Kama Magufuli ni Bora kuliko Kikwete, Basi naamini ajaye ni bora kuliko Magufuli. Miaka 10 ikiisha aondoke

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,543
2,000
Kama baadhi ya watu wanavyoamini kuwa Rais Magufuli amefanya mambo mengi na Mazuri kuliko Kikwete, ndivyo hivyo ninavyoamini Mimi kuwa Atakayefuatia baada ya kipindi Cha miaka kumi cha uongozi wa Magufuli kumalizika, atakuwa Bora kuliko Rais wa Sasa na ataifanyia Tanzania mambo makubwa kuliko aliyoyafanya Magufuli.

Hivyo Basi miaka yake kumi ikiisha akabidhi ofisi ili mwingine akamate kijiti Kama ilivyo desturi. Niaminivyo Mimi Tanzania yenye watu zaidi ya milioni 50 tunao watu maelfu ambao Ni zaidi ya Magufuli.
 

Wamkopeka

Member
Apr 2, 2012
28
75
Acha kuingilia kazi ya Mungu.

Naamini hata Rais mwenyewe hawezi kukubaliana na comment yako, maana Mungu ndiye anawapa watu uwezo na vipaji na bahati nzuri Rais wetu anamjua Mungu pia.
Hakuna kama magufuli ,hatatokea habadani
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,048
2,000
Nchi hii watu wana matatizo, ni hatari sana kuongozwa na kiongozi anaetegemea "HISIA NA MOOD" anazoamka nazo asubuhi.

Ipo siku ataamka na "MOOD" afanye maamuzi mazito tusiotegemea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom