bahati mbaya
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 578
- 192
Binafsi nina mifano mingi tu katika ili tatizo la kutopata watoto. Nima mfanyakazi mwenzangu alikaa ndani ya ndoa miaka 15 bila kupata mtoto mwaka wa 16 mkewe akapata mimba. Alianza kusikia kichefu chefu mara hiki sipendi mwisho wa siku wakaenda hosptali akakuta ana mimba ya miezi 5. Sasa hivi mtoto wao mkubwa anasoma shule. Mwingine naye alikaa ndani ya ndoa miaka 12 bila mimba na wala dalili za kupata mtoto. Baada ya hapo mkewe akapata mtoto. mtoto wao kwa kipindi ana miaka 5. Mwingine alikuwa rafiki yangu, alipata rafiki wa kiume wakati ana mtoto wa miaka 4, alipoanza rafiki mara uchumba familia ya mwanaume wakawa hawampendi binti kwakuwa alikuwa family friend. Walidumu katika uhusiano kwa muda wa miaka 6 hivi. Wakafunga ndoa. Mke akawa hapati mimba kipindi chote tangu rafiki hadi ndoa. Ndugu wakaanza kumsakama kuwa hazai. Binti alikuwa na kazi ya uhakika akaanza kuangaika hospital moja baada ya nyingine. Kila anakokwenda anaonekana hana tatizo lolote. Mme anagoma kwenda kwa kisingizio kuwa mbona ana mtoto? Mke alipoona manyanyaso yamezidi siku moja akagharamia safari ya kwenda Nairobi yeye na mme, bila mme kujua kuwa wanakwenda kufanya ninini. Mme alidhani wanakwenda kutombea tu? Walivyofika wakaenda kupima ikaonekana mme ndiyo tatizo la kutopata mtoto. Bwana likamshuka! Ikabidi mama apandikizwe mbegu za mmewe. Hivi ninavyowaambia wana watoto wawili wakwao na yule wa mme aliyepewa zawadi. Ushauri wangu kwako, nenda na mkeo mpime mtapata ufumbuzi wa tatizo na njia ya kukabiliana nalo.