Kama sio chuki zako Kikwete na Lowassa tungempata wapi?

Kama sio chuki zako Kikwete na Lowassa tungempata wapi?

Yericko Nyerere

Platinum Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,027
Reaction score
20,519
Mwanafalsafa mmoja wa kiyunani alisema jambo moja linaloishi mpaka leo, kwamba hakuna upuuzi ulio upuuzi mtupu, pia kauli ilikuja kuchagizwa na kauli ya mfalisayo wa Ukaridayo aliyesema alama za nyakati zikifika mwamuzi ni Muumba tu,

Nafasi ya Urais sio nafasi ya kupata "kama zali". Hata uwe kiongozi mzuri kiasi gani huwezi kushtukizwa na kupewa mikoba ya nchi kirahisi rahisi tu. Lazima uwe umejipanga, umejiandaa na uko tayari. Hotuba za Magufuli zinadhihirisha kuwa aliingia kwenye kinyang'anyiro kwa kujaribu.

Membe alitangaza nia Lindi, Makamba alitangaza nia Mlimani City, Muhongo- Musoma, Mh.Lowassa;Arusha n.k. Magufuli alitangaza nia wapi? Alitaja vipaumbele gani? Nini kauli mbiu yake? HAKUNA. Huwezi kumpa mtu 'miaka 5 ya kujiandaa' kuongoza nchi. Tunataka mtu aliyejiandaa an akiingia ikulu aanze kuongozanchi mara moja. Mtu huyu ni Edward Lowassa.

Kuna tofauti kubwa kati ya Magufuli na Lowassa. Wote ni wepesi katika kufanya maamuzi. Lakini mmoja hufanya maamuzi yenye tija wakati mwingine hufanya maamuzi yenye madhara. Tuangalie mifano:

Mh.Magufuli 'alipiga' bei nyumba za serikali na leo hii serikali inatumia mamilioni kuwapangishia hotelini watumishi wake.HASARA! Mh.Lowassa amesimamia ujenzi wa UDOM na kuongeza idadi ya wataalam mbalimbali nchini.FAIDA.

Ndg.Makufuli amenunua vivuko, pantoni na mashine za tiketi kwa mabilioni lakini hazifanyi kazi/ hazina ufanisi.HASARA. Mh.Lowassa alisimamia ujenzi wa bomba la maji kutoka ziwa Victoria mpaka Shinyanga huku akipuuzia vitisho vya Wasudani na Wamisri vya kuhodhi matumizi ya maji ya Victoria kwa mkataba wa kikoloni.FAIDA.

Mh.Magufuli alibomoa fuel station "shell" huko Mwanza, serikali ikashindwa kesi, tukalipa mabilioni.HASARA. Mh.Lowassa alivunja mkataba wa City Water, hatukushtakiwa.FAIDA.

Mh.Magufuli alikamata wavuvi "halali" wa Asia ya mbali tumeshitakiwa, tumedondokea pua, tutawalipa meli yao na gharama nyingine kadhaa zenye thamani ya 16bilioni hapo hujajumlisha gharama za utunzaji wa wale samaki.HASARA. Mh.Lowassa, wakati ndege za Malawi zishaanza kuzurura maeneo ya Kyera na Nyasa huku tukiwachekea, alitoa tamko Bungeni...."tuko imara, tumejipanga...". Wakafunga Virago.FAIDA.

Ndg.Magufuli amewanyang'anya kandarasi wajenzi kadhaa kwa matamko tu bila kuzingatia taratibu za mikataba. Wametushtaki, wameshinda, tumewalipa.HASARA. Mh.Lowassa alitaka kuvunja mkataba wa Richmond, kama sio AG Johnson Mwanyika kuomba..."mapumziko ya saa moja nje ya mkutano" ili awasiliane na mamlaka ya juu na baadae kurejea na agizo kuwa..."imeagizwa; mkataba usivunjwe.." pengine leo tusingekuwa tunazungumzia Richmond, baba yake na Dowans, babu wa Symbion Powers. TUNGENUFAIKA.

UCCM wangu hauwezi kunipofua nisiuone ukweli huo hapo juu. Ujirani wangu na Mh.Magufuli hapa Chato hauwezi kunishinikiza nimuazime miaka 5 ya kujiandaa badala ya kutawala.

NITAMPIGIA KURA LOWASSA.
 
Kweli kabisa makofuli adi muda huu anaona kama ndoto hajiamini kabisa anaweza atakujitowa kwenye mbio kwakuogopa mafuriko ya lowassa!!!
 
Asante kwa uchambuzi muruwa.Watanzania wenzangu tutunze vema kadi zetu za kupigia kura.Tufanye mabadiliko mwaka huu.
 
ubarikiwe sana na uwe hai mpaka upige kura yako. AMEN
 
kwa sasa lowasa ni mwanasiasa anayeongelewa sana kila la heri
 
Yericko Nyerere

Watu kwa kupenda kupotosha ngoja nbasi nikusaidie kama haufahamu! Kuhusu uuzwaji wa nyumba wala haukuwa Uamuzi wa Magufuli wala Mkapa bali hili pendekezo lilitoka Benki ya Dunia na IMF ambao ndiyo wafadhili wakubwa wa nchi masikini, wao ndiyo waliiambia Serikali yetu ni lazima iuze nyumba ili kubana Matumizi (austerity) kwamba hizi nyumba zilikuwa na gharama kubwa sana kwa Serikali na siyo TZ tu ndio waliuza nyumba hata Kenya pia nyumba za Serikali nyingi ziliuzwa na sababu ni hiyo hiyo IMF hivyo kwa Magufuli ni kwamba alitokea tu kuwa Waziri muhusika wakati huo lkn kitendo kilikuwa ni lazima kifanyike maadamu TanZania ilikuwa inashirikiana na IMF na Benki ya Dunia hata Jefrey Sachs aliliongelea hili kwenye moja ya vitabu vyake, ni kama vile masharti mengine mengi yaliyowekwa na IMF ambayo hat fisado Lowasa mwenyewe aliyatekeleza... Hivyo acha kupotosha!
 
Last edited by a moderator:
On a serious NOTE, hivi wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea ndani ya CCM, slogan/kauli mbiu ya Magufuli ilikuwa nini? Nakumbuka Lowassa ailikuwa maamuzi magumu, Safari ya matuimani na mchakamchaka wa maendeleo.

Je, slogan/kauli mbiu ya Magufuli ilikuwa nini? ili kujitofautisha na watia nia wengine?!

Maana watia nia wote wa CCM tulifahamu mwisho wa siku atakayechaguliwa lazima anadi ILANI YA CCM.

Ili kujitofautisha na wana-CCM wengine basi kila mtia nia alikuwa na kauli mbiu yake. Je, kauli mbiu ya Magufuli ilikuwa nini?

Kama kweli Magufuli alikuwa hana kauli mbiu na kusubiri ILANI YA CCM, imtengenezee kauli mbiu, basi inawezekana kweli Magufuli alikuwa hakujiandaa kuwa Urais wa JMT. Magufuli ameokota pochi kwenye maandamano ya UKAWA.
 
Unaejiita Yericko Nyerere, toka babu dakatari wa kanoni padri Dr.W.Slaa akupe za uso leo ndiyo unarudi na ufataani mwingine!

Kwi kwi kwi teh teh teh
 
Last edited by a moderator:
Watu kwa kupenda kupotosha ngoja nbasi nikusaidie kama haufahamu! Kuhusu uuzwaji wa nyumba wala haukuwa Uamuzi wa Magufuli wala Mkapa bali hili pendekezo lilitoka Benki ya Dunia na IMF ambao ndiyo wafadhili wakubwa wa nchi masikini, wao ndiyo waliiambia Serikali yetu ni lazima iuze nyumba ili kubana Matumizi (austerity) kwamba hizi nyumba zilikuwa na gharama kubwa sana kwa Serikali na siyo TZ tu ndio waliuza nyumba hata Kenya pia nyumba za Serikali nyingi ziliuzwa na sababu ni hiyo hiyo IMF hivyo kwa Magufuli ni kwamba alitokea tu kuwa Waziri muhusika wakati huo lkn kitendo kilikuwa ni lazima kifanyike maadamu TanZania ilikuwa inashirikiana na IMF na Benki ya Dunia hata Jefrey Sachs aliliongelea hili kwenye moja ya vitabu vyake, ni kama vile masharti mengine mengi yaliyowekwa na IMF ambayo hat fisado Lowasa mwenyewe aliyatekeleza... Hivyo acha kupotosha!

Kwahiyo World Bank na IMF ndio waliomwambia Magufuli amuuzie hawara yake na mdogo wake nyumba za serikali, wakati hawakuwa waajiriwa wa serikali?!

Akili zako hazina tofauti na Zinjathropus. You need to be performed a head transplant.
 
Hilo silijui! Ila ninachokijua ni kwamba nyumba ilikuwa ni lazima ziuzwe kulingana na maagizo ktk Benki ya Dunia na IMF!

Wadau, mimi binafsi nashangazwa na Lowasa, kila kukicha umaarufu wake unaongezeka. Lowasa namfananisha na gogo la Udi, yaani kila ukilikata linazidi kutoa Marashi ya kuvutia, na Lowasa kila akichafuliwa anazidi kuwa maarufu. Imetumika gharama kubwa kumchafua Lowasa lakini naona umaarufu wake unazidi, kila kona ya nchi sasa ni Lowasa. Sijui kama imewahi kutokea duniani mtu akachafuliwa hivi lakini akazidi kuwa maarufu kiasi hiki. Nadhani huyu jamaa ana nyota isiyo na kifani
 
Watu kwa kupenda kupotosha ngoja nbasi nikusaidie kama haufahamu! Kuhusu uuzwaji wa nyumba wala haukuwa Uamuzi wa Magufuli wala Mkapa bali hili pendekezo lilitoka Benki ya Dunia na IMF ambao ndiyo wafadhili wakubwa wa nchi masikini, wao ndiyo waliiambia Serikali yetu ni lazima iuze nyumba ili kubana Matumizi (austerity) kwamba hizi nyumba zilikuwa na gharama kubwa sana kwa Serikali na siyo TZ tu ndio waliuza nyumba hata Kenya pia nyumba za Serikali nyingi ziliuzwa na sababu ni hiyo hiyo IMF hivyo kwa Magufuli ni kwamba alitokea tu kuwa Waziri muhusika wakati huo lkn kitendo kilikuwa ni lazima kifanyike maadamu TanZania ilikuwa inashirikiana na IMF na Benki ya Dunia hata Jefrey Sachs aliliongelea hili kwenye moja ya vitabu vyake, ni kama vile masharti mengine mengi yaliyowekwa na IMF ambayo hat fisado Lowasa mwenyewe aliyatekeleza... Hivyo acha kupotosha!

Kura yangu ni kwa Lowassa tu. Magufuli hata ungempamba vipi hapambiki. Chema chajiuza kibaya............ Mtembezeni sana Magufuli ila jueni kura zinakwenda kwa Lowasa
 
Back
Top Bottom