Kama Ndoto Zetu Zilishindwa Kutimia, Basi Tutimize za Wanetu!

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Ni Jambo la kawaida na Ambalo kila mmoja lishamtokea yaani kuwa na zile ndoto za utotoni.
Ni Ndoto ambazo zilikuwa zinabeba ambition Halisi ya Binadamu!

Kwa sababu tofauti za kifamilia, kijamii na Hata kielimu pia wengi wetu tumeshindwa kutimiza zile ndoto zetu!

Kwa Mfano nikiwa mtoto Mdogo Galileo Galilei alikuwa idol mkubwa kwangu, Nakumbuka nilikuwa Darasa la 5 Kipindi Ambacho Kila mtu alikuja kugundua i was the Genius of my era in my Region, Kipindi ambacho hata mimi nilihisi i was Extraordinary!

Basi toka hapo Ndoto zangu zikawa Kuwa Mwanasayansi, Nikaja kuvutiwa sana na maswala ya Jiografia Japo nilikuwa mtata pia wa Hesabu na Sayansi, Nikatokea tena Kumkubali Mwanafunzi wake Galileo Galilei Yaani Nicholaus Corpenicus...kwa kitabu cha shule ya Msingi ameandikwa katika Kitabu Kinaitwa Mfumo wa Jua!

Kutokana na Changamoto za Kimaisha na Kielimu sikufanikiwa kutimiza Ndoto yangu ya Kuwa Mwanasayansi, labda ni career niliyowahi Kuipenda sana katika Maisha yangu yaani kuja kuitwa Mwanasayansi oneday!...Ndio Hivo Haijawezekana na i cant blame kwa hili Maana nafikiri hata wazazi wao hawakulielewa Hili.

Namshukuru Mwenyezi Mungu Maana Nimeishia Kuwa Engineer na nina Furaha kwa sababu ndio Mahala Ambapo Mungu Baba Amenijaalia Kufikia.

Ushauri wangu ni Huu kwa wazazi wenye Uelewa na Wenye Ndoto ya kuwajenga watoto wao katika Future Nzuri, yaani wafanye Kila liwezekanalo kutimiza ndoto za watoto wao japo Hata Kama zao Hazikufanikiwa Kutimia!

Ni vema ukaangalia Mwanao Anapenda nini katika utoto wake, kama ni Daktari basi Mjengee Mazingira Mazuri ya kuwa Daktari, kama anataka kuwa Padre mjengee mazingira Rafiki Pia!


Nawapenda Katika Kristo!

Mbarikiwe Katika Jina La Bwana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom