Kama maandishi ya risiti za kielekitronik yanafutika zina maana gani?

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Naomba nipewe ufafanuzi kuhusu hizi risiti zinazotolewa na mashine za kielekitronik za EFD ambazo hufutika baada ya muda mfupi.

Kwa mfano nilikuwa na shauri katika mahakama ya wilaya, cha kushangaza baada ya shauri hilo kumalizika na kufungua madai ya gharama nilizotumia kuendesha kesi hiyo niligundua kuwa risiti zote za EFD za shilingi 3,820,500 nilizokuwa nimetunza kwa ajili ya kumbukumbu zilikuwa zimefutika zote hazina maandishi yoyote.

Kwa maana hiyo madai yangu yamekosa uhalali baada ya kuambiwa nitafute njia ya kuwasilisha risiti nyingine.

Naomba wizara ya fedha inayohusika na suala la mashine hizi itusaidie njia mbadala itakayotusaidia kuondokana na kero kama hizi.
 
  • Thanks
Reactions: SIM
Hilo ni tatizo kubwa. Jitahidi kila unapopewa risiti za EFD, toa photocopy kisha zitunze pamoja. Angalau utaweza kuwa na kumbukumbu.
 
  • Thanks
Reactions: SIM
Pole mkuu hii ilishanitokea nilinunua bati kama mia moja nikaomba niziache pale dukani mpaka nitakapo timiza idadi ya ninazohitaji ndipo nizichukue nikapewa hizo risti za mashine siku ya kwenda kuchukua mzigo wangu nakuta zilishafutika zimebaki nyeupe peee
 
Hilo ni tatizo kubwa. Jitahidi kila unapopewa risiti za EFD, toa photocopy kisha zitunze pamoja. Angalau utaweza kuwa na kumbukumbu.
Kwa kumbukumbu tu haina tatizo, shida iko unapotaka kuzitumia kama kielelezo maana photocopy hazikubaliwi kisheria.
 
Naomba nipewe ufafanuzi kuhusu hizi risiti zinazotolewa na mashine za kielekitronik za EFD ambazo hufutika baada ya muda mfupi.

Kwa mfano nilikuwa na shauri katika mahakama ya wilaya, cha kushangaza baada ya shauri hilo kumalizika na kufungua madai ya gharama nilizotumia kuendesha kesi hiyo niligundua kuwa risiti zote za EFD za shilingi 3,820,500 nilizokuwa nimetunza kwa ajili ya kumbukumbu zilikuwa zimefutika zote hazina maandishi yoyote.

Kwa maana hiyo madai yangu yamekosa uhalali baada ya kuambiwa nitafute njia ya kuwasilisha risiti nyingine.

Naomba wizara ya fedha inayohusika na suala la mashine hizi itusaidie njia mbadala itakayotusaidia kuondokana na kero kama hizi.
Sasa fungua shauri la kuwadai TRA kwa risiti zao kufutika.
 
Kuna risiti wanatoa jamaa wa barabarani ambazo hazina maandishi lakini ni deliberate action ya rushwa. Mungu atunusuru tu kwa kweli.
 
Na mbaya zaidi zinafutika baada ya muda mfupi. Ndani ya miezi 2 au 3.
 
Naomba nipewe ufafanuzi kuhusu hizi risiti zinazotolewa na mashine za kielekitronik za EFD ambazo hufutika baada ya muda mfupi.

Kwa mfano nilikuwa na shauri katika mahakama ya wilaya, cha kushangaza baada ya shauri hilo kumalizika na kufungua madai ya gharama nilizotumia kuendesha kesi hiyo niligundua kuwa risiti zote za EFD za shilingi 3,820,500 nilizokuwa nimetunza kwa ajili ya kumbukumbu zilikuwa zimefutika zote hazina maandishi yoyote.

Kwa maana hiyo madai yangu yamekosa uhalali baada ya kuambiwa nitafute njia ya kuwasilisha risiti nyingine.

Naomba wizara ya fedha inayohusika na suala la mashine hizi itusaidie njia mbadala itakayotusaidia kuondokana na kero kama hizi.

