Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,940
Kwa muundo wa Muungano wetu, hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu, mkweli wa nafsi na asiye mnafiki, anayeweza kutetea kuwa muundo huu uliopo upo sawa sawa.
Ndiyo maana watu wote maarufu, wenye akili na maadili yasiyotia shaka, bila ya kujali vyama vyao, dini zao au umri wao, hakuna hata mmoja atakuambia kuwa muundo wetu wa Muungano upo vizuri.
Ndiyo maana Kinana alipotaka kuupinga ukweli, alionekana kujidhalilisha zaidi na kuonekana mtu mnafiki na aliyekosa uzalendo, kwa sababu alishindwa kuzijibu hoja za Lisu, Jaji Nyalali, Jaji Warioba, Wabunge G55, akaishia kupiga porojo.
Lisu, kwenye suala la Muungano, alichokisema hazikuwa porojo, hayakuwa majungu bali aliuongea ukweli mtupu. Kwenye ukweli, hata umlete nani, hataweza kuufanya uonekane ni uwongo. Zaidi kitakachotokea ni kumdhalilisha na kumvunjia heshima huyo mtu anayeukana ukweli, kama ilivyotokea kwa Kinana.
Hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu, awe CCM, CHADEMA, ACT au asiye na chama, ambaye atasema muundo wa Muungano huu uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar, upo sawa:
Tume ya Warioba ilitamka muundo wa Muungano upo hovyo.
Wabunge 55 wa CCM, walitamka kuwa muundo wa Muungano upo hovyo. Wakaungwa mkono na wabunge wote wa CCM. Serikali ya CCM chini ya Rais Mwinyi ikakubali kuwa muundo wa muungano ni hovyo, ikaridhia iundwe Serikali ya Tanganyika. Nyerere ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM, mtu mmoja tu, akakataa.
Tume ya Jaji Nyalali ilitamka kuwa muundo wa Muungano ni hovyo.
Lisu leo anachokitamka siyo kipya, bali anakazia kinachojulikana na kukubaliwa na wote wenye akili timamu na walio wakweli.
Kwa sasa hakuna mtu hata mmoja mwenye akili timamu anayeweza kusimama hadharani kuwa muundo wa Mungano wetu upo vizuri.
Wananchi tusimame na hawa wenye akili na walio wakweli.
Mimi naamini, kwenye hili, hata Rais Samia, japo hajatoa kauli yoyote hadharani, ataungana na wenye akili kukiri kuwa muundo wa Muungano siyo sawa, unahitaji marekebisho makubwa. Labda anachokosa ni ujasiri wa kunena, hasa kwenye hatua ya sasa.
Nina hakika siku ambayo Samia atasema kuwa, Muungano wetu unahitaji marekebisho, machawa wajinga wote, mtawaona namna watakavyomshangilia na kumsifu.