Kama ni kweli na ushahidi upo....

Hapo niki imagine nitakuwa nabashiri, kudhani, na kuhisi tu.

Sitaki kufanya hivyo na ndo maana naomba wote wanaodai Paul Makonda si jina lake wanipe ushahidi ili niridhike halafu nianze kumshukia na yeye.
Unasubiri nini na wewe kufanya Research yako kupata majawabu ?

Viashiria vi dhahiri kuwa jamaa ni Daudi Bashite.
Kama kweli ana vyeti Original tofauti na Madai ya watu kitu gani kinamzuia kujitokeza na ku Clear atmosphere ?

Mbona yule DED mteule ambaye watu walimzushia kuwa ni Manager wa hotel na ana Certificate tu ya Hotel Management Mamlaka yake ya uteuzi ilikuja na kutoa Clarifications na yeye akatoa vyeti vyake hadharani

Why ya Bashite kunakuwa na kigugumizi sana ?

Wengi wanajenga hoja based on this,watu hawana haja ya kumpeleka Mahakamani,wanataka Mamlaka yake ya uteuzi either itoe clarification ama imchinjie baharini
 
Hakuna mwenye ushahidi zaidi ya blabla tu.
Ukituhumiwa ukakaa kimya ni Dalili kuwa unachotuhumiwa ni kweli.
Its up to you to prove the other side wrong.
Mind you this is Political Game
 
Makonda hakuwa na ushahidi wa kutosha dhidi ya aliowataja na wanaomtuhumu nao hawatuonyeshi ushahidi wa tuhuma zao.

Upumbav.u pu.mbavu tu.
Na ndio Maana wengine wamemfungulia Mashataka na wengine kumlaani.
Yeye Kimyaaaaa
 
Duh!

Kama ni hivyo basi serikali nzima, viongozi wote wa kisiasa wakiwemo Mbowe, Lisu, Lema, Zito, na hata huyo Gwajima nao wangekaa pembeni, siyo?
Wanatakiwa wakae pembeni na sio hao pekee .
 

Nimependa hiyo slogan yako ya pili hapo chini. Jana nilikuwa mahakamani (mimi si "msomi" kama wanavyoitana wao), ila kilichonishangaza ni kuona mawakili (vijana wa kike na wa kiume, wao wanaitwa "juniors") wakijadiliana issue ya Makonda kwa kufanya reference kwa Mange...eti si unaona Mange kaandika! Hata Gwajima naye kasema kanisani!

Nikajiuliza sana kama wasomi wetu ndiyo hawa, ambavyo kwa uelewa wangu, tuna mamlaka kama NECTA, NACTE au TCU, ambao ndiyo wenye kuthibtisha madai hayo, kwa nini basi madai dhidi ya Makonda yasipelekwe huko? Maana hata kubadili majina sheria inaruhusu. Sasa accusers wake sijui kwa nini wako kwenye limbo kufanya yale ambayo tunadhani ni sahihi
 
Na kwanini labda ushahidi wa vyeti hauonyeshwi?

Tuliona kina Jesca Magu na matokeo yao. Ya huyu hayapo?
 
Nauliza kma Serekali haishitakiwi yle Marehemu Cristopha Mtikila hajawahi kuishitaki Serekali? mi pia sina Elimu nauliza ili nijue
 
..subiri kesi ya kikatiba ikianza cross examination ndo atabanwa mbele ya hon judge,

Akitia tu mguu, watamkaanga. Ataambiwa aseme yeye ni nani na alizaliwa lini na wapi. Then majibu yake yatapelekea probing zaidi.
 
Kesi ya jinai inaendeshwa na serikali na sio mtu binafsi.

Mwenye wajibu wa kuchunguza na kumpeleka huyo jamaa mahakamani ni serikali.
Serikali mpaka ipate malalamiko kutoka kwa walalamikaji..na mpaka sasa hakuna walalamikaji
 
Nchi ya longolongo hii,hakuna aliyetayari kutoa ushahidi hapa.Hata huyo homeboy wake mnafiki tu mbona hakusema tangu zamani?
 
Ukituhumiwa ukakaa kimya ni Dalili kuwa unachotuhumiwa ni kweli.
Its up to you to prove the other side wrong.
Mind you this is Political Game
Kwamaana hiyo Mbowe ana O kweli kwakuwa hajajibu tuhuma?
Tuacheni utani. Kwa wanasiasa ukijibu kila kitu,hutafanya kazi nyingine kwani kila ukijibu watakuletea jipya
 
Unasubiri nini na wewe kufanya Research yako kupata majawabu ?

We yako ushafanya?

Viashiria vi dhahiri kuwa jamaa ni Daudi Bashite.

Viashiria tena? Mi nataka ushahidi...sitaki viashiria. Ushahidi unao? Kama unao tuwekee basi hapa ili tumshukie kihalali maana wengine hatupendi kuonea watu na hatupendi uonevu wa aina yoyote ile.

Kama kweli ana vyeti Original tofauti na Madai ya watu kitu gani kinamzuia kujitokeza na ku Clear atmosphere ?

Kwani analazimika kujibu kila kisemwacho juu au dhidi yake?

Watu washasema kuwa hawezu kutungisha mimba...nalo unataka ajitokeze alijibu?

Watu washasema kuwa yeye ni shoga...nalo unataka ajitokeze alijibu?

Mbona yule DED mteule ambaye watu walimzushia kuwa ni Manager wa hotel na ana Certificate tu ya Hotel Management Mamlaka yake ya uteuzi ilikuja na kutoa Clarifications na yeye akatoa vyeti vyake hadharani

Huyo ni yeye na huo ulikuwa uamuzi wake.

Why ya Bashite kunakuwa na kigugumizi sana ?

Unaweza kuthibitisha kuwa yeye ni Bashite na si Makonda?

Wengi wanajenga hoja based on this

Based on what? Spite and conjencture?

watu hawana haja ya kumpeleka Mahakamani,wanataka Mamlaka yake ya uteuzi either itoe clarification ama imchinjie baharini

Na ikisema kila kitu kiko sawa mtaamini? Mtakubali? Au ndo mtazidi kuhamisha magoli?

This whole thing is dumb.
 
Na kwa taarifa yako,bunge lisipo chukua hatua stahiki dhidi ya waziri mwenye dhamana na ambae alisimamia zoezi zima la kuhakiki vyeti,,,,,tutawawajibisha sisi wananchi.
 
Ukituhumiwa ukakaa kimya ni Dalili kuwa unachotuhumiwa ni kweli.
Its up to you to prove the other side wrong.
Mind you this is Political Game

So you admit that there's no 'there there' but rather everything is politically motivated, right?
 
Hebu mtu mwenye ushahidi auweke hapa mtandaoni kwenye "Public Court " kama hamuiamini mahakama ili tuthibitishe au Mtafuteni basi huyo Paul Makonda original aseme chochote - akikosekana hata sister, baba au mjomba wapo
 

"Msomi" acha uongo bana. Hebu soma kifungu cha 99 cha Sheria ya Mwenendo wa Jinai (Criminal Procedure Act) ya Tanzania. Private prosecution ipo bana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…