Kama Mbowe kabambikiziwa kesi, vipi wenzake 3?

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,136
7,711
1. Halfani Bwire Hassan
2. Adam Hassan Kasekwa@Adamo
3. Mohamed Abdillah Lingwenya.

Hao ndio washitakiwa wanao daiwa kutumiwa na Mbowe kutekeleza vitendo vya Kigaidi na walifunguliwa Mashitaka hayo tangu mwezi wa nane mwaka 2020, tangia hapo hatukusikia popote pale viongozi wa chadema wakidai au wakishinikiza kuwa watuhumiwa hao sio Magaidi au walibambikiziwa.

Viongozi wa chama waliendelea na majukumu yao kama kawaida na Mwenyekiti akakimbilia nchi za nje akaishi huko na familia yake kwa raha mustarehe huku vijana hao wakiendelea kusota gerezani wasijue hatima yao.

Ila baada ya kukamatwa Mbowe ndipo sasa inaonekana Mbowe kabambikiziwa kesi sio Gaidi.

Hapo unajifunza nini?

Tuchukulie mfano; ikitokea Mbowe anaachiwa huru, inamaana hao wenzake 3 wataachwa waozee jela!!! maaana inaonekana tamaa ya viongozi na wafuasi bwana mkubwa Mbowe awe huru sio hao makapuku ambao kwa sasa hawana faida.

Hapa tunajifunza kuwa vijana msikubali kutumiwa vibaya.

Kwa sasa Mbowe ndio anaonekana anathamani zaidi kuliko kina Bwire.

Tuheshimu sheria, sheria haibagua, hivyo mamlaka zote lazima zihakikishe kuwa sheria haibagui maana watu wote wapo sawa mbele ya sheria bila kujali cheo au wadhifa wa mtu, Mbowe sio mtu maalumu mbele ya sheria, sheria haibagui, sio Bwire na wenzake wanafungwa pingu Mbowe anaachwa!! hio sio sawa, kama ni pingu wafungwe wote ama la wasifungwe wote.

Vijana msikubali kutumiwa vibaya, Ona mbowe alivyo daiwa kuwatumia vibaya jamaa hao halafu yeye akalala mbele.

Tuchape kazi kwa bidii.
 
Mtoa mada naona umetumwa kuwaaminisha watu unacho kiamini wewe kwa maslahi yako na tumbo lako na aliye kutuma wananchi wanafahamu na tayali Watanzania wanajua na aliye wazindua ameshaenda zake usilazimishe watu waamini unachoamini wewe.
 
Back
Top Bottom