea.. Ulioa Mchawi. Ulioa mtu asiyejua Kujitunza mwenyewe kimwili na mambo ya Hapa Na Pale usiyoyajua Binti katoka nayo wapi

Wazee wetu walijua Familia nyingi zina mambo yao Na Matatizo Lukuki na Mambo mengi yanarithishwa kwa Vizazi vyao. Kwahiyo walipochunguza Walijua Ukoo fulani una Mambo Haya na Haya na Kuamua kuyarekebisha Mambo hayo yasiendelee na Kama Ni mambo mabaya zaidi ukoo huo Ulikuwa huwezi kwenda kuoa Hapo hata Siku moja. Mabinti wa Pale walikimbiwa na Watu hata kama Walikuwa na Uzuri wa Kuvutia Kila Wanaume.

Sasa Mabinti hao ndio Wanaona Bora wayakimbie maeneo wanayotambulika kwa sana na Mambo ya Ukoo wao na kukimbilia miji ya Mjini ambayo watu wengi hawawajui. Sasa wanakutana na Wewe usiyejielewa pia Unamuona Binti Keshafika mjini unamchunguza Ki mjini mjini. Eti ameshakuwa na Wanaume wangapi.. Mara anajua kupika..na mambo yasiyokuwa na Juu wala chini unajiridhisha kwa Mambo ya Hovyo unamuweka Ndani. Kumbe kuna Mambo ya Ki roho huyajui yanakuja Kukuibukia Unaanza Kutafuta Waganga wakutibie

Ndugu zangu Dunia Hii ina Roho za kila Aina chunguzeni Roho hizo kutoka Katika sehemu mnayoenda kuoa au kuolewa. Kuna Koo zingine Hazifai kuoa

ASANTENI
Siku hizi tunatazama amefungasha ukubwa kiasi gani nyuma
 
Ni nadra sana kukuta mwanamke mwenye tabia njema anatoka kwenye familia ya hovyo.

Na hata kama mwanamke anatabia njema lakini anatoka kwenye familia ya hovyo, basi sioni kama kuna shida hapo maana unaemuoa ni yeye na sio familia yake.

Ndugu unajua nini maana ya Laana.? Ukoo fulani umelaaniwa? Basi Nenda Kaoe ukiwa unajua Kwamba Sehemu fulani kuna Laana Fulani halafu sema Mimi sioi Familia naoa Mwanamke

Chunguza Ndugu yangu hata kama Umemkuta Mtu anatabia Njema Maana Watu huiga tabia ili Wakuteke uoe. Atajifanya anajua Mapenzi kumbe ndio anakuua hivyo.
 
Japo mimi siamini hilo suala la laana ya ukoo.

Tuseme ni jambo baya ambalo lipo kwa ukoo mzima, so hata huyo mwanamke naye atakuwa aningia, hivyo nayeye hatokufaa.

Au hii laana inakuwa kwa ukoo wa mwanamke ukimtoa yeye.
 
Kwa hiyo niwape watoto majina Kama ;Mahindi,Mtama,Mbelewele...sivyo?
Kama Unaona Kuwaita Watoto wako majina ya Mazao ndio bora Waite ndugu. Mimi nimekuambia Kwamba Unapompa Mtoto wako jina Chunguza Kwanza Jina Hilo asili yake. Unaweza Mpa Hata jina Lolote Unalolijua kikubwa Jua Asili yake na Mambo gani mazuri na Mabaya yaliyopo kwenye Hilo Jina
 
Mapenzi ni uduanzi tu,,, kama unaoa wewe oa tu..

Liwalo na liwe...

Tupo nje ya muda sana,, tusiupoteze kwenye upuuzi
 
Sijui unazungumzia ndoa za vijijini au mijini, ndoa nyingi za mijini zinaanzia njiani na kumalizia njiani, wahusika wanaofanikisha ndoa huwa hawajuani, wanaooana hawajuani na watoto wao kama wakibahatika hawatakujua kwao zaidi ya hapo mjini waishipo na hii ni kwa sababu baba na mama makwao hakueleweki kitu, ukienda itabidi utafute pakufikia, baba na mama wanamjua mzazi mmoja au pengine hata huyo mmoja hawamjui yuko wapi! Siku ya harusi wanaombwa watu wawe eti baba na mama wakwe! Wote hawa makabila tofauti na wao pia hawajui makwao! Ukweli tuko wakati mgumu na mbaya ambapo vijijini kwetu kumekufa kwani vijana tulikukimbia.
Sasa Imagine ndugu wewe umekimbia Huko Kwa Sababu pamevurugika Unategemea Roho zilizovuruga huko Kwenu Zitakuacha Wewe uendelee kujijenga Vizuri mahali Ulipo.

