Kama Lowassa ni Fisadi: Kwanini Apelekwi Mahakamani Kama Wakina Mramba Na Mgonja?

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
WanaJF,

Kwa sasa imedhihirika kuwa Lowassa ni chaguo la wengi kutokana na makundi mbalimbali ya jamii kumuomba agombee nafasi ya urais. Sio wazee, wasio wakina mama, sio mashekhe na wala sio wanafunzi ambao wana kigugumizi juu ya uwezo wa Lowassa.

Kwa kuwa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu kumesikika tetesi juu ya ufisadi wake na juu ya utajiri wake. Je, hao wanaotoa tuhuma hizi ni kwanini wasitandaze ushahidi wao na kumpeleka Mamvi mahakamani? Nadhani hili lingekuwa jambo la busara sana! Maana tulishuhudia wakina Mramba, Mgonja na wengineo wakilambishwa sakafu Mahakamani. Iweje iwe ngumu kwa Mamvi?

Ifike wakati Watanzania tuwe na nguvu na ujasiri wa kudai ushahidi. Yale mazoea ya kuendeshwa kwa hisia na dhana tuachane nayo. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tunapingana na siasa za majitaka ambazo zinaelekea kushamili nchini.

Yote kwa yote, Lowassa anakubalika, Watanzania tumpe nafasi.
 
Wana CCM Mnaoweweseka na Lowassa

Magazeti yaleo hasa Nipashe imebeba ujumbe wa wana CCM kwa makundi wakiomba Lowassa achukue form ya kugombea urais na wengine kumchangia kabisa sh million mbili kwa ajili ya kuchukua form hiyo.

Hakika wanaCCM hawa wanaweweseka kwani Lowassa hafai kuwa rais kwa sababu kuu 2

  1. Mtu anayejitajirisha kwa kutumia ofisi ya uma hafai kuwa kiongozi kwa sababu siyo mfano wa kuigwa( a role model), hakuna kitu kinaitwa utajiri wa asili, hata akiuza ngombe zake zote na za wamasai wengine hawezi kununua nyumba London.
  2. Pili umri ule na afya ile niyakumalizia urais , siyo kuanza urais.
Wana CCM tulieni chama chenu kimewatayarishieni kiongozi wa urais ambaye ni bora kabisa ambaye ataliongoza taifa hili na kulirudisha katika msingi yake waliyoiweka waasisi yani utu wa mtu ni kazi na walasiyo pesa

Ukipenda pesa huku unamadaraka ya urais huwa ina madhara makubwa mbeleni, muulize Shah wa Iran
 
Hawakukutana na Mwenzie Barabarani
 
Hemu tusaidie mkuu,

Kwa mita ya mraba moja huko London ni kama Pound ngapi? Na hiyo nyumba ya Lowassa ina mita ngapi za mraba? Nauliza haya kwa kuwa naamini lazima utakuwa umeiyona title deed ya kiwanja husika.

Tafadhali nijibu, kama huna jibu, tunarudi kule kule kwenye mambo ya hisia na dhana....mambo ambayo wenye akili huru hatupendi yatuendeshe.
 
Kama mimi ningekuwa mwana siasa ningejiunga na LOWASA kwa kuwa ndie anaeonekana kuwa na meno makali kulikowote ndani ya ccm sijaona mtu mwingine ambaye ataweza kuchukua ushindi IKIWA wapinzani hawata shinda .........
 
Hemu tusaidie mkuu,

Kwa mita ya mraba moja huko London ni kama Pound ngapi? Na hiyo nyumba ya Lowassa ina mita ngapi za mraba? Nauliza haya kwa kuwa naamini lazima utakuwa umeiyona title deed ya kiwanja husika.

Tafadhali nijibu, kama huna jibu, tunarudi kule kule kwenye mambo ya hisia na dhana....mambo ambayo wenye akili huru hatupendi yatuendeshe.

Mke wa Kaizari hatakiwi kutiliwa shaka, shaka peke yake inatosha kumpa taraka mke wa Kaizari,huyo mtu wako alijaribu kuomba urais siku za nyuma jina lake lilikatwa kwa ajili uadirifu wake ulitiliwa shaka.
 
11095402_651460818314635_8107952895787715250_n.jpg
 
Japo Lowassa ana kashfa kibao lakin nadhan ni bora kuliko kuwa na rais ambaye ni kibaraka wa familia ya kikwete, "membe"
 
Back
Top Bottom