Mahakama itoe hati ya kumkamata kiongozi wa dini aliyesema Rais amfutie kesi Mbowe

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,109
7,685
Kiongozi wa dini aliye muomba Mh. Rais amfutie kesi Mbowe na wenzake ni kosa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa ameingilia mchakato wa mahakama ktk kutoa haki.

Tamko la kiongozi huyo wa dini limeonyesha wazi kuidharau mahakama na kuingilia taratibu za mahakama.

Kiongozi huyo wa dini anafahamu wazi kuwa kesi hiyo ipo Mahakamani na inaendelea kusikilizwa na ni kosa kuizungumzia kesi iliyoko Mahakamanii lkn kwa maksudi kabisa Kiongozi huyo wa dini akaamua kutamka neno hilo la kuvuruga na kuingilia utaratibu wa mahakama.

kitendo hicho sio tu kaidharau Mahakama bali ameidhihaki na kuiona mahakama si chochote sio lolote, hivyo endapo mahakama haitochukua hatua ktk vitendo/kitendo kama hiki basi Mahakama itakuwa sio chombo cha kutoa haki.

Kama leo Vingozi wa dini wanadiriki kuto kuheshimu Muhimili wa Mahakama kwa kuomba eti Rais mfutie kesi Mbowe basi tutegemee siku nyingine pia wataomba Pia Sabaya afutiwe kesi. Tutavuruga nchi yetu kama hatuto heshimu utawla wa sheria.

Viongozi wetu wa dini tunawaonba wawe makini na matamko yao ambayo yanaweza kuleta utata na kuvuruga taratibu za nchi, wajiepushe kujiingiza kwenye mambo ya kisiasa wazi wazi kwani watatugawa sisi waumini wao, lengo la viongozi wa dini ni kutuunganisha sio kutugawa kwa misingi ya kisiasa, kama tunavyo muona baba askofu wamkula na wengine ambao mara zote wanatugwa kwa misingi ya kisiasa.

Hivyo ili kulinda uhuru na hadhi ya mahakama ni vyema Kiongozi huyo wa dini akamatwe na afikishwe mbele ya mahakama ili aweze kujibu tuhuma za kuingilia na kudhihaki taratibu za Kimahakama.

Utawala wa Sheria lazima uheshimiwe kwa kuviheshimu vyombo vyetu vilivyo pewa mamlka kwa mujibu wa Katiba.
 
Naunga mkono hoja ,haiwezekani Kama taifa kuhamishiwa kwenye mijadara ya ajabu utadhani Tanzania hii Kuna Mbowe pekee,tuna watanzania wengi Sana wenye kuhitaji huruma ya rais lakini leo hii the talk in town imekuwa juu ya huyu gaidi Mbowe ,huu Ni upuuzi.

Hao viongozi wa dini waende kuhubiri habari za uzinzi na ulevi, mambo ya sheria wawaachie Wanasheria.

Mbona sijawahi hata siku moja kuona mwanasheria akiwasemea au kuwaingilia watumishi wa mungu?
 
Mahakama ionyeshe jinsi inavo toa hiyo haki sio kutoa vitisho tu na maneno mengi "justices is not only heard but also must be seen" ni kazi ya mahakama kurejesha heshima ya mahakama sio kutoa vitisho watu sio wajinga kukumbilia kwa executive organ.
 
Naunga mkono hoja ,haiwezekani Kama taifa kuhamishiwa kwenye mijadara ya ajabu utadhani Tanzania hii Kuna Mbowe pekee,tuna watanzania wengi Sana wenye kuhitaji huruma ya rais lakini leo hii the talk in town imekuwa juu ya huyu gaidi Mbowe ,huu Ni upuuzi.

Hao viongozi wa dini waende kuhubiri habari za uzinzi na ulevi ,mambo ya sheria wawaachie Wanasheria.

Mbona sijawahi hata siku moja kuona mwanasheria akiwasemea au kuwaingilia watumishi wa mungu?

Mkuu unalipwa ??
 
Mm sijaelewa umeandika nn mwana CCM mwenzangu.

Mahakama uwafungulie mashitaka kiongozi aliyeomba kwa rais kuwa mh Mbowe aachiwe au asamehewe. Hapa mahakama itamshitaki kwa kosa gani? Kivipi ombi lake limeathiri maamuzi ya mahakama au mchakato wa kesi hii?

Umesema pia, kesi ikiwa mahakamani ni kosa kuizungumzia ila hujasema kuizungumzia ki vipi. Kwa hiyo na wewe ufunguliwe mashitaka kwa kosa la kuzungumzia kesi iliyopo mahakamani?

