Kama Simba "Called King For A Reason".

Meizon

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
279
105
Habari wakuu, kwa Mara nyingine tena nawasilisha kwako mada niliyo iandaa ili kukufanya uwe bora zaidi. Huu bado ni mwanzo wa mwaka 2017 na ni imani yangu umejipanga kuboresha maisha yako huku Mungu akiwa tegemeo lako.

Katika pita pita zangu nilikutana na kipindi kwenye runinga juu ya mfalme wa mwitu, yaani SIMBA! Nilijifunza mengi kumuhusu mnyama huyu na wengine pia lakini kama muandishi ilinibidi kujaribu kugeuza kile nilicho jifunza na kukiweka katika mtazamo wa kibinadamu zaidi.

1014553aec31ea809db81dd72879ddc6.jpg


Katika sifa nzuri nyingi nilizo ziona, zifuatazo ni sifa mbili za simba ambazo ukizijua unawezajifunza mambo mengi makubwa;

1.SIMBA ANAJITAMBUA YEYE NI MFALME: Hakika nimeliona hili na nikastaajabu mno. Ni pale nilipomuona simba dume akienda kunywa maji mtoni ghafla mamba akajaribu kumuwinda! Ni wazi kwamba mamba anauwezo mkubwa wa kumuuwa simba endapo angemvuta kwenye maji lakini simba huyu hakukimbia pale mamba alipo panua mdomo wake kujaribu kumdaka baadala yake alikwepa kisha akaanza kuunguruma kitemi!! (hapa ilinibidi nitabasamu kwa raha kwani nilikwisha ona mamba akiwaonea swala, nyati, nyumbu na pundamilia! Hivyo nilikuwa na shauku kuona je,kwa simba inakuwaje?)....haikuchukuwa muda mamba akajirudisha kwenye maji taratiibu na kumuacha simba Yule akinywa maji kwa raha zake.

Rafiki; kujitambua ni nguzo ya ubora wako, kuna mambo huwa yanaonekana magumu kwetu kwasababu hatujajitambua sisi ni kina nani.
Haitoshi kuitwa flani, unatakiwa kujijua wewe ni flani! (Note that no one should tell you who you are, you define yourself)

2.SIMBA JIKE HUMPIMA DUME KABLA HAJAKUBALI AMPANDIE: Hili litawalenga wanawake hasa japo hata mwanaume unaweza jifunza. Ili simba jike akubali kupandiwa na dume basi hupitisha takribani wiki 2 akilichunguza dume hili kama je, lina NGUVU? LINAJUA KUJILINDA? na LINAUWEZO WA KUMLINDA?
Kipindi hiki jike huwa mkali sana pale dume likijaribu kumpanda (MFALME WA MWITU HABEBI MIMBA KIJINGAJINGA).
Sababu ni kwamba dume mmoja hutawala eneo kubwa la pori pamoja na majike zaidi ya 6. Simba dume huweka alama kwenye mipaka ya imaya yake kwa kutumia mikojo, dume mwingine haruhusiwi kuingia katika eneo hilo vinginevyo anataka kupindua ufalme wake kwa kupigana na kumfukuza. Endapo dume mwenye imaya atapigwa na kunusurika kuuawa basi huondolewa na huenda kutafuta falme nyingine (NA NI KWA KIPINDI HIKI TU SIMBA DUME HUWINDA KAMA JIKE SABABU HANA MAJIKE ANAYO YATAWALA).
Dume jipya huakikisha limeondoa mbegu ya dume lililolipigwa kwa kuuwa vitoto vyote vitakavyo kuwepo hapo (ndio watu husema simba dume hula vitoto vyake). Hii ndiyo sababu majike huwa makini kuchaguwa dume la kuwapanda kwani huumizwa pale vitoto vyao vinapo uawa na dume geni.

Rafiki; kila uamuzi unaouchukuwa Leo unaathari kubwa baadaye, hivyo ni muhimu kuwa makini. (Dakika 10 za sex tamu hupelekea miezi 9 ya kulea mimba na miaka 20 ya child support endapo hukujipanga! Tuwe makini!)

Usifanye jambo kwa sababu unaweza Bali lifanye kwa sababu unataka kulifanya!.

Do not do it just because you can, but do it because you want to!


Vijana wengi Leo hii tunaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi kwasababu tu tunaweza kufanya hivyo lakini sio kwasababu tunataka. Kumbuka huwezi kukitaka kitu ambacho hujakijua wala kukichunguza vinginevyo uwe mpuuzi!

Leo nitakomea hapo na muda mwingine nitakuja na sifa nyingine za simba ambazo zinamafunzo kwetu japo ni binadamu sio wanyama. Ahsante!
(www.ardhinyeusi.wordpress.com)
Instagram, facebook and twitter username ----> Ardhinyeusi.
 
Back
Top Bottom