Kama si mzee Aboud Jumbe kusingekuwapo na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama si mzee Aboud Jumbe kusingekuwapo na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Babylon, Apr 22, 2009.

 1. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mzee Aboud jumbe kama binadamu mwingine ana upungufu wake lakini chakushangaza leo serekali mbili hizi hawataki hata kuyazungumzia yae mazuri aliyowafanyia pande mbili hizi za Mungano.

  Kama asingelikubali kunganisha chama cha ASP ule mwaka 1977 kusengekuwapo na CCM, leo ukiwauliza wanafunzi hawamjuwi Mzee aboud jumbe ni nani wao wanambiwa tu muanzishi wa CCM ni mwalimu Nyerere, lakini ikumbukwe historia ipo siku itabainisha hili na mengine.

  Nakumbuka kama leo siku ile ya kunganishwa ASP na TANU mzee wetu shekh Thabit Bin kombo mtumzima alitokwa na machozi machozi yale yalikuwa na maana yake. Leo imefika pahala hawa watu hawataki hata kuyaeleza au kulitaja jina la mzee Aboud lakini tusijisahau kuwa hakuna aliyejiumba, hapa wanamsubiria ili waje watueleze ambayo wanataka wao tuyasikie.

  Mungu ampe afya nzuri mzee wetu baadhi yetu hatuto msahau kwa mazuri aliyotuletea na tupo tayari kumsamehe kwa makosa aliyofanya ambayo leo hii yanatukosesha usingizi.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  BABYLON,
  Hata huko Zimbabwe kuna watu wanasema kama sio Mugabe, Zimbabwe wasingekuwa Huru leo.....sidhani kama maneno haya yana ukweli, na hata kama upo haufuti machafu ya mtu huyu...Waswahili wanasema Mzazi (baba) sio kutunga mimba kwani kila mwanamme rijali anaweza, baba ni yule anayeweza kulea vizuri hadi mtoto akakua!
   
 3. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi juu ya jitihada zake julias kuweka lugha ya kiswahili iwe ndio ya taifa bado baadhi yetu inatupa tabu ?mimi sijazungumzia zimbabwe hapa .Vereje leo hii kiumbe huyu analeta ya zimbabwe, matatizo ya zimbabwe ni yao wenyewe. mimi nazungumzia yaliyo yetu kila mtu hulia mama yangu na halii mama yetu
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  the fallen hero
   
 5. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  PENGINE MWENYEWE ANASHUKURU KUSAHAULIWA KWA BLUNDER HIYO. Huyu Mzee ameamuwa kumrudia Mungu kwa madhambi yake hili Likiwa kubwa.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hivi ni kweli Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi alitaka kuvunja muungano?

  Nini kilikuwa kiini cha "machafuko ya hali ya hewa" Zanzibar yaliyopelekea kujiuzulu kwake?

  Seif Sharif Hamad alimchongea nini kwa Nyerere wakati akiwa waziri kiongozi?

