Kama ni wewe ungetokaje kwenye hichi kitanzi

Kama ni wewe ungetokaje kwenye hichi kitanzi

Mimba abebe mwingine halafu stress ziende kwa mwingine
Haya mambo yapo sana
Wajibu wake ni kumpa moyo mke wake kwani alibakwa hayakuwa mapenzi
Mwambie aaache ujinga bali amsaidie mkewe maana ndio mwenye tatizo kubwa kuliko yeye

Akae nae karibu sana na kumliwaza kila wakati badala ya yeye kujifanya kaumia sana
 
Kama ni kweli kwanini hakumuuliza hayo maswali kabla hajamuoa.
In short jamaa alikurupuka kuoa kabla hajapata taarifa muhimu za anaemuoa, mwisho wa siku anakuja kumchunguza bata ilhali ameshamla... Kunywa pombe sio option kama mke wake alibakwa na hawakuendelea kunyanduana baada ya hapo huyo mwanamke hana hatia kwenye huo mkasa ila kama kuna viashiria vya kuzagamuana hapo anaweza kuchukua hatua... Kimsingi sababu za kuendelea na ndoa ni nyingi kuliko za kuvivunja atulize akili vizuri afanye maamuzi ya moyo wake in neutral ground under no influence either ya pombe au mtu yoyote.
 
Kama amemkuta na mtoto na amekubali kuwa naye sasa tatizo Nini Ni? Ili takiwa aulize hayo kabla hawajaingia rasm katika uhusiano.,.Kila mtu anahistoria yake wengine wamepitia mambo ya kufedhehesha kuchimbua yaliuopita haina maana anajiadhibu bure tu swala la msingi Ni kuhakikusha Kama kwa Sasa mke wake Ni MUAMINIFU bac

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Habari ndugu zangu..

Nafupisha sana, na jamaa yangu mmoja ameoa single mama pasipo kujua baba wa mtoto wake ni nani japo mwanamke alimwambia jamaa kuwa baba mtoto bado yupo hai kijijini kwao.

Katika purukushani za maisha za jamaa kutaka kujua baba halisi ni nani, mkewe kwa huzuni kuu akamweleza kuwa baba mtoto ni kaka yake wa tumbo moja kabisa, na alibeba mimba baada ya kaka yake kumbaka porini wakati wameenda kuchota maji huku akimtishia kuwa atamwekea sumu kwenye chakula chake nyumbani amuue kama atasema kwa wazazi

Jamaa ambaye ndiye mume wake sasa , hakutaka kuamini ila aliitisha wazee wapande za mkewe na kuwaeleza ndipo akakalishwa chini na kuambiwa kwamba binti yetu ni kweli amezaa na kaka yake kutokana na kaka yake kum-baka, na sisi alituficha mpaka mimba ilipokua kubwa kiasi cha huwezi kuitoa na ukitoa tuliona ni kuhatarisha maisha ya binti yatu

Wao kama wazee walibidi waache tuu binti yao azae mtoto ambaye baba yake mzazi ni kaka yake wadamu kabisa ,

Jamaa hajataka kuamini mpaka sasa hivi akili yake imevurugika sana kawa mlevi kupindukia na nyumbani halali tena yeye ni kushinda baa tuu.

Jamaa kaniomba ushauri ila nimekosa cha kumshauri kabisa ukizingata tuliwakanya vijana wasioe single mama, na huyu single mama ndiyo wa aina hiyo.

Wakubwa kwa wadogo leteni ushauri wa kina ili niweze kumsaidia huyu mwamba
Aludi2 hom
 
Kama amemkuta na mtoto na amekubali kuwa naye sasa tatizo Nini Ni? Ili takiwa aulize hayo kabla hawajaingia rasm katika uhusiano.,.Kila mtu anahistoria yake wengine wamepitia mambo ya kufedhehesha kuchimbua yaliuopita haina maana anajiadhibu bure tu swala la msingi Ni kuhakikusha Kama kwa Sasa mke wake Ni MUAMINIFU bac

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Jamaa aliuliza juu juu hakuchimba sana . Sasa kaja kujua , shemej yake ndiye mume mwenzake amepata stress sana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kama ni kweli kwanini hakumuuliza hayo maswali kabla hajamuoa.
Anavyo dai aliuliza ila yeye alipo jibiwa baa mtoto yupo hai anasema alijua ni mtu wa mbali.. baada ya kuoa nakufikia kuzaa na mwanamke watoto wawili.. ndipo anakuja kujua ni kaka yake na mkewe ndiye wamezaa nae, sasa anaona maisha ni machungu sana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Ila haya maisha yana mambo mengi sana, sasa hapo atakua anamwitaje shemeji au mume mwenzake?
Hapo ndiyo balaa ilipo, yeye anasema angekua mwanaume mwingine wa mbali hakuna shida.. tatizo ni shemeji yake ndiye aliye mzalisha mkewe

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli kwenye hilo hekima na busara inahitajika na wewe kama rafiki unatakiwa uweke juhudi kubwa sana ya kumsaidia Rafiki yako asizidi kutopea ktk ulevi. Naw ujaribu kuwashirkisha wazazi wa Mwanaume na viongozi wa Dini ili musaidie huyo ndugu. Ni ngumu kuipokea lakini Rehema za Mungu zitawavusha ktk hilo.
Sawa sawa mkuu.. ngoja tujaribu kufanya kadiri inavyo wezekana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Huyo mwanamke kosa Lake nini??
Mimi kama mshauri wa rafiki yangu, mwanamke nionavyo hanakosa la moja kwa moja ila anakosa la makusudi la kutokusema wazi mapema kuwa alizaa na kaka yake wa damu moja ( shemeji yake na mume wake) .

Ila japo inarekebishika na kusameheka maana hakujitakia bali alibakwa na kaka yake,

Kwa upande wa jamaa yangu ni onavyo, yeye ni kwamba kapatwa na shambulio la kiakili na nafsi baada yakujua kuwa shemeji yake ndiye baba wa mtoto aliye zaa na mkewe.

Sasa hapo ndipo kazi ilipo ya kumuweka sawa ili aweze kukubaliana na mazingira aliyo nayo kwa sasa kwaajili ya maslai yake binafsi na watoto wake pamoja na mkewe.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni ngumu kumeza.

Namshauri jamaa akomae tu na mkewe maana yalishatokea tayari kamwe hayawezi kubadilishwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom