Kama simu yako imepasuka kioo, imejaa wino, n.k. fanya hivi kunyonya vitu vyako uvitunze ama uhamishie simu mpya

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Iliwahi nitokea hii, simu nilinunua laki 4 ikapasuka kabisa kioo, kuulizia bei ya kioo laki 2 na elf 80, nikasema potelea mbali heri ninunue simu mpya tu, lakini kulikuwa na vitu vya muhimu ndani ya simu na inahitaji nivihamishe.

1702318304988.png

Simu imedondoka kwenye sakafu kioo chote kimejaa wino ama kimezima lakini simu inaita, mesej zinaingia, n.k. unaenda kwa mafundi kama watatu unakuta kioo ni gharama kubwa.

Katika hali kama hio ni heri uachane na hio simu maana waweza weka kioo ukakuta kumbe na kamera imezingua, ni heri ununue simu mpya tu.

Cha kufanya ili uchukue mafaili yako kwenye simu ya zamani inabidi utumie kifaa kinaitwa “USB C DOCK” (hii ni kwa simu zenye tundu la usb c)

1702317685030.png
Hiki ni kifaa unachomeka kwenye rundu la simu unaconnect inaonekana kwenye tv kwa waya wa hdmi tunaotumia hata kwenye vingamyuzi, utachomeka keyboard na mouse ili kuitumia simu na ukachomeka flashi kuhamishia mafaili yako.

Kifaa hiki ni kama laki hivi lakini waweza kuongea na wauzaji uwape hata elf 5 au 10 ukitumie mara moja kuhamishia vitu vyako kisha unaenda kuvihamishia kwenye simu mpya.

Picha na videos unazihamishia kwa kuzinyonya folder la dcim

Meseji na call logs tumia app kama sms and call backup

Whatsapp unaibackup kisha utahamisha folder.
Telegram nayo unahamisha folder
 
Ni kifaa kizuri sana. Nikikumbuka simu yangu iliharibika ikiwa na kumbukumbu zangu fulani mpaka leo naiwaza. Nitakikitafuta
 
Back
Top Bottom