Kama ni wewe ungefanyaje?

Kama ni wewe ungefanyaje?

Mkuu ulikuwa umepanda Bus gani hilo? Nimeipenda hiyo ya kufungua dirisha na kutoa kichwa nje kuchungulia kulikoni!!

Sio basi mkuu. Ni ndege..Boeing 737..Kwenye ndege hakuna kutoa kichwa nje mkuu
 
Mkuu Socratic sikukashifu kwamaana sijui kunaukweli gani katika hili, ila hililinawezeka sana kama ukichanganya bangi ya Arusha, mrungi wa meru kenya na vodka, unaweza ukapita nje ya msikiti ukasikia mapambio ya injili au ukapita baa ukasikia watu wanakemea mapepo.
 
Uko ndani ya ndege. Kukiwa na utulivu mkubwa ambapo watu wengi wanaonekana kusinzia. Umejiegemea kwenye seat yako ukitafakari hili na lile.. Ghafla unaskia sauti ya kilio cha mtoto mchanga kwa mbali.. unageuka huku na kule na unajiridhisha sauti ile unayoiskia haitoki ndani ya ndege bali nje. Unajiuliza mara mbili mbili.. unashangaa . Ghafla unajiskia ulazima wa kwenda haja ndogo, unapokaribia mlango wa choo unaanza kuhisi mle ndani kuna nyoka kibao. Unajipa ujasiri na kufungua mlango, mlango haufunguki. Unasukuma tena mlango bado haufunguki. Unapata hisia kuna nyoka mkubwa yuko mlangoni ndio maana mlango haufunguki.Unaamua kuahirisha tukio unarudi kukaa kwenye kiti chako unakutana na boonge la turbulent, unaanza kuhisi ndege inadondoka…unaangalia saa..ni saa 5 usiku na bado kuna kama masaa matano kabla ya ndege kutua. Unafungua dirisha kuangalia nje ni giza totoro, unachokishuhudia nje ni mvua kubwa na radi, pia sauti ya kilio cha kitoto kichanga inasikia Zaidi. Haraka unafunga dirisha.Unaamua kupambana na hofu kwa kujiimbisha,…Mbinguni..kuna makao mazuri sana. unaangalia pembeni unajistukia umekuwa ukiimba kwa sauti kiasi cha kuwaamsha baadhi ya abiria wenzako ambao wanakuangalia kwa jicho la kukushutumu na pia unatambua kama wimbo wenyewe unakusuta. Unaacha kuimba na kuiruhusu hofu iliyokushika itawale. Unawasha kitv unaangalia geographical location ulipo… ramani inakuonesha unapita Bermuda triangle. Unatamani ushuke.

Mkuu unachokishuhudia huko nje ni balaa, unaona bora ufunge tu dirisha

Sio basi mkuu. Ni ndege..Boeing 737..Kwenye ndege hakuna kutoa kichwa nje mkuu

Hapo kufungua dirisha ndo unatuchanganya. Kumbe boing 737 inafunguka madirisha?
 
Mkuu Socratic sikukashifu kwamaana sijui kunaukweli gani katika hili, ila hililinawezeka sana kama ukichanganya bangi ya Arusha, mrungi wa meru kenya na vodka, unaweza ukapita nje ya msikiti ukasikia mapambio ya injili au ukapita baa ukasikia watu wanakemea mapepo.

Hahaha.umenichekesha sana.wewe ni mzoefu wa hivyo vitu nini? hii kitu imetokea kweli mkuu.
 
Hapo kufungua dirisha ndo unatuchanganya. Kumbe boing 737 inafunguka madirisha?
kuna dirisha ambalo unaweza kufunga au kufungua na kuona nje. ila kuna dirisha lingine la kioo kwa nje ambalo huwezi kufungua ila unaweza kuona nje. Hii ipo hata kwenye baadhi ya nyumba za kawaida. Nadhani nimeeleweka mkuu.
 
Hii ndoto mbaya inatisha sana,badala ya kuwaza nyoka ebu jaribu kuota kuwa ulihisi kuna tembo mkubwa sana
 
Jamani wote wazima hapa?

Haya mimi nasalimia tu, nawatakieni kazi njema
 
Back
Top Bottom