Kama Uliacha Kufanya Haya Kwa Mke wako. Jua umeoa Uliyoyataka mwenyewe

FabNXTzqEtcgazfbjjfo

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
1,472
1,828
Ndugu Waafrika. Tumeacha Mema kwa Mambo mafupi yanayopita na Kudandia Tamaduni za Hovyo

Wazee wetu waliangalia haya Kabla Hawajamruhusu Mtoto wao kuoa /kuolewa
Walichunguza Familia ya Binti
Walichunguza Jina la Binti
Walichunguza ukoo
Walichunguza magonjwa

Walichunguza Familia Ya Binti
Familia ya Binti huchunguzwa kwa sababu binti ndio anaenda Kuolewa. Familia zilizojaa Ushirikina, wambea watu wasiofaa katika jamii. Hawa Mabinti zao ilikuwa ni ngumu sana kupata wanaume wa Kuwaoa. Ni familia zilizokuwa zinaepukwa Sana. Na Kumbuka Wazee Walikuwa wanazungumza na Familia husika na Kuwa karibu nazo Kabla Watoto wao hawajaoana

Walichunguza Jina la Binti
Jina ni kitu kikubwa kuliko watu wanavyodhani. Unapompatia Mwanao jina Hakikisha Jina Hilo lina maana na Linaendana na Wakati na Epuka kabisa kumpatia mtoto wako jina la Ndugu wako au Babu zako au wajomba zako wa Nyuma. Wazee wetu Walichunguza majina maana Kuna Watu wamepewa majina Kumbe hayo majina Yalikuwa mabaya huko nyuma. Unampatia Jina Mtoto wako kutoka kwa Mjomba sijui Bibi. Kumbe huyo Bibi alishawahi kuwa mchawi.. Mshirikina.. Mwizi wa wanaume za watu. Mwizi wa mali. Malaya.. N. K n. K

Kwahiyo majina Hayo yalichunguzwa na Kama yalitakiwa kurekebishwa Basi Yalirekebishwa ili hizo tabia zisimpate Mtoto.


Hayo yaliyobaki Kwa akili timamu unajua kabisa Walichunguza mengi.

Sasa Wakati huu
Mwanaume anakutana na binti club, Sherehe za Harusi, Ukumbini, kwenye semina,barabarani n.k Tamaa zinamjaa anaona Huyu anafaa kuwa mke (nani kakuambia)

Mabinti wengi Mnaowaona Kama hamjawachunguza Jueni wametoka na Mambo yao huko kwao na kwenye Ukoo wao ambayo ww huyaelewi na Yatakutesa na Ndicho ulichokioa hicho ndugu yangu. Unamuoa Binti kumbe Wazazi wake au ndugu au Babu zake na Bibi zake walishamlaani huko na Kumtamkia maneno kama Vile (popote utakapoenda Hutofanikiwa, utakapoenda Na ukiolewa hutopata mtoto, utakapoenda Mwanaume utakayekuwa naye hatofanikiwa, Utakapoenda Hutoweza tulia na Mwanaume mmoja )

Baada ya Hayo unakuja Kulalamika ooh Ss hivi mke wangu ndio unaonyesha Makucha. Hapana ndugu ulioa Matatizo hayo kabla hujayarekebisha. Ulioa mchoyo.. Ulioa mmbea.. Ulioa Mchawi. Ulioa mtu asiyejua Kujitunza mwenyewe kimwili na mambo ya Hapa Na Pale usiyoyajua Binti katoka nayo wapi

Wazee wetu walijua Familia nyingi zina mambo yao Na Matatizo Lukuki na Mambo mengi yanarithishwa kwa Vizazi vyao. Kwahiyo walipochunguza Walijua Ukoo fulani una Mambo Haya na Haya na Kuamua kuyarekebisha Mambo hayo yasiendelee na Kama Ni mambo mabaya zaidi ukoo huo Ulikuwa huwezi kwenda kuoa Hapo hata Siku moja. Mabinti wa Pale walikimbiwa na Watu hata kama Walikuwa na Uzuri wa Kuvutia Kila Wanaume.

Sasa Mabinti hao ndio Wanaona Bora wayakimbie maeneo wanayotambulika kwa sana na Mambo ya Ukoo wao na kukimbilia miji ya Mjini ambayo watu wengi hawawajui. Sasa wanakutana na Wewe usiyejielewa pia Unamuona Binti Keshafika mjini unamchunguza Ki mjini mjini. Eti ameshakuwa na Wanaume wangapi.. Mara anajua kupika..na mambo yasiyokuwa na Juu wala chini unajiridhisha kwa Mambo ya Hovyo unamuweka Ndani. Kumbe kuna Mambo ya Ki roho huyajui yanakuja Kukuibukia Unaanza Kutafuta Waganga wakutibie

Ndugu zangu Dunia Hii ina Roho za kila Aina chunguzeni Roho hizo kutoka Katika sehemu mnayoenda kuoa au kuolewa. Kuna Koo zingine Hazifai kuoa

ASANTENI
 
Kuhusu jina hapo umepuyanga kwa kweli..wala haina uhusiano kabisa na tabia ya mtu..kuna akina yohana majambazi..kuna akina mudi mashoga..kuna wakina mariamu malaya wa kutupa...so naomba dhana ya jina ondoa kabisa.