  Hamad aliteta nini na Nyerere Butiama baada ya kutoka CCM?
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Good questions!
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kama kuna binaadamu m-binafsi hapa Tanzania aliyewahi kuishi basi Nyerere anaongoza, si kuwa aliifuta historia ya mashujaa wengine waliotoa mali zao na roho zao kwa nchi hii bali aliwafanya wakaonekana maadui wa nchi hii, na kujigeuza yeye kwa kila sifa inayomstahiki na isiyomstahiki,mbali na Jumbe watu kama Bibi Titi Moh'd, Oscar Kambona,Kasela Bantu n.k waliomtengeneza na Kumpromote Nyerere enzi hizo, walifikia hata kutoa fedha na mali zao kumpeleka Nyerere U.N akawasemee kwa kuwa tu alijua kingereza, wengine walimbeba hata pale alipotaka kupinduliwa (Oscar kambona), shukurani za mtu huyu kwa watu wote hao ni kama za punda, aliwapiga mateke na kuwanyanyasa kama vile hakuwahi kuwajua seuza kupata hisani zao,Manyanyaso aliyomfanyia BB TT, kwa kisingizio cha kutaka kumpindua, yanasikitisha hata leo ukiyasoma tu, lau kama kungekuwa na vyombo vya habari siku hizo kama ilivyo sasa vikapaza sauti zao kwa madhila waliyofanyiwa "mashujaa waliosahaulika" nchi hii na "kufutwa" historia na michango yao ya ujenzi wa taifa hili na Mwalimu Nyerere kwa makusudi, hakuna mtu angelitoa chozi lake kwa kifo chake.
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Mzee Jumbe alihujumiwa akapigwa mkwara ...akakuabali kuachia ngazi....tena bila hata shari na amejipumzikia anakula pepo zake taratibu huko kigamboni ila ameshaulika kabisa katika historia....sidhani hata kama huwa anapata mialiko...yote kama mstaafu
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Junius,
  Hivi si kweli kuwa Bibi Titi alishiriki katika mipango ya kumpindua Nyerere? Pamoja na Kambona? Ubinafsi unaousema ni upi? Wa kumsamehe Bibi Titi asiwekwe kitanzi? Aliyetoa fedha zake kumpeleka Nyerere UN alikuwa Mzee Rupia. Kambona naye alibebwa tu na TANU. Aliifutaje historia ya mashujaa? Ni wapi Nyerere ameandika historia ya juhudi za ukombozi? Acheni kupindisha ukweli wakati tunaoujua ukweli bado tupo hai.
   
 11. S

  Sahiba JF-Expert Member

  #11
  Apr 22, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni hatari aibu na fedheha kwa jamii ya mtanzania inayoendelea kumtukuza na kumsifu mtu aliyejenga foundation iliyoendelea kuisulubu nchi hadi hii leo.Ccm wakati ule ilijengwa kwa misingi ya udikteta,ugaidi,umafia na upelelezi wa ndani kwa ndani kwa kila mwanadamu mwenye mawazo tofauti na ya mzee basi cha moto atakiona.Hii inasababisha kuitilia mashaka CUF ambayo siasa zake zinamzunguka Seif Sharif kiasi cha kulingana na siasa za Nyerere.Sio siri kwamba viongozi wa juu wote wa Cuf wanamuogopa Seif na hii itaendelea ikiwa Seif atakamata urais wa Zanzibar na matokeo yake atageuka kuwa Sultan.

  SAHIBA.
   
 12. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #12
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni kweli hii nchi haina mambo ya huyu alikuwa mtu muhimu no watu wanaangalia huyu mtu anaweza kutusaidiaje kwenye mambo yetu. Mfano Mzee Kawawa unadhani hizi sifa anazopewa sasa zinatoka moyoni? Akha wapi mbona huko nyuma walikuwa kimya?

  Nchi hii ina watu wengi wameifanyia mazuri lakini hawajulikani. Lazima mtu historia yake ijulikane iwe nzuri au mbaya kwani Hitler historia yake inavyoimbwa unafikili ni kwanini? Ili wengine nao wajifunze kuwa siyo ubinadamu kufanya vile.

  Hivyo ingekuwa vizuri hawa watu tuwajue na waandikwe kwenye historia ya nchi. Kwani mtoto wako nyumbani akidokoa anakosa kuwa mtoto wako? Atabaki kuwa mtoto wako.
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa wote wana-JF waliochangia mada hii hadi sasa, mnasahau kwamba wakati Jumbe (pamoja na wengine) alipokuwa anajibidiisha kuiasisi CCM, hakujua kwamba yangemkuta yaliyomkuta. Ne mengineyo mengi yanayowakuta Wazanzibari hadfi kufikia majuto kwa wengi wao.

  Kwa Wazanzibari, kuanzishwa kwa CCM kulikuwa 'ironical' -- kwani ilikuwa ni mwanzo wa mwisho wa 'sauti' huru ya Wazanzibari, kwani baada ya hapo masuala yote kuhusu mustakabali wa visiwa hivyo yalikuwa yanaamuliwa Dodoma. Hata masuala ya kuchagua viongozi wao.

  Matokeo yake ni kwamba CCM imeziduwaza na kuzidumaza fikra za Viongozi wa Zanzibari kiasi kwamba misimamo yao mingine inasikitisha kweli kweli.

