Kama kweli ushirikina ndio sababu kubwa ya ajali nchini Tanzania basi nitasafiri tu kwa miguu!

Tukianza kuamini hivi basi kila kitu kin achokwama tutasema ni ushirikina...msije mkasema ushirikina umesababisha hata Sukari kupata...

Msomi wa kweli na hasa Mwana taaluma huheshimu sana mawazo ya Watu kisha huyafanyia Kazi na Utafiti wa kutosha kwani yawezekana ukawaona hao Madereva wapuuzi ila kuna jambo la msingi hapo la kuangaliwa kwakuwa wao ndiyo watumiaji wa muda mwingi wa hizi barabara kuliko Wewe ambaye husubiri tu Pasaka au Christmas ukahesabiwe kwenu huko Vunjo. Tatizo lenu mnataka kukwepesha kuwa USHIRIKINA hauna nafasi wakati pengine wengi wetu ni WASHIRIKINA wa KUTUKUKA. Mimi nasema kuwa hawa Madereva wana HOJA ya msingi na tujifunze kuheshimu michango ya Watu hata kama mnazidharau professions zao kwa Kigezo cha Usomi wenu wa kukariri na kununua vyeti au kutoa rushwa za namna mbalimbali.
 
Mkuu hakuna Dereva makin kama wa Bus. Tatizo route ndefu mfano Mbeya - Arusha unafikiri Dereva atatembea huo mwendo unaotaka??
Miundo mbinu yetu ndo inasababisha yote haya Dereva analazmika ku over take magar hata sita ili awah

Ukiangalia hapo chini ya UZI wangu hiki ulichokiandika nacho kilikuwa ni moja ya sababu zao mbadala hawa Madereva na wala hawakukataa ila na Wao kama watumiaji wa hivi vyombo nao wamekuja na ya kwao hivyo si vibaya na sisi tukawasikiliza na kuyatafakari kwa kina haya mambo kwani siku zote namba 10 huanza na 1.
 
Hayo waliyoyasema siyashangai, ndio dunia ilivyo. Haya nawe utairiwa TCRA wakupe onyo au adhabu sababu wengi wanapenda kutojifunza au kujua kuna mambo yapo duniani na yapo wapende wasipende.

Nchi zingine za Afrika haswa hiyo ni watakuambia ni kawaida, na kuna maajabu zaidi mtu huwezi kuamini.

Inasikitisha lakini nao hao, siku zao utimia nao wanateseka au kufa kifo kibaya. Hata ndege za abiria nazo utumika katika haya, hata chochote...
 
Ni nani wewe uliyefanya utafiti? Mlikuwa team ya watu wangapi mlio fanya tafiti hiyo? Nashauri watu wa system wawe wanaufuatilia watu kama nyie.
7a01c1e2f4c0b559b5379b0acf3722f5.jpg
hii ni ya masaa mawili yaliyopita hapa Shekilango kuingia Mabibo, huu sio uchawi ni ujinga
 
Ukiangalia hapo chini ya UZI wangu hiki ulichokiandika nacho kilikuwa ni moja ya sababu zao mbadala hawa Madereva na wala hawakukataa ila na Wao kama watumiaji wa hivi vyombo nao wamekuja na ya kwao hivyo si vibaya na sisi tukawasikiliza na kuyatafakari kwa kina haya mambo kwani siku zote namba 10 huanza na 1.
Ni kweli mkuu... Mfano yule Dereva wa city boy aliezngua ivi juz kat ni Dereva flan kiwango sana mi nshawah panda ile bus sema ndo hiyo masiala yameleta yote haya ila yuko vizur sana.

Sema wameleta UTOTO NJIANI..

Yani hata ww leo hii ukapewa uendeshe bus akili yako lazima Ivo.. Ukiendesha BUS kizee ivo huwez Pata kaz popote utaishia kukaa bench
 
Nashangaa 'Gentamizin' anashambulia yeyote anaye kosoa andiko hilo. Kwanza siye aliye leta taarifa hiyo. Hata ingekuwa ni muhtasari, muhtasari una kanuni zake achilia report (taarifa) ya uchunguzi wa jambo. Andiko hili halina vigezo, nachelea kusema ni utunzi kutoka mahali pasipo na anwani. Walio wengi huchukizwa na ajali hizi kwa madhara yanayo tokana nazo!
 
Ni kweli barabarani kuna mengi....hasa wanaosafiri usiku kucha hukutana na vibwanga vya kila aina.
Kwa mchana sijui lakini uchawi upo...na watu wanaroga ili wafanikiwe.
 
Kuna hata moja linalokwenda njombe,bukoba,mwanza au mbeya hapo?!?!
Hahahahaah Mpwa ajali ni ajali hata ikitokea nyumbani kwako ni ajali tu! Information is Power! I thought it was worth sharing!!!!
 
Watanzania tunapenda mizaha mizaha kwa kila kitu. Ije iwe siasa uchumi rasilimali na Ajali. Mizaha tu ndio maana tunapoteza ndugu zetu wengi kwenye ajali. Hata kuamini ushirikina ni mizaha tuu
 
Hata hivyo nakushukuru kwa kuusoma mpaka hapo ulipoishia katikati kwani yawezekana kwa uchawi ulionao pengine ungemalizia kuusoma wote UZI nao ungefutika " kimazingara ". Ubarikiwe kwa kuuokoa UZI wangu AMEN!
Ha ha ha wewe kweli mambo ya ushirikina umezoea yaani hata UZI nao umeuingiza katika uchawi..!?
 
Hata uwe na pesa kama nini umuhimu wa shule unabaki pale pale. Shule zetu zikitoa elimu ujinga utapungua sana na maafa yatapungua kwa hakika.
 
Ushirikina upo na ndo unaorudisha maendeleo sana ya nchi yetu na ukifuatilia utagundua watu weng wanaish maisha nje na ndoto zao na wenginr wanafarik vifo vya utata kisa haya mambo ya kishirikina na ndo unaorudisha maendeleo yetu nyuma.
 
Maana kuna watu hawapend kuona mafanikio ya wenzao ndo maana hata sishangai hao madereva kusema kuwa ushirikina ndo unaosababisha ajal
 
Tengeneza na Wewe research topic yako ukafanye na yako kisha utuletee humu hizo so called intellectual findings zako badala ya " kubwabwaja " tu. Halafu mbona unapinga sana hii kitu au na Wewe ndiyo " wale wale " mnaotutoa " makafara " kila uchao? Narudia tena hili jambo la USHIRIKINA unaweza ukalidharau ila nakuambia unaweza ukakuta hizo sababu walizozitoa hao Madereva zikawa na ukweli ila tunakataa tu kwa dhania ya kwamba siku hizi hakuna Uchawi huku yawezekana hata wengine sasa hivi hizo Elimu au Pesa zenu mmezipata au mnazipata kwa kuwafanyia " ulozi " na " makafara " wenzenu ila humu JF mnajifanya " kupovuka " kwa kupinga. Acheni UNAFIKI UCHAWI UPO NA WATANZANIA NI WAAMINI UCHAWI WAZURI TU NA NDIYO MAANA MWEZI JANUARY KUNA RIPOTI ILITOLEWA NA GAZETI LA MWANANCHI KUWA TANZANIA NI YA PILI AFRIKA KWA WITCHCRAFT BAADA YA GHANA. Msidhani Watu tunapokuja humu na " kutiririka " basi huwa ni mambulula bali tunafahamu tunachokifanya na tuna uhakika nacho.

Hata hivyo akhsante kwa kuzidi kuchangia.

Hahahahahahahahahahahahah!

Mkuu mimi namuamini Mungu na naamini ni yeye ndie alinifungulia njia ya kwenda ughaibuni kujifunza wenzetu walitutawala vipi na kisha kutuacha sisi waafrika tukiwa tunatawaliwa na "wale" ambao wao wazungu waliwaaamini kwamba wataendeleza ukoloni mamboleo.

Miaka kibao nimetembea ulimwenguni hata kabla ya kuingia JF, mimi naamini katika njia bora za kisasa za kuleta maendeleo iwe binafsi, kijamii au kitaifa.

Mimi naongea kutokana na taarifa za ajali za barabarani na chanzo chake na hizo data zinapatikana idara ya usalama barabarani.

Majeruhi wanahojiwa, vipimo vinachukuliwa na simulation au reconstruction inafanywa na inatakiwa tu mwendelezo wa semina elekezi na mafunzo mengine.

Imani za kishirikina haziwezi kuepukwa na jamii ya watanzania kwasababu wengi wanaamini kwamba bila tunguli basi umaskini au maendeleo hayawezi kuja au hata yakija ni lazima yalindwe- na zana.

Ushirikina ni sanaa na ikipata washiriki na wakaiamini kuwa ndio sehemu ya maisha, basi inakuwa si sanaa bali ni sehemu ya maisha.
 
Mkuu hakuna Dereva makin kama wa Bus. Tatizo route ndefu mfano Mbeya - Arusha unafikiri Dereva atatembea huo mwendo unaotaka??
Miundo mbinu yetu ndo inasababisha yote haya Dereva analazmika ku over take magar hata sita ili awah
Ndiyo uzembe wenyewe huo tunaouzungumzia. Halafu route ndefu mara nyingi zinakuwa na madereva wawili
 
Ushirikina ndo unaowafanya waendeshe kwa spidi?
ushirikina ndo unaowafanya waendeshe kwa kuhama hama kwa mbwembwe wakikutana?
ushirikina ndo unawafanya wajaze abiria wengi kuliko kiasi
ushirikina ndo unawafanya wabadili siti za magari na kuongeza idadi ya siti?
ushirikina ndo unaowafanya wahonge mizani na trafiki?
Yes, sababu wanakua sio wao bali ni ile roho chafu inayowaongoza kufanya mambo mabaya.
 
Back
Top Bottom