Camsingi lea mtoto katika mazingira yote rafiki kwa ukuaji mzuri wa tabia njema.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mchaga kwa msukuma/mmasai/mnyakyusa
Msambaa kwa waha/wandigo
mluguru kwa mkinga
Mhehe kwa mhaya/mfipa
mrangi kwa mmakonde etc

tambua mbinguni hamuna kuoa wala kuolewa, ishi kadiri ya kitabu cha maisha yako, usinakili vya wenginee utaangukia pua
 
We nae hata hutumii akili. Zamani watu walikuwa wachache...wanaishi kwenye jamii ya watu wachache, hawahami hami kama siku hizi kutoka mji mmoja kwenda mwingine.
Labda pia shule ni hapo hapo kasoma na kufia hapo hapo.

Siku hizi unakutana na mtu masafa huko kabila lingine huo muda tunautoa wapi wa kuanza kuchunguzana? Dunia inatupeleka jinsi inavyoenda kuna mambo hatutaweza kuyacontrol ni kuyaacha tu yawe hivyo.
Labda twende kidigitali zaidi tutumie private investigators
 
We nae hata hutumii akili. Zamana watu walikuwa wachache...wanaishi kwenye jamii ya watu wachache, hawahami hami kama siku hizi kutoka mji mmoja kwenda mwingine.
Labda pia shule ni hapo hapo kasoma na kufia hapo hapo.

Siku hizi unakutana na mtu masafa huko kabila lingine huo muda tunautoa wapi wa kuanza kuchunguzana? Dunia inatupeleka jinsi inavyoenda kuna mambo hatutaweza kuyacontrol ni kuyaacha tu yawe hivyo.
Si kwamba hajatumia akili.Katumia.Ila haujaridhika na kiwango alichokitumia.
 
Kwani Biblia ilisema tuchungaze kwanza au tuliagizwa tuje tuijaze dunia?

hebu tuleteeni michongo ya kusaka pesa mambo ya kuchunguza tuyaache maabara huko
Ushajiuliza kwanini Unatafuta Pesa? Familia ndio msingi mkubwa wa wewe mwanaume kuangaika. Sasa Tafuta pesa Halafu Uje kupata Mwanamke mshirikina akutoe Uhai wako amiliki mali
 
Kuhusu jina hapo umepuyanga kwa kweli..wala haina uhusiano kabisa na tabia ya mtu..kuna akina yohana majambazi..kuna akina mudi mashoga..kuna wakina mariamu malaya wa kutupa...so naomba dhana ya jina ondoa kabisa.

Camsingi lea mtoto katika mazingira yote rafiki kwa ukuaji mzuri wa tabia njema.

#MaendeleoHayanaChama
Wewe tatizo lako unahisi jina La Kwenye Biblia Ndio jina Sahihi. Unajua Asili ya Hayo Majina? Yohana sijui Petro sijui Mariamu unajua Asili yake au Mnayaitaga Tu watoto wenu. Ndio maana Nikasema Jina Lolote linaweza Kuwa Laana Kwa Mtoto. Paulo pia alikuwa mmuaji na Mtesaji
 
Wewe tatizo lako unahisi jina La Kwenye Biblia Ndio jina Sahihi. Unajua Asili ya Hayo Majina? Yohana sijui Petro sijui Mariamu unajua Asili yake au Mnayaitaga Tu watoto wenu. Ndio maana Nikasema Jina Lolote linaweza Kuwa Laana Kwa Mtoto. Paulo pia alikuwa mmuaji na Mtesaji
Tupendekezee majina mkuu.
 
Life is not so serious kiasi hiko

Mmeelewana weka ndani enjoy maisha, akizingua tupa nje.

Endelea na maisha.
Ukitaka Kujua Kuna MATATIZO soma Nyuzi za Binadamu wa Humu JF kwenye hizo Ndoa. Wewe unaongea Kirahisi rahisi. Ngoja Uje ufanyiwe haya

Kupumbazwa kila anachotaka unafanya
Ukiwa na mali anakupiga Ugonjwa hujitambui
Ukoo wako huwezi usaidia zaidi ya Wa Kwake
 
Back
Top Bottom