Kama startimes ni digital "WASHENI ANALOG HARAKA"

Kama startimes ni digital "WASHENI ANALOG HARAKA"

DOMA

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2011
Posts
944
Reaction score
367
King'amuzi hiki kimekua kero afadhari hata ningekuwa nje ya mji sasa katikati kila wakati ni no service mara picha zigande kwa kweli kama ndio digital hii nawataka analog iwashe haraka sio kila siku ni kuchezeana tu.
 
wana king'muzi cha kukodi unaweza kufanya hivyo ili kikizingua unawarudishia
 
King'amuzi hiki kimekua kero afadhari hata ningekuwa nje ya mji sasa katikati kila wakati ni no service mara picha zigande kwa kweli kama ndio digital hii nawataka analog iwashe haraka sio kila siku ni kuchezeana tu.

hao ndio wa china mimi nilikua nacho nikakiuza nimenunua ting aal.002.mambo burudani hamna no sevisi wala no sgnal.tena narekodi vipindi ninavyo vipenda.tatizo watanzania tunapenda vitu vya bei raisi na wachina wameshatujua.vipindi vyenyewe niki china china tuhamna lolote yani ni bora serikali ingeviunga mkono ting na basectrancemission.kama zanzibar.walivyo ingia ubia na ting.lakini siunajua serikali yetu.inavyo wadharau wazawa na kuwatukuza wageni.sasa hangalia wazawa wanatoa kitu kwaliti.haibu kwa serikali na tcra.
 
Kwa mlionunua king'amuzi cha Startimes mmeliwa mazima.

Sijawahi kuona quality mbaya ya picha kama ya ving'amuzi vya Startimes
 
Mimi kinanikera na kimenichosha sana,chanel ninazoona clear ni tbc na chanel ten tu,zingne ni scratch mwanzo mwisho.
 
mwingine ni ushabiki tu, mimi napata picha na sauti pretty clear......hamna mgando wala fresh! tatizo ni sehemu ulipo na antena yako tu. mwanzoni nilikuwa natamani kutupa hiki king'amuzi lakini niliporefusha antena yangu, mambo shwari sana
 
CTO,hebu tupe faida yake na initial installation cost.na je ina monthly charge?nimesikia wengi wakiisifia
 
kuna kitu nataka niulize sijakifanyia kazi lakini nataka nijue.
Kuna rafiki yangu ana simu ya nokia n72 ina TV out uwa anaingia youtube anastream video then anaiunga kwenye tv anakuwa naangalia zile video kupitia tv.
Voda na dstv wana ile huduma yao ya kulipia 2500 kwa week ukawa waangalia channels zao za dstv kupitia simu.
Sasa hivi kama una simu usiyotumia kwa mawasiliano yenye TV out si unaweza tumia hii kuangalia dstv channels kwa hiyo bei cheap
 
mwingine ni ushabiki tu, mimi napata picha na sauti pretty clear......hamna mgando wala fresh! tatizo ni sehemu ulipo na antena yako tu. mwanzoni nilikuwa natamani kutupa hiki king'amuzi lakini niliporefusha antena yangu, mambo shwari sana
Unafikiri channel zote za nchini zinapatikana kwenye mfumo huu?
Yaani mambo ya ichi hii ni kukurupuka tu utadhani mtu aliyezinduka kwenye kifafa...
 
CTO,hebu tupe faida yake na initial installation cost.na je ina monthly charge?nimesikia wengi wakiisifia
Ukiwa na Satellite Dish/Decoder set unapata local channels zilizo katika satellite (ITV, TBC1, Capital TV, Startv, et al) na channel nyingi za bure. Gharama ni decoder/dish (kama laki mbili kasoro chache and may be less) kama pia utamwita fundi akufungie (kuna fundi anafanya kwa less than 20 000Tsh). Baada ya hapo hutagombana na Startimes tena! :smile:
 
  • Thanks
Reactions: Paw
thanks a lot mkuu.Maana huu mfumo tusipojiangalia tutakuwa na ving'amuzi vyote nyumbani kwetu.
 
King'amuzi hiki kimekua kero afadhari hata ningekuwa nje ya mji sasa katikati kila wakati ni no service mara picha zigande kwa kweli kama ndio digital hii nawataka analog iwashe haraka sio kila siku ni kuchezeana tu.

Fungua mlango wa kuingizia kadi bila ya kuzima king'amuzi chako. Chomoa kadi kisha ingiza tena, utaona mawimbi na kukamaa kwa picha kwa muda, baada ya dakika tatu tatizo la kukamaa kwa picha litakuwa limekwisha. Leo ni siku ya nne sijapata tazizo la kukatika katika kwa sauti na picha kukamaa.
 
Back
Top Bottom