Sasa Imagine mnakutana na Mwanamke na Yeye kakumbia Huko huko Kwao kwa Sababu ya Mambo ya Hovyo hovyo. Mtakuwa mnajenga Kweli au mnabomoa.
 
Huko hakupo tena kulikwisha sambaratika hakuna mtu ni magofu matupu.
 
Ndugu Waafrika. Tumeacha Mema kwa Mambo mafupi yanayopita na Kudandia Tamaduni za Hovyo

Wazee wetu waliangalia haya Kabla Hawajamruhusu Mtoto wao kuoa /kuolewa
Walichunguza Familia ya Binti
Walichunguza Jina la Binti
Walichunguza ukoo
Walichunguza magonjwa

Walichunguza Familia Ya Binti
Familia ya Binti huchunguzwa kwa sababu binti ndio anaenda Kuolewa. Familia zilizojaa Ushirikina, wambea watu wasiofaa katika jamii. Hawa Mabinti zao ilikuwa ni ngumu sana kupata wanaume wa Kuwaoa. Ni familia zilizokuwa zinaepukwa Sana. Na Kumbuka Wazee Walikuwa wanazungumza na Familia husika na Kuwa karibu nazo Kabla Watoto wao hawajaoana

Walichunguza Jina la Binti
Jina ni kitu kikubwa kuliko watu wanavyodhani. Unapompatia Mwanao jina Hakikisha Jina Hilo lina maana na Linaendana na Wakati na Epuka kabisa kumpatia mtoto wako jina la Ndugu wako au Babu zako au wajomba zako wa Nyuma. Wazee wetu Walichunguza majina maana Kuna Watu wamepewa majina Kumbe hayo majina Yalikuwa mabaya huko nyuma. Unampatia Jina Mtoto wako kutoka kwa Mjomba sijui Bibi. Kumbe huyo Bibi alishawahi kuwa mchawi.. Mshirikina.. Mwizi wa wanaume za watu. Mwizi wa mali. Malaya.. N. K n. K

Kwahiyo majina Hayo yalichunguzwa na Kama yalitakiwa kurekebishwa Basi Yalirekebishwa ili hizo tabia zisimpate Mtoto.

Hayo yaliyobaki Kwa akili timamu unajua kabisa Walichunguza mengi.

Sasa Wakati huu
Mwanaume anakutana na binti club, Sherehe za Harusi, Ukumbini, kwenye semina,barabarani n.k Tamaa zinamjaa anaona Huyu anafaa kuwa mke (nani kakuambia)

Mabinti wengi Mnaowaona Kama hamjawachunguza Jueni wametoka na Mambo yao huko kwao na kwenye Ukoo wao ambayo ww huyaelewi na Yatakutesa na Ndicho ulichokioa hicho ndugu yangu. Unamuoa Binti kumbe Wazazi wake au ndugu au Babu zake na Bibi zake walishamlaani huko na Kumtamkia maneno kama Vile (popote utakapoenda Hutofanikiwa, utakapoenda Na ukiolewa hutopata mtoto, utakapoenda Mwanaume utakayekuwa naye hatofanikiwa, Utakapoenda Hutoweza tulia na Mwanaume mmoja )

Baada ya Hayo unakuja Kulalamika ooh Ss hivi mke wangu ndio unaonyesha Makucha. Hapana ndugu ulioa Matatizo hayo kabla hujayarekebisha. Ulioa mchoyo.. Ulioa mmbea.. Ulioa Mchawi. Ulioa mtu asiyejua Kujitunza mwenyewe kimwili na mambo ya Hapa Na Pale usiyoyajua Binti katoka nayo wapi

Wazee wetu walijua Familia nyingi zina mambo yao Na Matatizo Lukuki na Mambo mengi yanarithishwa kwa Vizazi vyao. Kwahiyo walipochunguza Walijua Ukoo fulani una Mambo Haya na Haya na Kuamua kuyarekebisha Mambo hayo yasiendelee na Kama Ni mambo mabaya zaidi ukoo huo Ulikuwa huwezi kwenda kuoa Hapo hata Siku moja. Mabinti wa Pale walikimbiwa na Watu hata kama Walikuwa na Uzuri wa Kuvutia Kila Wanaume.