Mwisho umegusia mambo ya siasa, ebu fafanua uhusiano wa viongozi wa dini na wanasiasa kupitia ombi lao.

Isije kuta umevurugwa na Putin na upo kwenye MNING'INIO mkubwa.
 
Kama ombi la kiongozi huyu lingekua baya na la kupuuzwa, tusinge liona kwenye taarifa ya ikulu

Mtoa mada take care, acha uchonganishi
 
Naunga mkono hoja ,haiwezekani Kama taifa kuhamishiwa kwenye mijadara ya ajabu utadhani Tanzania hii Kuna Mbowe pekee,tuna watanzania wengi Sana wenye kuhitaji huruma ya rais lakini leo hii the talk in town imekuwa juu ya huyu gaidi Mbowe ,huu Ni upuuzi.

Hao viongozi wa dini waende kuhubiri habari za uzinzi na ulevi ,mambo ya sheria wawaachie Wanasheria.

Mbona sijawahi hata siku moja kuona mwanasheria akiwasemea au kuwaingilia watumishi wa mungu?
Kwani kinachokuuma mpaka tumbo lako la uzazi licheze ni nini? Mbowe alipita na mamako au?
 
Naunga mkono hoja ,haiwezekani Kama taifa kuhamishiwa kwenye mijadara ya ajabu utadhani Tanzania hii Kuna Mbowe pekee,tuna watanzania wengi Sana wenye kuhitaji huruma ya rais lakini leo hii the talk in town imekuwa juu ya huyu gaidi Mbowe ,huu Ni upuuzi.

Hao viongozi wa dini waende kuhubiri habari za uzinzi na ulevi ,mambo ya sheria wawaachie Wanasheria.

Mbona sijawahi hata siku moja kuona mwanasheria akiwasemea au kuwaingilia watumishi wa mungu?
Umeghafilika kweri-kweri.
 
Umasikini unaleta chuki na roho mbaya. Jamii masikini ndiyo zenye wachawi, wezi, wakabaji, wafitini na wauaji. Kuna vitu mtu akuandika najua huyu umasikini umemtawala na unsmsumbua.
 
Cha ajabu nini mbowe kuomba aachiwe ikiwa kesi yake inajulikana mwisho wake?

Ni bora aachiwe tu maana tayari inaonekana atashinda kesi, ili kukwepa aibu ya kushindwa ni bora aachiwe tu kwa maombi haya
 
Kiongozi wa dini aliye muomba Mh. Rais amfutie kesi Mbowe na wenzake ni kosa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa ameingilia mchakato wa mahakama ktk kutoa haki.

Tamko la kiongozi huyo wa dini limeonyesha wazi kuidharau mahakama na kuingilia taratibu za mahakama.

Kiongozi huyo wa dini anafahamu wazi kuwa kesi hiyo ipo Mahakamani na inaendelea kusikilizwa na ni kosa kuizungumzia kesi iliyoko Mahakamanii lkn kwa maksudi kabisa Kiongozi huyo wa dini akaamua kutamka neno hilo la kuvuruga na kuingilia utaratibu wa mahakama.

kitendo hicho sio tu kaidharau Mahakama bali ameidhihaki na kuiona mahakama si chochote sio lolote, hivyo endapo mahakama haitochukua hatua ktk vitendo/kitendo kama hiki basi Mahakama itakuwa sio chombo cha kutoa haki.

Kama leo Vingozi wa dini wanadiriki kuto kuheshimu Muhimili wa Mahakama kwa kuomba eti Rais mfutie kesi Mbowe basi tutegemee siku nyingine pia wataomba Pia Sabaya afutiwe kesi. Tutavuruga nchi yetu kama hatuto heshimu utawla wa sheria.

Viongozi wetu wa dini tunawaonba wawe makini na matamko yao ambayo yanaweza kuleta utata na kuvuruga taratibu za nchi, wajiepushe kujiingiza kwenye mambo ya kisiasa wazi wazi kwani watatugawa sisi waumini wao, lengo la viongozi wa dini ni kutuunganisha sio kutugawa kwa misingi ya kisiasa, kama tunavyo muona baba askofu wamkula na wengine ambao mara zote wanatugwa kwa misingi ya kisiasa.

Hivyo ili kulinda uhuru na hadhi ya mahakama ni vyema Kiongozi huyo wa dini akamatwe na afikishwe mbele ya mahakama ili aweze kujibu tuhuma za kuingilia na kudhihaki taratibu za Kimahakama.

Utawala wa Sheria lazima uheshimiwe kwa kuviheshimu vyombo vyetu vilivyo pewa mamlka kwa mujibu wa Katiba.

EFC04457-5C02-4A92-BEED-892C7105D5CA.jpeg
 
Back
Top Bottom