Vile vi risiti ni very cheap, roller moja inaanzia buku 2 nakuendelea na inawezekana pia imekuwa hivo ili ku accommodate watu wa chini waweze kuzinunua., pia kuna transactions za bei ndogo , issue nyingine pia wanataka zisikae mda mrefu Maana inatakiwa iwe submitted with in 6 month after transactions . Kuna baadhi ya kampuni hawatumii zile risiti wao wanatumia invoice za kawaida (A4 size au A5) lakini zinakuwa na code chini kabisa mwa page , hizi unaweza ku print nyingi uwezavyo na zinadumu, kampuni kubwa hutumia njia hii .
 
Naomba nipewe ufafanuzi kuhusu hizi risiti zinazotolewa na mashine za kielekitronik za EFD ambazo hufutika baada ya muda mfupi.

Kwa mfano nilikuwa na shauri katika mahakama ya wilaya, cha kushangaza baada ya shauri hilo kumalizika na kufungua madai ya gharama nilizotumia kuendesha kesi hiyo niligundua kuwa risiti zote za EFD za shilingi 3,820,500 nilizokuwa nimetunza kwa ajili ya kumbukumbu zilikuwa zimefutika zote hazina maandishi yoyote.

Kwa maana hiyo madai yangu yamekosa uhalali baada ya kuambiwa nitafute njia ya kuwasilisha risiti nyingine.

Naomba wizara ya fedha inayohusika na suala la mashine hizi itusaidie njia mbadala itakayotusaidia kuondokana na kero kama hizi.
Kwa ajili ya manufaa yako ya siku zijazo.
kila risiti unayopewa ikiwezekana IPIGE PHOTO KOPI.
Hii itakusaidia kutunza kumbukumbu zako.
Wino wa EFD HUCHUCHUKA baada yakipindi fulani.
 
Pole mkuu hii ilishanitokea nilinunua bati kama mia moja nikaomba niziache pale dukani mpaka nitakapo timiza idadi ya ninazohitaji ndipo nizichukue nikapewa hizo risti za mashine siku ya kwenda kuchukua mzigo wangu nakuta zilishafutika zimebaki nyeupe peee
Mkuu ikawaje tena? Walikuelewa?
 
Ni kweli risti zinatupa shida sana mfano nimenunua mzigo dar risiti nazikusanya ili kupeleka kwa mhasibu so unashangaa zimefutika wakat zilihifadhiwa mahali salama
 
Kwa kumbukumbu tu haina tatizo, shida iko unapotaka kuzitumia kama kielelezo maana photocopy hazikubaliwi kisheria.

Wenye meno walitaka tu kutuuzia Mashine ,na wamefanikiwa kupata pesa nyingi sana.Mashine ya Usd 100 unakuja kulazimishwa kuuziwa kwa Usd 450 na papo hapo ufanisi wa hiyo Mashine haulingani na kiwango cha pesa.Ni low quality kabisa..
 
Naomba nipewe ufafanuzi kuhusu hizi risiti zinazotolewa na mashine za kielekitronik za EFD ambazo hufutika baada ya muda mfupi.

Kwa mfano nilikuwa na shauri katika mahakama ya wilaya, cha kushangaza baada ya shauri hilo kumalizika na kufungua madai ya gharama nilizotumia kuendesha kesi hiyo niligundua kuwa risiti zote za EFD za shilingi 3,820,500 nilizokuwa nimetunza kwa ajili ya kumbukumbu zilikuwa zimefutika zote hazina maandishi yoyote.

Kwa maana hiyo madai yangu yamekosa uhalali baada ya kuambiwa nitafute njia ya kuwasilisha risiti nyingine.

Naomba wizara ya fedha inayohusika na suala la mashine hizi itusaidie njia mbadala itakayotusaidia kuondokana na kero kama hizi.
Naomba msaada pia, mimi nikiandika z report inaandika error alafu in background inaprint karatasi haina maandishi, nini tatizo
 
Back
Top Bottom