Hivi ni kweli Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi alitaka kuvunja muungano?
Nini kilikuwa kiini cha "machafuko ya hali ya hewa" Zanzibar yaliyopelekea kujiuzulu kwake?
Seif Sharif Hamad alimchongea nini kwa Nyerere wakati akiwa waziri kiongozi?
Hamad aliteta nini na Nyerere Butiama baada ya kutoka CCM?
Kama kuna binaadamu m-binafsi hapa Tanzania aliyewahi kuishi basi Nyerere anaongoza, si kuwa aliifuta historia ya mashujaa wengine waliotoa mali zao na roho zao kwa nchi hii bali aliwafanya wakaonekana maadui wa nchi hii, na kujigeuza yeye kwa kila sifa inayomstahiki na isiyomstahiki,mbali na Jumbe watu kama Bibi Titi Moh'd, Oscar Kambona,Kasela Bantu n.k waliomtengeneza na Kumpromote Nyerere enzi hizo, walifikia hata kutoa fedha na mali zao kumpeleka Nyerere U.N akawasemee kwa kuwa tu alijua kingereza, wengine walimbeba hata pale alipotaka kupinduliwa (Oscar kambona), shukurani za mtu huyu kwa watu wote hao ni kama za punda, aliwapiga mateke na kuwanyanyasa kama vile hakuwahi kuwajua seuza kupata hisani zao,Manyanyaso aliyomfanyia BB TT, kwa kisingizio cha kutaka kumpindua, yanasikitisha hata leo ukiyasoma tu, lau kama kungekuwa na vyombo vya habari siku hizo kama ilivyo sasa vikapaza sauti zao kwa madhila waliyofanyiwa "mashujaa waliosahaulika" nchi hii na "kufutwa" historia na michango yao ya ujenzi wa taifa hili na Mwalimu Nyerere kwa makusudi, hakuna mtu angelitoa chozi lake kwa kifo chake.
Junius,
Hivi si kweli kuwa Bibi Titi alishiriki katika mipango ya kumpindua Nyerere? Pamoja na Kambona? Ubinafsi unaousema ni upi? Wa kumsamehe Bibi Titi asiwekwe kitanzi? Aliyetoa fedha zake kumpeleka Nyerere UN alikuwa Mzee Rupia. Kambona naye alibebwa tu na TANU. Aliifutaje historia ya mashujaa? Ni wapi Nyerere ameandika historia ya juhudi za ukombozi? Acheni kupindisha ukweli wakati tunaoujua ukweli bado tupo hai.
Kwa wote wana-JF waliochangia mada hii hadi sasa, mnasahau kwamba wakati Jumbe (pamoja na wengine) alipokuwa anajibidiisha kuiasisi CCM, hakujua kwamba yangemkuta yaliyomkuta. Ne mengineyo mengi yanayowakuta Wazanzibari hadfi kufikia majuto kwa wengi wao.
Kwa Wazanzibari, kuanzishwa kwa CCM kulikuwa 'ironical' -- kwani ilikuwa ni mwanzo wa mwisho wa 'sauti' huru ya Wazanzibari, kwani baada ya hapo masuala yote kuhusu mustakabali wa visiwa hivyo yalikuwa yanaamuliwa Dodoma. Hata masuala ya kuchagua viongozi wao.
Matokeo yake ni kwamba CCM imeziduwaza na kuzidumaza fikra za Viongozi wa Zanzibari kiasi kwamba misimamo yao mingine inasikitisha kweli kweli.
Nitatoa mfano. Ktk uchaguzi wa 2005, pamoja na kwamba ilionekana kuwa ni zamu ya Visiwani (ingawa haiko ki-Katiba) kutoa rais, na kwamba walikuwa na candidate ambaye alikuwa very strong, viongozi wa huko, kwa sababu zisizokuwa na msingi kabisa, waliamua kuwa potelea mbali, na kuonekana kuwaambia watu wa bara: "endeleeni tu nyinyi kutoa Rais tena! Sisi hapana."
Halafu hapo hapo wanapiga kelele ya kutaka usawa baina ya pande mbili za muungano!
Hivi ni vitu vinahitaji kuwekwa wazi wakati huu-kwa manufaa ya historia ya nchi yetu na vizazi vyetu vijavyo. Hivi nini kilijiri. Msituambiue tu -Kuchafuka kwa hali ya hewa ya Kisiasa. Hii ni khushi- haijitoshelezi.
