Humu duniani kuna hatari nyingi sana. Hata kuweka pesa kwenye akaunti tu ni hatari kubwa. Kwani wakiamua kukitapeli wanaweza na serikali ikinyamaza hiyo itakuwa imekwisha.
Kuna wakati jamaa zangu walitapeliwa na watu wa bitcoin. Lakini nikaja kumsikia Rais wa nchi anapigia upatu mambo ya crytocurrency.
Tuna wasomi, wamepata exposure kwa gharama ya kodi zetu, lakini hawawezi kutulinda hata wakiwa serikalini.
Hatujui iwapo biashara ya crytocurrency ni ya kweli hadi tutapeliwe kwanza.
Tumekuwa wahanga wa makampuni ya kitapeli mengi yanayopata leseni na vibali vya kufanya kazi nchini. Huenda ikawa ni njia ya serikali kujiingizia kipato, lakini mi nasema ni uonevu mkubwa.
Hata hivyo baada ya kutapeliwa na Kalynda safari hii, tunasubiri kutukanwa tena kuwa hatuna akili na tuna tamaa ya pesa.
Bado makampuni ya crytocurrency yanakuja kuvuna tena mapesa ya bure kwa Watanzania. Zitatumika kauli za Rais jinsi alivyoisemea na hakuna mtu wa serikalini ataingilia kati kuokoa pesa za Watanzania.
Wakati wa Hayati Magufuli usingeona ujinga kama huu. Na hakika, kama ningekuwa Rais, ningewapoteza mmoja baada ya mwingine wanaosaidia utapeli huu. Maana huu ni ugaidi wa uchumi.
Unawafanya watu waogope kutumia fursa halali za kibiashara kimataifa, kwa kuwa hakuna usalama na serikali hailindi watu binafsi wanaohatarisha kufanya biashara kama hizi.