Mwanamageuko
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 8,596
- 5,584
Mwisho wa ccm ni 2015,liwalo na liwe
Tajeni na chama m'badala (pamoja na sifa zake) cha kukiweka madarakani baada ya kuitoa CCM.
We ukombozi wa fikira, unalopoka sana. Sijui unaumwa mkendu?
Tajeni na chama m'badala (pamoja na sifa zake) cha kukiweka madarakani baada ya kuitoa CCM.
Nilitaraji ungetaja na sifa zake ambazo ni tofauti na za CCM.Chadema
Nilitaraji ungetaja na sifa zake ambazo ni tofauti na za CCM.
MAKADA WATANO CHADEMA KORTINI *Ni watuhumiwa wa tindikali Igunga 2011 *Waachiwa na kukamatwa, wapelekwa Tabora MAKADA watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Igunga, wakituhumiwa kummwagia tindikali Musa Tesha mwaka 2002. Watuhumiwa hao, walifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora jana, ambapo upande wa mashitaka uliondoa shitaka lililokuwa likiwakabili mahakamani hapo, hivyo kuachiwa huru lakini walikamatwa tena hapo hapo na kurudishwa korokoroni. Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Ajali Milanzi, mwendesha mashitaka wa polisi, Cosmas Mboya aliondoa shitaka lililokuwa likiwakabili watuhumiwa hao kwa kutumia kifungu cha 98 (A) cha Sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 1985, kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kuhusu mwendesha mashitaka kufanya hivyo. Baada ya kuondoa shitaka hilo, Hakimu Milanzi alikubaliana na upande wa mashitaka na kusema kuwa, washitakiwa wako huru. Baada ya kufutiwa shitaka hilo, watuhumiwa walianza kutoka nje ya mahakama lakini ghafla walizingirwa na askari zaidi ya 40 waliokuwa wamesheheni silaha aina ya mabomu, bunduki na pingu ambao waliwakamata tena. Walifungwa pingu, kisha wakapakiwa ndani ya magari mawili ya polisi ambayo yaliondoka eneo la mahakama kwa kasi huku yakiwaacha wananchi waliokuwa wamefurika mahakamani hapo katika mshangao. Mkuu wa Polisi Wilaya ya Igunga (OCD), Abeid Maige aliwaambia waandishi wa habari kuwa watuhumiwa wamepelekwa Tabora kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka mengine mapya. Hata hivyo hakuyataja. Washitakiwa hao ni Evodius Justian (30) mkazi wa Bukoba, Osca Kaijage (36) mkazi wa Ndala mkoani Shinyanga, Rajabu Daniel (24) mkazi wa Singida na Seif Magesa (37) mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza. Wote walifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Igunga Aprili 12 mwaka huu, kwa kosa la kummwagia tindikali Mussa Tesha (26) mkazi wa Igunga Mjini, wakati wa kampeni za Uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba mwaka 2011. CHANZO: MtanzaniaChadema
Thubutu yakoMwisho wa ccm ni 2015,liwalo na liwe