Kama mke hazai ni vema kuachana naye?

Kama mke hazai ni vema kuachana naye?

Mutta

Senior Member
Joined
Mar 24, 2011
Posts
101
Reaction score
11
Nimeoa mke miaka SABA lakini hazai ,nifanyeje wakati nimefunga naye ndoa?Mimi nina uhakika mzima.Naombeni msaada umri unanitupa mkono
 
Mkuu, nendeni hospitali kupimwa kujua tatizo ni nini na inaweza kuwasaidia..
 
owa mke wa pili kama muislam na kam unauwezo wa kuwahudumikia wote. dini hii yetu nyepesi sana kama hujapata kwake utapata kwengine nyote mtakua happy
 
Mmeshapimwa wote? Kama hamjapimwa umejuaje kama mwenye matatizo ni yeye na si wewe!? Pole sana najua hili linakuchanganya sana kuona miaka inakimbia huku mambo yakiwa hayajipi. Kama hamjapimwa basi ni vizuri kuwaona Wataalam wa mambo ya uzazi wanaweza kuwasaidia kufikia lengo lenu la kuitwa Baba na Mama. Kila la heri.
 
Kwanza napenda nikupe pole

Ndoa si watoto,wala mali,kazi,pesa,ndugu,marafiki,elimu,dhahabu,magari,nyumba na vingine vingi unavyojua wewe hivyo vyote si ndoa.Ndoa ni makubaliano ya watu wawili mke na mume kukubaliana kuishi pamoja kwa upendo na kuvumiliana katika nyakati zote umaskini au utajiri,raha au tabu,magojwa au afya na mengineyo.

Ulikubali kumuoa mkeo kwa sababu ulimpenda na ukamchagua wewe uishi naye katika maisha yako yote,matokeo ya ndoa ni pamoja na watoto,mali,kazi na vingine vyote vitakavyokuja baada ya kuanza kuishi pamoja.

Tatizo la mke kuzaa si lako wala la mkeo maana ulimuoa kwa sababu ulimpenda na si sababu anazaa au azai,muhimu hapa ni kushirikisha watu wazima wenye hakima na si marafiki wala ndugu maana wengi ni wanafiki na pia jaribu kuonana na watu wa afya pia.

Mie nimekaa na mke wangu baada ya miaka 3 ndiyo akapata ujauzito najua inaumiza lakini hapo ndipo kipimo chako cha imani na uvumilivu wenu ulipo.Mwamini mungu funga na kuomba atakusaidia.mafanikio mengine yako katika maisha yako kwa mkeo wa ndoa.

Rafiki yangu mmoja mwezi January katikati mke wake kazaa mapacha baada ya kuishi naye kwa miaka 12 kwenye ndoa,unafikiri asingefanya uvumilivu nadhani angeweza kuona hao mapacha?aliweza kufanikiwa kiuchumi lakini Mtoto ilikuwa shida.uvumilivu ndiyo unaotakiwa katika maisha yetu.

Napenda kukutia moyo usikate tamaa na endelea kuwa mvumilivu haja ya moyo wako Mungu atakujibu,usiogope swala la umri,umri na number tu hakuna aliyeweka contract na Mungu wa hiyo hilo lisikutishe.


WEEKEND NJEMA
 
What if wewe ndio una tatizo?? Unadhani ingekuwa sawa yeye kukuacha?

Hili nalo neno.
Usimuache mkeo Mutta, soma ushuhuda wa jamii 01 unaweza kukutia moyo. Pole sana maana ni kipindi kigumu unapitia.
 
Mimi nilioa na ndani ya mwezi huo huo tayari ikanasa, ilipofikisha miezi miwili ikaleta shida hivyo dokta alishauri itolewe kwa ajili ya usalama wa mama,tulikubali ikatolewa na kupatiwa huduma zote za matibabu baada ya miezi miwili alipata tena ujauzito uliofia tumboni ndani ya mwezi mmoja,sasa nipo hapa sijui mustakabali wa maisha yetu ni nini!!inatuumiza sana mimi na mke wangu mpendwa,ila nimeahidi kuvumilia hadi mwisho.
 
Kuwa mvumilivu bado mapema Mungu ndiye muweza muombe yeye tu

Kama ni mkeo usimuache bwana utakuwa umempa mzigo mkubwa mwingine maana hapo alipo anaumia kwa hali yake ya kutozaa so kaeni mdiscus mambo yenu juu ya mtoto.IKUMBUKWE KUWA HAJAJITAFUTIA HALI HIYO YA KUTOZAA.
 
Nimeoa mke miaka SABA lakini hazai ,nifanyeje wakati nimefunga naye ndoa?Mimi nina uhakika mzima.Naombeni msaada umri unanitupa mkono

Kwanini unasema una uhakika wewe ni mzima?! Did you go for medical check up?!
Anyway, umeshawahi kumsimanga kwa tatizo la kutopata mtoto? Kama hujawahi, then Don't Do it! If you do it, nae akiwa na imani kwamba nae yupo fit, then atatafuta njia mbadala ya kukuzalia mtoto! hayo yakitokea na mtoto kuzaliwa, utajiona kidume kumbe ni mtoto wa mwenzio!
 
Ingekua wewe ungefurahia kuachwa? Umejuaje kama tatizo sio lako? Je ukimuacha then baada ya mda yeye akazaa na mtu mwingine na wewe ukiwa bado hujapata mtoto utajisikiaje?
 
Mutta, kwa namna ulivyojieleza wewe ni kati ya wanaume wanaotafuta cheap solution na huishia pabaya. Mpe mwenzio nguvu na matumaini. Shikamana naye mkapime wote. kama shida yako ni mtoto nenda fertility clinic hapo mikocheni. halahala usije ukajikuta wewe ndio mwenye matatizo. maana kwa jinsi ulivyojieleza yawezekana ulishaanza kumsema mwenzio maana unajiona 'mzima'. Ngoja nikupe ushuhuda:

Nina rafiki yangu ambaye mwaka huu anatimiza miaka 45 na hana dalilu ya mimba. Aliolewa miaka 15 iliyopita. Aliwahishika mimba mara ya kwanza ila iliharibika. Baada ya hapo hajawahi kushika mimba tena. Amehangaika kila hospitali hata marekani ameenda na kila sehemu ambapo ameambiwa inawezekana ameenda wapi. Huku mumewe akiamini yeye ni mzima. si alimpa ujauzito wa kwanza iweje leo awe na tatizo yeye wakati mimba ilimharibikia mwanamke? Basi kipindi fulani mke akiwa nje kwa kozi fupi mume kamtembelea na kaamkuta busy kumeza madawa na kufanya mazoezi kwa ajili ya kushika mimba. alimsindikiza hosp siku hiyo Dk mzungu alipomuona mumewe akasema Naam! heri umekuja maana nawe wahitaji kupimwa maana mkeo hana tatizo lolote! kumbuka bibie ameshafanya kila kipimo Dar na kila daktari anamwambia mbona wewe mzima?
Haya bila ajizi walimpima mwanaume na wakagundua yeye ndio mwenye matatizo. Mwanaume alihamaki. Hakuamini na kuja juu alifanya hivyo. hapo ndoa imeshakaa miaka 9 haina mtoto. Na mwanaume pengine alishatembeza bakora huko nje ila hapati majibu. Mwanaume akaamua kwenda hosp nyingine bila mkewe ili afanyiwe kipimo hicho. majibu yale yale. akarudi Tz kwa hamaki akaenda aga khan majibu yaleyale.
Akaamua kuamini ila kumbuka alishamfanyia vituko sana mkewe. mara kumsema vibaya kwa ndugu zake na hata marafiki zake wengi. kuwa mwanamke ni mbovu. leo hii amefundua yeye ndio problem na hawezi kufanya kitu. maana umri wake umeashaenda sana huyo baba hata akinywa dawa na akibadilisha diet imeshindikana.

kwa hiyo Mutta usikimbilie kutafuta wa nje. Ndoa ni safari ndefu sana. Na wite wawili ndio mnatengeneza ndoa ukimwingiza wa tatu utaharibu mambo. kumvuka huyo wa tatu hawezi akakusubiri wewe kisa una mke. na yeye atamtafuta wa kwake wa kumpooza ukiwa haupo. mwisho huwa mbaya.

wengi wamepata ukimwi kwa kutafuta watoto. kuna waliobahatika kupata watoto ila mara nyingi wa kusingiziwa. Mwanamke akishajua shida yako ni mtoto na kila mkifanya mapenzi hashiki mimba, atakutafutia mtoto wewe subiri uone. Yamemkuta rafiki yake mume wangu. akamwacha mkewe kisa mtoto baada ya ndoa ya miaka 3. kampata binti akamzalia mtoto ila ukimwangalua mtoto wala hawafanani hata kidogo. Amekaa miaka anataka mwingine binti kajimwaga mitaani na kamsogezea mwingine na huyu sasa kituko maana hayupo kwa mama wala baba na wala hafanani na mkubwa wake. Baba kagundua kosa afanyeje amebaki kujipooza kwa pombe. ni mlevi pindukia. mkewe qliyemwacha akapata mwanaume mwingine akashika mimba ila bahati mbaya alifariki wakati wa kujifungua.

Liwe somo kwako.
 
Nimeoa mke miaka SABA lakini hazai ,nifanyeje wakati nimefunga naye ndoa?Mimi nina uhakika mzima.Naombeni msaada umri unanitupa mkono

usimuache watoto hutoka kwa Mungu "...........mwili kurudi mavumbini maana watokana na mavumbi na roho kurudia ilikotoka"nafsi na roho hutoka kwa Mungu.
fanya maombi mazito pamoja na kuomba rehema sara alipata mtoto akiwa na miaka mia,KUNA JAMBO GANI LILILOGUMU KUMSHINDA BWANA?
 
Back
Top Bottom