  Nitatoa mfano. Ktk uchaguzi wa 2005, pamoja na kwamba ilionekana kuwa ni zamu ya Visiwani (ingawa haiko ki-Katiba) kutoa rais, na kwamba walikuwa na candidate ambaye alikuwa very strong, viongozi wa huko, kwa sababu zisizokuwa na msingi kabisa, waliamua kuwa potelea mbali, na kuonekana kuwaambia watu wa bara: "endeleeni tu nyinyi kutoa Rais tena! Sisi hapana."

  Halafu hapo hapo wanapiga kelele ya kutaka usawa baina ya pande mbili za muungano!
   
 14. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #14
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  JASUSI.
  Hivi si kweli kuwa Mwalimu alipanga Propaganda hizi, kwasababu "mbovumbovu" na akazigandamiza katika vichwa vya "wanafunzi" wake kama nyinyi ambao,alikuimbisheni unafiki,mkaitikia ndo ukweli,alikusomesheni batili mkasema haki,alipanga hila na madhila kwa wote waliotaofautiana nae,kama Kambona alitaka kumpindua kwanini asitumie fursa ile ya maasi ya kijeshi1960s ambao walikuwa wakimsikiliza yeye tu wakati ule, aje asubiri badae? BB TT kukataa "ujamaa,azimio la Arusha na kudhulumiwa watu mali zao" ndo alistahili kitanzi? basi ni afadhali angempiga kitanzi kuliko kumpeleka kule kiinua miguu zanzibar,na kuvuliwa nguo na watoto wadogo wa kuwazaa kama si kuwajukuu,ama kweli ww "umekhitimu" mafunzo ya "Mwalimu" wako? na kweli unadumisha "fikra" zake. Usitake kukataa kama fedha za safari ya U.N zilichangwa sikusema Mzee Rupia hakutoa, pengine yeye alitoa nyingi hasa, lakini juhudi hizo zilifanyika kwa pamoja, na walimuwezesha kufanikisha kawarudi kinyume.
   
 15. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #15
  Apr 22, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Propaganda zipi unazozizungumzia rafiki yangu? Sijakuelewa.
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Apr 22, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  eti kuwa BIBI TITI na WENZAKE WALIPANGA KUMPINDUA,MAANA WAKATI ANASHIKILIWA KULE KIINUA MIGUUU, ALILAZIMISHWA AWATAJE WATU JUST FOR "IMPLICATION" KWA MAAGIZO YA MWALIMU, WATU "WALIOMSHUGHULIKIA" BADO WANGALI HAI HAPA NA TUNAO, HAWAFICHI KITU WANASEMA WAZI WAZI....
   
 17. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi ni vitu vinahitaji kuwekwa wazi wakati huu-kwa manufaa ya historia ya nchi yetu na vizazi vyetu vijavyo. Hivi nini kilijiri. Msituambiue tu -Kuchafuka kwa hali ya hewa ya Kisiasa. Hii ni khushi- haijitoshelezi.
   
 18. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Usicheze na Mwalimu wewe. Ni mweledi. Na mjanja. na Mlaghai. Anachokitakam kiwe huanza kukipinga na kuwazubaisheni kumbe huku anakifiringa. Acha tu wewe na hadithi yake- Zanzibar haiwezi kumezwa. Amefanya nini?
   
 19. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nawaheshimu sana wazee wetu waliopo na waliondoka. Mzee Thabit Kombo ana kosa la kuichukua Shirazi Association kuiunganisha na African Association kuunda ASP. Mzee Aboud Jumbe ana makosa zaidi ya kuichukua ASP kuiunganisha na Tanu kuunda CCM. (Naomba radhi kama nimewakwaza wanasiasa)- Naongelea kwa mintarafu ya historia tu.
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Yapo mengi kuhusu historia ya nchi yetu hayajaandikwa popote.Ni wakati muafaka sasa wa kuanza kuyaandika ili hata sisi tusiokuwapo miaka hiyo tuweze kuyasoma na kujielimisha nayo.
   
Loading...