Socratic
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 568
- 308
Uko ndani ya ndege. Kukiwa na utulivu mkubwa ambapo watu wengi wanaonekana kusinzia. Umejiegemea kwenye seat yako ukitafakari hili na lile.. Ghafla unaskia sauti ya kilio cha mtoto mchanga kwa mbali.. unageuka huku na kule na unajiridhisha sauti ile unayoiskia haitoki ndani ya ndege bali nje. Unajiuliza mara mbili mbili.. unashangaa .
Ghafla unajiskia ulazima wa kwenda haja ndogo, unapokaribia mlango wa choo unaanza kuhisi mle ndani kuna nyoka kibao. Unajipa ujasiri na kufungua mlango, mlango haufunguki. Unasukuma tena mlango bado haufunguki. Unapata hisia kuna nyoka mkubwa yuko mlangoni ndio maana mlango haufunguki. Unaamua kuahirisha tukio unarudi kukaa kwenye kiti chako unakutana na boonge la turbulent, unaanza kuhisi ndege inadondoka…
Unaangalia saa..ni saa 5 usiku na bado kuna kama masaa matano kabla ya ndege kutua. Unafungua dirisha kuangalia nje ni giza totoro, unachokishuhudia nje ni mvua kubwa na radi, pia sauti ya kilio cha kitoto kichanga inasikia Zaidi. Haraka unafunga dirisha.Unaamua kupambana na hofu kwa kujiimbisha,…Mbinguni..kuna makao mazuri sana.
unaangalia pembeni unajistukia umekuwa ukiimba kwa sauti kiasi cha kuwaamsha baadhi ya abiria wenzako ambao wanakuangalia kwa jicho la kukushutumu na pia unatambua kama wimbo wenyewe unakusuta. Unaacha kuimba na kuiruhusu hofu iliyokushika itawale. Unawasha kitv unaangalia geographical location ulipo… ramani inakuonesha unapita Bermuda triangle. Unatamani ushuke.