Kama ningekuwa Tour Guide wa Lissu hapa Dar

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
10,982
2,000
KAMA NINGEKUWA TOUR GUIDE WA LISSU HAPA DAR

From: JF Jukwaa la Siasa
Thread starter: Missile of the Nation (JF-Expert Member)

Ratiba yangu ya siku mbili ingekuwa hivi:

1. Soko la Samaki Feri
Chukua mwendokasi, tena anzia Mbezi, njoo nalo mpaka soko la samaki feri, muda wa asubuhi ni mzuri zaidi maana utakutana na wateja wenzako wengi sana hapo feri, nunua Samaki mkubwa aina ya Jodari. Zunguuka zunguuka humo sokoni wala usiwe na haraka, waulize wavuvi kama unataka kuanzisha shughuli za uvuvi ufanyeje, waulize kuna changamoto gani etc

2. Chukua Pantoni uende Kigamboni
Kata tiketi yako hapo Feri, subiria pantoni, vuka nenda zako Kigamboni huko Ukanywe Chai nzuri sana ya maziwa kwenye mgahawa mmoja karibu na stendi ya magari ya kwenda mji mwema. Hapa napo usiwe na haraka, kanunue bigjii kwenye duka moja la Mangi, kuna akina mama pale wanauza vitunguu siyo vibaya ukawaungisha. Zunguuka eneo lote soko la kigamboni, kisha chukua pantoni yako rudi upande wa pili

3. Nenda Mbagala Kizuiani huko Uswazi.
Wewe si una mtoto wa mjomba, wa shangazi ya binamu wa baba yako anatafuta chumba eh?. Chukua madalali hapo Uingie ndani ndani uswazi ukaangalie vyumba vya kupanga, tembea huko ndanindani polepole kwa raha zako, njiani wasalimie wazee, wakubwa kwa wadogo. Ulizia bei mbalimbali za vyumba vya kupanga

4. Ukitoka mbagala chukua daladala nenda Tandale sokoni.
Ukifika Tandale sokoni tena hapa ndo usitoke mapema kabisaaaa, kanunue T-Shirt na jeans, raba safiii, ukitoka hapo kuna sehemu wanauza Gahawa, kagonge vikombe vya kutosha vya kahawa na kashata

5. Kuna vingunguti soko la Mbuzi
Mheshimiwa Lissu, kama una hamu ya kula mbuzi basi chukua daladala mpaka hapo vingunguti, kamatia meee wa haja, aliyeshiba, yule ambaye CCM wanasema ni beberu, baadae fanya berbecue na wana ambao mko nao man to man kwenye kampeni. Raha jipe mwenyewe au vipi

6. Usisahau kwenda Abajalo Sinza, Ilala kuangalia mazoezi ya mpira ya Masela
Wewe si unapenda soka eh?, basi tembelea viwanja vya mpira vya masela ukaone machizi wanapiga soka

7. Ukitoka hapo kuna Soko la Manzese
Huko kuna Singlendi kali kinyama na Sandozi, pita pale ujichukulie Singlendi kwa bei ya kishkaji

8. Nenda Mlimani City
Hapo ununue Dawa ya mbu, kisha chukua daladala mpaka ubungo mawasiliano, kule nje kuna kuna protector za Simu nzuri sana, Ukifika pale tembea tembea sana tu mpaka upate protector unayoitaka

9. Usisahau kwenda soko la Tegeta pale kuna machungwa mazuri sana pale, ukitoka hapo kamata daladala mpaka makumbusho, pale unaweza kuamua kununua cover kwa ajilibya simu yako

10. Soko la Guguruni
Kuna matikiti mazuri sana, hapo pia mheshimiwa usikose, yaani hapo unaweza kupata matikiti yale yenyewe kwa bei chee

11. Mahakama ya ndizi
Pale karibu na shekilango kuna ndizi nzuri sana za bukoba, ukitoka hapo nenda stendi ya mabasi ya mkoa ukaulizie nauli ya kwenda Singida kwa sababu wewe unataka kwenda Singida kusalimia

12. Baada ya hapo unaweza kwenda Club ya Yanga
Pale Jangwani kukata kadi ya uanachama maana wewe pia si ni "mwananchi"?, Lakini siyo vibaya ukaenda pale kujua historia ya club yako uipendayo ya Yanga kuwa imechukua ubingwa mara ngapi, imemuua mnyama mara ngapi, Sunday Manara alifunga magoli mangapi na vitu kama hivyo. Ukitoka hapo si vibaya ukaenda club ya Simba ili kujifunza mfumo wao wa uwekezaji na kupata historia ya Mnyama. Kwana King Kibaden alivyoipiga Yanga Hattrick katika ushindi wa kihistoria wa Simba dhidi ya Yanga wa goli 6-0 wewe Lissu ulikuwa na umri gani?, basi nenda pale kaelezwe historia ya Wekundu wa Msimbazi.

Hiyo ni ratiba ya siku mbili tu za kwanza za kuijua Dar!

Nitakupa ratiba ya siku mbili zinazofuata
 

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
19,414
2,000
Na hapo tayri atakuwa amepata asilimia zaidi ya 50 ili awe rais?

Kweli bavicha ni fungu la kukosa!
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,832
2,000
Waliomsimamisha kampeni walifanya kosa kubwa sana. Kampeni ya kutembelea wananchi ni kubwa kuliko ya jukwaani. Aendelee kutembea kukutana na sana nchi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom