Kama mwanamke wako amewahi kukupa mojawapo ya maneno haya, unatakiwa kujitafakari

Mkuu upo kwa asilimia 99. Mimi nilishafanya utafiti wa kutosha na kujiridhisha, mwanamke anayetamka maneno ya aina ya hiyo kwa kurudia-rudia, mara nyingi anakuwa ameshakugeuza kama chapati bila ya wewe kujijua.

Sent from my Infinix X697 using JamiiForums mobile app
Ni kweli mkuu, lakini nilipompiga chini na mwenyewe alishangaa.
 
Kama mwanamke wako amewahi kukupa mojawapo ya maneno haya, unatakiwa kujitafakari.

"Usifikiri sitongozwi...nakuheshimu tu!"

" Usidhani nakuogopa, nakuheshimu... "

" Hata mimi naweza kufanya... lakini nimeamua kukuheshimu! "

" Nimewakataa wanaume kibao kwajili yako..."

" Nafanya hivi kwajili yako...."

Brother, hayo maneno sio credit kwako bali ni dharau. Nyuma ya dhamira yake anaamini kuwa umebahatika kuwa naye na anayafanya hayo kwa kukuhurumia. Kama ndivyo, inamaanisha kuwa anaigiza. Na maigizo yana mwisho. Mapenzi ni two-way traffic... Usikubali kuwa blackmailed!

Heshima ya kwanza ya mtu ni kwa utu wake mwenyewe. Anatakiwa kujiheshimu kwajili yake na Mungu wake, kisha wewe unufaike na hiyo heshima. Lakini kama anadhihirisha kwa matamshi yake kuwa anajiheshimu kwajili yako, basi hiyo ni kebehi. Ni suala la muda tu, heshima yake ita-expire na ataamua kuishi atakavyo.

Mwanamke anayejiheshimu, anafanya hivyo kwajili ya utu wake mwenyewe kwanza. Kwa vile anajua thamani yake. Lakini pia atajiheshimu kwajili ya Mungu wake, wazazi wake na heshima ya familia yake. Hata mkigombana ama kuachana yeye ataendelea kujiheshimu, kwasababu heshima ni sehemu ya maisha yake katika kunasibu utu wake.

Kama anajiheshimu kwajili yako, manake amechagua kuwa kifungoni. Heshima ya kweli ya mtu ni ile anayoitunza kwajili ya thamani ya utu wake mwenyewe.

Kama kuna mavazi ameamua kuyaacha kwajili yako, basi anaigiza, ipo siku yeye halisi ataibuka. Na pengine ukiwa mbali, atataka kuvaa vile atakavyo. Na ataishi katika matao yake.

Na ewe dada, hakuna haja ya kuigiza maisha. Ishi maisha yako. Acha akukubali vile ulivyo. Akujue vile ulivyo. Vaa unavyopenda, ishi unavyotaka; kunywa unachopenda; ili akikupenda akupende pamoja na mavazi yako na tabia zako. Akipenda boga, atapenda na ua lake.

Zaidi sana, jiheshimu wewe kwajili yako na sio kujiheshimu kwajili yake. Msingi wa heshima ya mtu, ni kwajili yake mwenyewe. Na kama ukifanya kwajili yake, basi iwe kwajili ya upendo wa agape na utashi wako. Isiwe kama unampa favour.

Unajua nakuheshimu?View attachment 2734624
Swala LA kuogopa kauli ya, mwanamke, niliacha zamani, hata akiniambia, unafikiri hawa watoto ni wa kwako? Mi, nauliza, oooh kumbe ni wa na ni?
Namtimua faster nyumbani,watoto nalea mwenyewe, maana sio kosa Lao,
Tena naweza hata wapeleka ulaya, waishi huko, kuhusu huduma ya mzigo, misambwanda imejaa kibao kitaa, tena inameremeta balaa
 
Muda mwingine hasira tu, wakiwa na hasira husema chochote but kama anakupenda hata asemaje bado utaona upendo wake
 
Kwenye hasira kuna mengi sana.
Wengi wetu hutoa maneno yenye huaribifu na uchungu mkubwa kwa wenzetu wakati wa hasira.

Kujidhibiti kuongea chochote wakati wa hasira ni mazoea yenye faida sana na kulinda mahusuano.
 
Kama mwanamke wako amewahi kukupa mojawapo ya maneno haya, unatakiwa kujitafakari.

"Usifikiri sitongozwi...nakuheshimu tu!"

" Usidhani nakuogopa, nakuheshimu... "

" Hata mimi naweza kufanya... lakini nimeamua kukuheshimu! "

" Nimewakataa wanaume kibao kwajili yako..."

" Nafanya hivi kwajili yako...."

Brother, hayo maneno sio credit kwako bali ni dharau. Nyuma ya dhamira yake anaamini kuwa umebahatika kuwa naye na anayafanya hayo kwa kukuhurumia. Kama ndivyo, inamaanisha kuwa anaigiza. Na maigizo yana mwisho. Mapenzi ni two-way traffic... Usikubali kuwa blackmailed!

Heshima ya kwanza ya mtu ni kwa utu wake mwenyewe. Anatakiwa kujiheshimu kwajili yake na Mungu wake, kisha wewe unufaike na hiyo heshima. Lakini kama anadhihirisha kwa matamshi yake kuwa anajiheshimu kwajili yako, basi hiyo ni kebehi. Ni suala la muda tu, heshima yake ita-expire na ataamua kuishi atakavyo.

Mwanamke anayejiheshimu, anafanya hivyo kwajili ya utu wake mwenyewe kwanza. Kwa vile anajua thamani yake. Lakini pia atajiheshimu kwajili ya Mungu wake, wazazi wake na heshima ya familia yake. Hata mkigombana ama kuachana yeye ataendelea kujiheshimu, kwasababu heshima ni sehemu ya maisha yake katika kunasibu utu wake.

Kama anajiheshimu kwajili yako, manake amechagua kuwa kifungoni. Heshima ya kweli ya mtu ni ile anayoitunza kwajili ya thamani ya utu wake mwenyewe.

Kama kuna mavazi ameamua kuyaacha kwajili yako, basi anaigiza, ipo siku yeye halisi ataibuka. Na pengine ukiwa mbali, atataka kuvaa vile atakavyo. Na ataishi katika matao yake.

Na ewe dada, hakuna haja ya kuigiza maisha. Ishi maisha yako. Acha akukubali vile ulivyo. Akujue vile ulivyo. Vaa unavyopenda, ishi unavyotaka; kunywa unachopenda; ili akikupenda akupende pamoja na mavazi yako na tabia zako. Akipenda boga, atapenda na ua lake.

Zaidi sana, jiheshimu wewe kwajili yako na sio kujiheshimu kwajili yake. Msingi wa heshima ya mtu, ni kwajili yake mwenyewe. Na kama ukifanya kwajili yake, basi iwe kwajili ya upendo wa agape na utashi wako. Isiwe kama unampa favour.

Unajua nakuheshimu?View attachment 2734624
Umenena vema sana
 
Mimi sijui nina matatizo! Ila naona ndivyo inavyotakiwa iwe.

Braza, kama anaileta nyapu ikihitajika au hata kama haihitajiki anaileta unaichakata, wewe hizo kauli wala zisikutie msongo msongoni. Kuna jamaa humu ndani aliwahi sema

Akijifanya Malaya, unamchukulia kimalaya malaya tu unakuwa huna cha kupoteza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom