Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,635
- 729,557
Naweza kuonekana chizi kiwango cha rough road kutokana na hii mada
Mwaka jana kuna mtu alitengeneza video inayoonyesha duka maarufu la vipuri vya magari la KISANGANI likiwa limefungua tawi jingine linalodili na vipuri vya binadamu.
Ndani ya hilo duka kuna vipuri mbali mbali vya binadamu kuanzia akili(IQ) za viwango tofauti midomo inayojua kusuta miguu nk nk.
Technology imefika mbali sana siku hizi simu ikikuzingua kuna sehemu ya kuifanyia rooting ama kuna sehemu ya kuifanyia factory data reset yani hapa simu inarudi upya kwenye roho yake kama ilivyozaliwa(sio hili ganda la nje)imagine kama ni binti anataka kuwa mwanamwali tena (Tanga zipo hizi lakini bahati mbaya wakamruhusu mvimba macho awaibie ujuzi).
Wazungu hawalali wanajaribu kwa njia zote kufanya hili liwezekane
Kuufanyia mwili
Overhaul
Rooting
Factory data reset
Kwamba hatutahitaji tena hospital za vichaa, mtu akiugua tu uchizi anafanyiwa rooting ama factory data reset anakuwa mpya yule yule wa awali bila uchizi.
Kijana akiathirika tu na madawa ya kulevya huhitaji kumpeleka sober house...unamfix tu anakuwa sawa...tungeokoa vijana wengi sana
Wenzetu wako mbali sana kwenye hili ukiichoka jinsia yako unaenda hospital kufanyiwa upasuaji unapewa jinsia nyingine na siku ukihitaji kurudia asili yako nadhani wanakurudisha.
Kama hii kitu ikiwezekana tutaokoa
Ndoa nyingi sana (hakuna kuzeeka)
Walevi wengi sana
Wezi wengi sana nknk
Nyoka ndie kiumbe hai pekee aliyepewa neema hii ya kujifanyia factory data reset anapozeeka! Nyoka huyuhuyu aliyemdanganya Eva (Hawa)kuna siri kubwa hapa.
Inawezekana kabisa tukadhani hiki ni kitu cha kufikirika kisichowezekana kabisa lakini huko tuendako hili litakuja kutokea.