Sasa Mabinti hao ndio Wanaona Bora wayakimbie maeneo wanayotambulika kwa sana na Mambo ya Ukoo wao na kukimbilia miji ya Mjini ambayo watu wengi hawawajui. Sasa wanakutana na Wewe usiyejielewa pia Unamuona Binti Keshafika mjini unamchunguza Ki mjini mjini. Eti ameshakuwa na Wanaume wangapi.. Mara anajua kupika..na mambo yasiyokuwa na Juu wala chini unajiridhisha kwa Mambo ya Hovyo unamuweka Ndani. Kumbe kuna Mambo ya Ki roho huyajui yanakuja Kukuibukia Unaanza Kutafuta Waganga wakutibie

Ndugu zangu Dunia Hii ina Roho za kila Aina chunguzeni Roho hizo kutoka Katika sehemu mnayoenda kuoa au kuolewa. Kuna Koo zingine Hazifai kuoa

ASANTENI
Umeongea point sana japo wachangiaji wengi humu ni watoto miaka 15-30 hawawezi kuelewa unachoongea ila ni ukweli mtupu na ndio maana ndoa siku hizi hazidumu kama zamani
 
Hujaongexa hapo ubikra kwasasa watakwambia technolojia
Ndugu ukitaka kujua mambo ya Uchunguzi yana nguvu zake katika mahusiano. Hebu pata Mwanamke ambaye si Bikra kama Una akili timamu kuna Jambo litakujia Kichwani tu huyu keshatumika. Kwahiyo Kama Ulikuwa na Imani kwa Asilimia 100 basi zitashuka kwa kiasi Chake.

Ndio maana Kuna Ndoa Wanawake wataanza Kuwasiliana na Wanaume waliowahi Kushiriki nao na Wengine wakikosa Mambo waliyoyapata kwa Ex zao kutoka kwako basi Jua Mahusiano yenu hayotokuwa na Amani ndani yake. Kuna Nguvu kubwa sana kwenye Bikra za Wanawake na Zikichezewa hovyo hovyo na Wanaume ambao hawajitambui Na Hawajafundwa Vyema Wanaleta Balaa kwa Wale watakaowaoa Hao Wanawake.

Ugomvi kidogo ndani atapeleka mawazo nje ya Mahusiano yenu na Pengine kutafuta Faraja Huko
 
Japo mimi siamini hilo suala la laana ya ukoo.

Tuseme ni jambo baya ambalo lipo kwa ukoo mzima, so hata huyo mwanamke naye atakuwa aningia, hivyo nayeye hatokufaa.

Au hii laana inakuwa kwa ukoo wa mwanamke ukimtoa yeye.
Laana Ndugu zipo. Kama ww ni muumini wa Dini Fulani basi hata Kwenye vitabu vya dini Mungu Alitoa Laana humu ukisoma na Inaathiri Jamii nzima iliyopewa hiyo laana.

Sasa Kama Mke mtarajiwa Amepata Laana Hiyo. Mfano Mke wako mtarajiwa alishawahi kuwatukana wazazi wake au Bibi zake au hata wajomba zake wakati wa ukuaji wake na kuwadharau kisa tu amefika Mjini au Kufanikiwa kwa Kiasi fulani. Then wazazi wake wakamlaani kwa kumtamkia maneno fulani(Hutofika mbali,utaangaika maishani,hutodumu kwenye ndoa yako,hutopata mtoto) maneno hayo jua Yanaishi na kuna siku yatatimia.

Sasa ww umekutana na mwanamke huyo ukaweka Ndani bila Kujua lolote lile utegemee hayo Maneno yakianza Kutimia Basi Uwe tayari kuyabeba
 
Back
Top Bottom