Kama ni wewe ungetokaje kwenye hichi kitanzi

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Habari ndugu zangu..

Nafupisha sana, na jamaa yangu mmoja ameoa single mama pasipo kujua baba wa mtoto wake ni nani japo mwanamke alimwambia jamaa kuwa baba mtoto bado yupo hai kijijini kwao.

Katika purukushani za maisha za jamaa kutaka kujua baba halisi ni nani, mkewe kwa huzuni kuu akamweleza kuwa baba mtoto ni kaka yake wa tumbo moja kabisa, na alibeba mimba baada ya kaka yake kumbaka porini wakati wameenda kuchota maji huku akimtishia kuwa atamwekea sumu kwenye chakula chake nyumbani amuue kama atasema kwa wazazi

Jamaa ambaye ndiye mume wake sasa , hakutaka kuamini ila aliitisha wazee wapande za mkewe na kuwaeleza ndipo akakalishwa chini na kuambiwa kwamba binti yetu ni kweli ame zaa na kaka yake kutokana na kaka yake kum-baka, na sisi alituficha mpaka mimba ilipokua kubwa kiasi cha huwezi kuitoa na ukitoa tuliona ni kuhatarisha maisha ya binti yetu

Wao kama wazee walibidi waache tuu binti yao azae mtoto ambaye baba yake mzazi ni kaka yake wa damu kabisa ,

Jamaa hajataka kuamini mpaka sasa hivi akili yake imevurugika sana kawa mlevi kupindukia na nyumbani halali tena yeye ni kushinda baa tuu.

Jamaa kaniomba ushauri ila nimekosa cha kumshauri kabisa ukizingatia tuliwakanya vijana wasioe single mama, na huyu single mama ndiyo wa aina hiyo.

Wakubwa kwa wadogo leteni ushauri wa kina ili niweze kumsaidia huyu mwamba
 
Habari ndugu zangu..

Nafupisha sana, na jamaa yangu mmoja ameoa single mama pasipo kujua baba wa mtoto wake ni nani japo mwanamke alimw
Mwambie aache utoto!!

Huyo MTOTO aliezaliwa ni damu yao ni sawa na wakwake tu!!

Yeye aendelee na maisha na huyo mtoto aitwe majina matatu ya kwake mwenyewe yaani haachi kitu!!

Simple sana hiyo MTOTO wa ndugu yako ni wako!!

Mwambie arudi nyumbani akapige show ya kibabe kupoza moyo!!!ACHA ujinga mwambie!!
 
IMG_8011.jpg
 
Habari ndugu zangu..

Nafupisha sana, na jamaa yangu mmoja ameoa single mama pasipo kujua baba wa mtoto wake ni nani japo mwanamke alimwambia jamaa kuwa baba mtoto bado yupo hai kijijini kwao.
😅😅😅😅🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Aiseee hizi story za incest zimekuwa nyingi sana 😆😆😆
 
Habari ndugu zangu..

Nafupisha sana, na jamaa yangu mmoja ameoa single mama pasipo kujua baba wa mtoto wake ni nani japo mwanamke alimwambia jamaa kuwa baba mtoto bado yupo hai kijijini kwao.
Kama alisha kubali kuoa single maza kwanini aendelee kumchunguza si alisha kubali ..... kwa haraka haraka bata huwa ana harisha lakini katika uhalisia bata hujisaidia siyo kwamba ana harisha ....tafakari chukua hatua
 
Hii ni chai iliyojazwa majani
Haya mambo hutokea sana, maana wajinga wanazaliwa kila siku na kila siku wanafanya besidei kuashiria kuwa wanaendelea kuishi.

Huwa hawajisumbui kutaka kuujua ukweli, wanajidanganya kuwa iki mradi mmependana basi hautakiwi kujua past. Yaani wanalazimisha watu wafuate mioyo badala ya kutumia akili wakati Biblia imeonya kuwa Moyo ni mdanganyifu hivyo watu wasifuate mioyo yao, bali akili zao.
 
Habari ndugu zangu..

Nafupisha sana, na jamaa yangu mmoja ameoa single mama pasipo kujua baba wa mtoto wake ni nani japo mwanamke alimwambia jamaa kuwa baba mtoto bado yupo hai kijijini kwao.
Kwa kweli kwenye hilo hekima na busara inahitajika na wewe kama rafiki unatakiwa uweke juhudi kubwa sana ya kumsaidia Rafiki yako asizidi kutopea ktk ulevi. Naw ujaribu kuwashirkisha wazazi wa Mwanaume na viongozi wa Dini ili musaidie huyo ndugu. Ni ngumu kuipokea lakini Rehema za Mungu zitawavusha ktk hilo.
 
Jamaa hajataka kuamini mpaka sasa hivi akili yake imevurugika sana kawa mlevi kupindukia na nyumbani halali tena yeye ni kushinda baa tuu.
Mimi mbona sioni cha kumvuruga mtu akili hapo? Mwambie jamaa yako aache kudeka huo ndio ukubwa! Kama ingekua dada alimficha kuwa ana mtoto kabla hajamuoa hapo labda jamaa angeweza ku panick. Lakini kama mtoto alikua anajua yupo, na sasa amejua kua mtoto alipatikana kwa kubakwa wala sio kwa umalaya au nini, kosa la mwanamke liko wapi?

Kwa msioelewa, haya mambo ya kubakana au kushikana nguvu maeneo ya vijijini hasa vijana wakiwa wadogo ni mambo ya kawaida sana na humalizwa kifamilia. Kijijini kwetu kuna dada kazaa na baba yake na maisha yanasonga.
 
Back
Top Bottom