Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
KAMA ni kweli Serikali ya Rais Magufuli haihusiki na utekaji watu na imedhamiria seriously kutaka kuwajua wanaoitwa "wasiojulikana" ianze kwa kumkamata Syprian Musiba.
Musiba ameweka bayana kuwa ama anahusika au anawafahamu fika watu hao wanaoongozwa na Ibilisi.
Musiba amesema, "sisi kama wanaharakati tunaomuunga mkono na kumtetea Rais Magufuli wote wanaomtukana Rais tutawafuata popote mlipo iwe tweeter, Facebook au Instagram na tukikukamata tutahakikisha unabaki kilema. Wewe Mdude Chadema ninakuonya acha mara moja kumtukana Rais, wewe mtu mmoja ukifa watanzania 54 milioni wakabaki hakuna hasara". Maana ya maneno haya ni kwamba Musibu anajua waliomteka Mdude!
Musiba akijua waliomteka Mdude maana yake anajua waliomshambulia Lissu kwa mabunduki na anajua walipo Ben Saanane na Azory Gwanda maana wote hawa wamepotea kwa tuhuma ya kumtusi Rais jambo ambalo halijathibitishwa na mahakama.
Musiba anasema, "sisi wanaharakati tunaompigania Rais, tutapambana na wewe maana tunaona Polisi kitengo cha Cyber Crime na TCRA wameshindwa kazi". Hiki ni kiburi kilichovuka mawingu kama Musibu na wenzie wana uwezo zaidi ya Jeshi la Polisi linalotengewa fedha za walipakodi na Bunge kutulinda na Mali zetu lakini Musiba anaona wameshindwa kazi. Nani anampa kiburi kijana huyu?
Musiba amefikia hatua hata ya kuwa msemaji wa CCM na kuiamuru CCM wamfukuze uanachama Bernard Membe na iwajadili January Makamba, Hussein Bashe na Nape Nnauye. Musiba ameagiza.
Kana kwamba haitoshi, Musiba amelitaka Bunge kurekebisha Katiba ili muda wa uongozi wa Magufuli urefushwe aongoze miaka 14. Musiba hadi amevaa ujasiri wa kumtukana Membe "pumbavu" halafu anasema Magufuli amerejesha maadili ilhali anatukana watu kama Membe anayestahili kumzaa.
Naona aliamua kujipa mamlaka kusema yote haya lakini nadhani Polisi imepata pakuanzia kujua "wasiojulikana" ambayo ni wazi Musiba ni miongoni mwao! Akamatwe!
#AchaWoga2020