Nebuchadinezzer
JF-Expert Member
- Oct 1, 2018
- 1,403
- 2,550
Sio kila kitu kinachosemwa na wengi ni sahihi siku zote. Kumuhudumia mtu umpendaye ni kitu cha kawaida na kimekuwepo tangu kuanza kwa maisha ya mwanadamu chini ya jua. Nadhani hii kauli ya "mchumba hasomeshwi" ni matokeo ya kutokuelewa maana halisi ya mchumba na uchumba.
Kumsomesha mchumba hakuna tofauti na kumpeleka mchumba wako hospitalini awapo mgonjwa. Au kumpatia chakula awapo na njaa. Ni moja ya huduma za kawaida. Unapojitolea kumsomesha mchumba wako unatakiwa ujitolee. Usitegemee malipo makubwa sana maana kusomesha ni kutoa huduma.
Nichukue nafasi hii kuwatia moyo vijana wote wanaosomeshwa au kusomesha kuwa hawajakosea kufanya hivyo. Somesheni kadri muwezavyo, akibadilika ni matokeo tu.