Hivi juu ya jitihada zake julias kuweka lugha ya kiswahili iwe ndio ya taifa bado baadhi yetu inatupa tabu ?mimi sijazungumzia zimbabwe hapa .Vereje leo hii kiumbe huyu analeta ya zimbabwe, matatizo ya zimbabwe ni yao wenyewe. mimi nazungumzia yaliyo yetu kila mtu hulia mama yangu na halii mama yetu
BABYLON,
Mkuu wangu unalia na Aboud Jumbe kwani yeye mama yako?..unalia kwa kipi haswa wakati huyu mtu ni wa kuchora yaani hakuwa na nafasi yoyote zaidi ya kuwa replacement ya Marehemu Karume..
Waniita KIUMBE... duh ama kweli umenichoka... sema kabisa Bangubangu maanake ndio zenu nyie kuchovya.. Na utaniita majina yote lakini jua moja nazungumza lugha ya KIUME toka sauti bara sibani sauti wala kuashiria kwa kwa vidole..
Hivyo kuwa msikivu na weka heshima mbele
..
Kwa miaka zaidi ya 12 akiwa rais wa Zazibar na makamu wa rais kaifanyia kitu gani Zanzibar na bara kiasi kwamba leo hii akumbukwe!..Binafsi namkumbuka kuwa serikali yake ndiyo aliyewahukumu KIFO kina Abdulrahman Babu na wenzake 32 kwa tuhuma za kumuua Karume..Kama sii Nyerere Jumbe angewaondoa na wapo waliouawa pindi waliporudi au kurudishwa Zanzibar..
Bila shaka kuunganishwa kwa TANU na ASP ni wazo liliotangulia akiwa rais wa Zanzibar na hata kama angeweza kuwa mtu mwingine yeyote ktk nafasi hiyo bado ASP na TANU zingeungana kwa sababu wazo hili lilitokana na Upinzani wa kisiasa ndani ya Zanzibar kuliko huku bara..Bara hatukuwa na sababu ya kuundwa kwa CCM isipokuwa kwa manufaa ya Zanzibar kwani watu kama Seif Sharrif Hamad pia became member of CCM na hilo baraza la Waporaji. Kwanza hao CCM wametupeleka wapi zaidi ya kuwa masikini zaidi..Upuuzi mtupu.
Mkuu wangu kama kuna HERO Zanzibar basi mimi nasema mjamaa mwenzangu Abdoulrahman Babu ndiye anastahiri kwani bila yeye huo Muungano wa nchi na vyama usingekuwepo..Hawa wote wamedandia Mapinduzi ya haki na yaliyokuwa kwa manufaa ya Wazanzibar..
Soma kidogo historia ya Babu hapa

- Wakuu labda kwanza muweke CV ya Mzee Jumbe, je alikuwa na qualifications za kutosha kuwa waziri katika ofisi ya Rais wa Zanzibar? Na hatimaye kuwa rais wa Zanzibar?
- Kama hakuwa na qualifications za kutosha, ina maana alipewa pewa sasa hawa waliompa walikuwa wanategemea nini in return kutoka kwake? Je ni nani waliomfikisha juu kwa njia za mkato?
- Kama kweli alikua nazo qualifications basi kweli alionewa, ninasema hivi kwa sababu kuna theories nyingi sana kuhusu kufika kwake juu, kwamba alifikishwa huko juu makusudi ili kuhitimisha muungano wa Tanu na ASP.
Ahsanteni.
William.
1. In 1979, Jumbe made history by launching the first democratic institution, the House of Representatives but members were mainly appointed instead of being elected by the people at large.
2. He also opened up his administration for people, who could otherwise have been kept out if the strict revolutionary principles were followed.
3. This move, which he later seemed to regret, was the source of his downfall.
4. He was at odds with, the so called, the committe of fourteen who included most of the people who participated in the revolution. Their influence began to decline and their powers, at times, questioned.
5. In an attempt to remedy the damage he droped most of these new elements in his government and made a radical move of attempting to back down from his support towards one central government for the whole of Tanzania.
6. In 1984, he was forced to resign by the CCM's central committe and Ali Hassan Mwinyi was appointed the new President of Zanzibar.
