Kama Serikali haikutaka Mwenyekiti Mbowe na msafara wake wakutane na wahanga basi ingepokea misaada kwani inahitajika sana

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,285
2,043
Hakika ni Jambo la AIBU na AJABU kwa Serikali kukataa KIPOKEA MISAADA iliyopelekwa na CHADEMA kwa Watanzania wenzao waliopata JANGA la MAFURIKO na wengi kufa na wengine kulazwa huku wengine wakiendelea kutafutwa.

Na kama Serikali ilikuwa haiwataki Waliopeleka MISAADA yaani VIONGOZI wa CHADEMA basi INGEKUBALI MISAADA iliyopelekwa na CHADEMA kwa WAHANGA wanaotaka hiyo MISAADA kwani hiyo MISAADA imechangwa na Watanzania wenye Uchungu na Maafa yaliyowapata Watanzania wenzao na SIO VIONGOZI wa CHADEMA tu.

Inavyoonekana CCM imeingiza SIASA kwenye hili Janga na kusahau kuwa hata hiyo MICHANGO inayotolewa na SERIKALI ni KODI za Watanzania bila kujali ITIKADI za WALIPA KODI.

CCM iache UBAGUZI usio na TIJA kwa TAIFA kwenye MASUALA na MATUKIO MAZITO Kama haya.

Watanzania tukemee hii TABIA ya UBAGUZI kwani inatengeneza CHUKI kwa WANANCHI.
 
Hakika ni Jambo la AIBU na AJABU kwa Serikali kukataa KIPOKEA MISAADA iliyopelekwa na CHADEMA kwa Watanzania wenzao waliopata JANGA la MAFURIKO na wengi kufa na wengine kulazwa huku wengine wakiendelea kutafutwa. Na kama Serikali ilikuwa haiwataki Waliopeleka MISAADA yaani VIONGOZI wa CHADEMA basi INGEKUBALI MISAADA iliyopelekwa na CHADEMA kwa WAHANGA wanaotaka hiyo MISAADA kwani hiyo MISAADA imechangwa na Watanzania wenye Uchungu na Maafa yaliyowapata Watanzania wenzao na SIO VIONGOZI wa CHADEMA tu.Inavyoonekana CCM imeingiza SIASA kwenye hili Janga na kusahau kuwa hata hiyo MICHANGO inayotolewa na SERIKALI ni KODI za Watanzania bila kujali ITIKADI za WALIPA KODI.
CCM iache UBAGUZI usio na TIJA kwa TAIFA kwenye MASUALA na MATUKIO MAZITO Kama haya.Watanzania tukemee hii TABIA ya UBAGUZI kwani inatengeneza CHUKI kwa WANANCHI.


Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
Sasa kama chedema wanazuiwa kuwaona wahanga wa nchi yao na wanakubali kirahisi hivi ni jaribio la mamlaka kuona ikiwa watanyang'anywa uchaguzi wana ubavu wa kukataa?
Chadema kukubali hili ni dalili tosha ya kwamba wapo radhi pia kukubali kunyang'anywa ushindi katika uchaguzi.
Chadema sijui wanafeli wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa mpaka kwenye matatizo...aisee
Misaada si inaweza kutumwa tuu. Mbona wengi wanasaidia kutokea huku mbali na inafika vizuri tuu. Au lazima twende ili tupige picha tukiitoa?!

Pili zoezi linaloendelea ni uokozi na hatua za awali za resettlement kwanini tusiwape nafasi vyombo vyote vya serikali na watu wa Hanang' kufocus rasilimali muda na watu kushughulika na hitaji hili la muhimu kwanza?!

Tatu ni unawezaje kuhakikisha swala hili halitageuzwa kuwa la kisiasa?! Na ikiwa, kwa bahati mbaya; likagezwa kuwa la kisiasa tutakuwa tumefanya jambo la hovyo sana. Watu wanaumia pale, tukakae tunapokea misaada na kupiga picha na kesema Chama kile Cha hovyo... !?

Ninadhani ni uamuzi sahihi.. na hata hao wa Chama Cha Mapinduzi sitarajii Kuona wanaigeuza hii kuwa swala la kisiasa.

Kwa muda huu tuungane tuwatoe wenzetu kwenye shida; hayo mengine tutafanya baadae. Kimyakimya na bereshi lako na majembe tunaenda kusaidia.. Kama kuna misaada tuitume kwa utaratibu uliopo wa kusaidia.
 
Misaada si inaweza kutumwa tuu. Mbona wengi wanasaidia kutokea huku mbali na inafika vizuri tuu. Au lazima tupige picha tukiitoa?!

Pili zoezi linaloendelea ni uokozi na hatua za awali za resettlement kwanini tusiwape nafasi vyombo vyote na watu wa Hanang' kufocus rasilimali muda na watu kushughulika na mahitaji halisi?!

Tatu ni unawezaje kuhakikisha swala hili halitageuzwa kuwa swala kisiasa?! Na ikiwa kwa bahati mbaya likagezwa kuwa la kisiasa tutakuwa tumefanya jambo la hovyo sana. Watu waumia pale, tukakar tunapokea misaada na kupiga picha...

Ni uamuzi sahihi.. na hata hao wa Chama Cha Mapinduzi sitarajii Kuona wanaigeuza hii kuwa kitu cha kisiasa. Tuungane tuwatoe wenzetu kwenye shida mengine tutafanya baadae. Kimya kimya na beteshi na majembe twendeni tukasaidie.. Kuna misaada tuitume.
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom