Kama ningekuwa Tour Guide wa Lissu hapa Dar

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,439
50,957
Ratiba yangu ya siku mbili ingekuwa hivi:

1. Soko la Samaki Feri
Chukua mwendokasi, tena anzia Mbezi, njoo nalo mpaka soko la samaki Feri, muda wa asubuhi ni mzuri zaidi maana utakutana na wateja wenzako wengi sana hapo Feri, nunua Samaki mkubwa aina ya Jodari. Zunguuka zunguuka humo sokoni wala usiwe na haraka, waulize wavuvi kama unataka kuanzisha shughuli za uvuvi ufanyeje, waulize kuna changamoto gani etc

2. Chukua Pantoni uende Kigamboni
Kata tiketi yako hapo Feri, subiria pantoni, vuka nenda zako Kigamboni huko ukanywe chai nzuri sana ya maziwa kwenye mgahawa mmoja karibu na stendi ya magari ya kwenda mji mwema. Hapa napo usiwe na haraka, kanunue bigjii kwenye duka moja la Mangi, kuna akina mama pale wanauza vitunguu siyo vibaya ukawaungisha. Zunguuka eneo lote soko la kigamboni, kisha chukua pantoni yako rudi upande wa pili

3. Nenda Mbagala Kizuiani huko Uswazi
Wewe si una mtoto wa mjomba, wa shangazi ya binamu wa baba yako anatafuta chumba eh?. Chukua madalali hapo Uingie ndani ndani uswazi ukaangalie vyumba vya kupanga, tembea huko ndanindani polepole kwa raha zako, njiani wasalimie wazee, wakubwa kwa wadogo. Ulizia bei mbalimbali za vyumba vya kupanga

4. Ukitoka mbagala chukua daladala nenda Tandale sokoni
Ukifika Tandale sokoni tena hapa ndo usitoke mapema kabisaaaa, kanunue T-Shirt na jeans, raba safiii, ukitoka hapo kuna sehemu wanauza Gahawa, kagonge vikombe vya kutosha vya kahawa na kashata

5. Kuna vingunguti soko la Mbuzi
Mheshimiwa Lissu, kama una hamu ya kula mbuzi basi chukua daladala mpaka hapo vingunguti, kamatia meee wa haja, aliyeshiba, yule ambaye CCM wanasema ni beberu, baadae fanya berbecue na wana ambao mko nao man to man kwenye kampeni. Raha jipe mwenyewe au vipi

6. Usisahau kwenda Abajalo Sinza, Ilala kuangalia mazoezi ya mpira ya Masela
Wewe si unapenda soka eh?, basi tembelea viwanja vya mpira vya masela ukaone machizi wanapiga soka

7. Ukitoka hapo kuna Soko la Manzese,
Huko kuna Singlendi kali kinyama na Sandozi, pita pale ujichukulie Singlendi kwa bei ya kishkaji

8. Nenda Mlimani City ununue Dawa ya mbu, kisha chukua daladala mpaka ubungo mawasiliano, kule nje kuna kuna protector za Simu nzuri sana, Ukifika pale tembea tembea sana tu mpaka upate protector unayoitaka

9. Usisahau kwenda soko la Tegeta pale kuna machungwa mazuri sana pale, ukitoka hapo kamata daladala mpaka makumbusho, pale unaweza kuamua kununua cover kwa ajilibya simu yako

10. Soko la buguruni kuna matikiti mazuri sana, hapo pia mheshimiwa usikose, yaani hapo unaweza kupata matikiti yale yenyewe kwa bei chee

11. Ukitoka Buguruni, nyoosha mpaka Tandika sokoni
Huko kuna nguo nzuri za akina mama, ukiamua kumletea zawadi shem huko Tandika sokoni ndo kwenyewe. Yaani pamba za huko ni za kimamtoni grade 1, Shem atafurahi sana

12. Mahakama ya ndizi pale karibu na shekilango kuna ndizi nzuri sana za bukoba, ukitoka hapo nenda stendi ya mabasi ya mkoa ukaulizie nauli ya kwenda Singida kwa sababu wewe unataka kwenda Singida kusalimia

13. Baada ya hapo unaweza kwenda Club ya Yanga pale Jangwani kukata kadi ya uanachama maana wewe pia si ni "mwananchi"?, Lakini siyo vibaya ukaenda pale kujua historia ya club yako uipendayo ya Yanga kuwa imechukua ubingwa mara ngapi, imemuua mnyama mara ngapi, Sunday Manara alifunga magoli mangapi na vitu kama hivyo. Ukitoka hapo si vibaya ukaenda club ya Simba ili kujifunza mfumo wao wa uwekezaji na kupata historia ya Mnyama. Kwani King Kibaden alivyoipiga Yanga Hattrick katika ushindi wa kihistoria wa Simba dhidi ya Yanga wa goli 6-0 wewe Lissu ulikuwa na umri gani?, basi nenda pale kaelezwe historia ya Wekundu wa Msimbazi.

14. Brother usisahau Treni ya Mwakyembe, kuanzia Posta mpaka Gongo la Mboto.
Chukua Treni ya Mwakyembe mida ya jioni jioni nenda mpaka Gongo la Mboto sokoni, Kama ukiweza kutembea mabehewa yote anzia kule kwenye kichwa cha dereva, tembea mpaka behewa la mwisho rudia tena hivi kama mara ishirini hivi ili uchague "behewa linalokufaa". Pale Gongo la mboto Sokoni kuna mikate mizuri sana, zunguuka mle sokoni polepole bila haraka, nunua mikate yako lainiii, kama ukiona vipi basi gonga supu ya pweza pale sokoni kuna supu nzuri sana

Hiyo ni ratiba ya siku mbili tu za kwanza za kuijua Dar!

Nitakupa ratiba ya siku mbili zinazofuata
 
Lissu kila analolifanya lipo very Calculated. Ni mpinzani ambaye anajua ku provoke na yupo smart kwenye masuala ya Sheria na Kanuni

Sent using Jamii Forums mobile app
CCM wamemrahisishia Lissu kampeni ya Dar.
Huu mkoa ulikuwa politically very demoralized, Sasa Wamemsaidia Lissu Kuupiga amsha amsha.

Ole wao Dar iende kwa Lissu. Wamekwisha!
 
50 Reactions
Reply
Back
Top Bottom