Mzee Aboud jumbe kama binadamu mwingine ana upungufu wake lakini chakushangaza leo serekali mbili hizi hawataki hata kuyazungumzia yae mazuri aliyowafanyia pande mbili hizi za Mungano .kama asingelikubali kunganisha chama cha ASP ule mwaka 1977 kusengekuwapo na CCM, leo ukiwauliza wanafunzi hawamjuwi Mzee aboud jumbe ni nani wao wanambiwa tu muanzishi wa CCM ni mwalimu nyerere, lakini ikumbukwe historia ipo siku itabainisha hili na mengine.nakumbuka kama leo siku ile ya kunganishwa ASP na TANU mzee wetu shekh Thabit Bin kombo mtumzima alitokwa na machozi machozi yale yalikuwa na maana yake .leo imefika pahala hawa watu hawataki hata kuyaeleza au kulitaja jina la mzee Aboud lakini tusijisahau kuwa hakuna aliyejiumba, hapa wanamsubiria ili waje watueleze ambayo wanataka wao tuyasikie. Mungu ampe afya nzuri mzee wetu baadhi yetu hatuto msahau kwa mazuri aliyotuletea na tupo tayari kumsamehe kwa makosa aliyofanya ambayo leo hii yanatukosesha usingizi.
Verdict. Kwa sisi Wazanzibari Mzee Jumbe, mazuri yake ni mengi kuliko yale mabaya. Ni shujaa wetu na hatutomsahau daima. Hata kina Seif na wenzake hawatamsahau Mzee Jumbe.Kama una chuki binafsi uwanja uko wazi kuzieleza. Unawezaje kuisemea Zanzibar wakati hujui chote juu yake.
Kama huku Bara Mzee ruksa alikuwa kuopowa watu kutoka kwenye njaa basi kule Zanzibar alikuwa Jumbe baada ya kuchukuwa madaraka baada ya kifo cha Karume. Ni kipindi cha Jumbe ndipo mahakama ya wazi ilifanyika kule Zanzibar. Wahaini waliendeshewa kesi kwa uwazi na kila siku ikitangazwa na kuonyeshwa kwenye TV na hukumu zilipotolewa waliohukumiwa kifo walikata rufaa na wakapunguziwa adhabu na kuwa miaka 18. La kutia maanani ni kuwa hao waliohukumiwa kifo walikiri wenyewe na kesi ya waliobaki ndio iliendelea kwa uwazi. Wacha uongo kusema kuwa Nyerere aliingilia kati kwani kama hujui huo wakati wa Nyerere kulikwishakuwa na kesi za Kubambikiziwa Uhaini mbili na hukumu za Kifo zilitolewa ingawa hazijatekelezwa.
Ni wakati wa Jumbe hii demokrasia ya kuwa na Wawakilishi aliianzisha na ni Rais pekee ukiondowa Karume mkubwa alieweka visiwa vyote viwili kwa usawa.
Kuhusu huku Bara vitu vilivyoagizwa kutoka nje kwa Zanzibarvikiishia huku Bara zikiwemo TV, sabuni na vyakula hasa wakati kabla ya vita vya wahujumu.
Mspojuwa Historia ni bora kukaa chonjo na kusoma.
Kama kuna binaadamu m-binafsi hapa Tanzania aliyewahi kuishi basi Nyerere anaongoza, si kuwa aliifuta historia ya mashujaa wengine waliotoa mali zao na roho zao kwa nchi hii bali aliwafanya wakaonekana maadui wa nchi hii, na kujigeuza yeye kwa kila sifa inayomstahiki na isiyomstahiki,mbali na Jumbe watu kama Bibi Titi Moh'd, Oscar Kambona,Kasela Bantu n.k waliomtengeneza na Kumpromote Nyerere enzi hizo, walifikia hata kutoa fedha na mali zao kumpeleka Nyerere U.N akawasemee kwa kuwa tu alijua kingereza, wengine walimbeba hata pale alipotaka kupinduliwa (Oscar kambona), shukurani za mtu huyu kwa watu wote hao ni kama za punda, aliwapiga mateke na kuwanyanyasa kama vile hakuwahi kuwajua seuza kupata hisani zao,Manyanyaso aliyomfanyia BB TT, kwa kisingizio cha kutaka kumpindua, yanasikitisha hata leo ukiyasoma tu, lau kama kungekuwa na vyombo vya habari siku hizo kama ilivyo sasa vikapaza sauti zao kwa madhila waliyofanyiwa "mashujaa waliosahaulika" nchi hii na "kufutwa" historia na michango yao ya ujenzi wa taifa hili na Mwalimu Nyerere kwa makusudi, hakuna mtu angelitoa chozi lake kwa kifo chake.
Guess what 'This move' implies to? It is the appointment of those were taken as opposition of revolution especially those from Pemba Island aong them Seif Sharifu.
In fact he tried to treat all islands at the same level but as it happened that those he trusted wanted more on the pretext of one island wellfare.